caxton
Senior Member
- May 8, 2015
- 145
- 149
Wadau nawasalimu,
Mke wangu ni mkorofi sana, naweza kusema hivyo, Jumapili nilikwenda kupata huduma za Barbershop iliyo mtaa wa pili kutoka mtaani kwangu, hii ni pamoja na kunyoa, scrub na mwisho nikaingizwa kwenye chumba cha massage
Wakati naendelea kufanyiwa huduma ya massage ghafla akatokea mke wangu na kuingia humo chumbani kwa nguvu pamoja na kuzuiliwa na vinyozi kuwa asiingie,akamkamata yule binti wa watu na kuanza kumpiga, na kuniamuru nivae nguo tuondoke, thank God tulisaidiana na vinyozi kumtoa shingoni mwa yule binti maana alikua amempiga kabali /roba.
Watu walijaa hapo nilifedheheka sana, maana picha iliyoonekana hapo ni kwamba nimefumaniwa kumbe sivyo.Wakati akiwa mjamzito alinisumbua sana kwa wivu, nikisimama na binti tu wa jirani hata kwa salam anazira kula, nikajua ni sababu labda ya mimba, lakini sasa ameshajifungua tangu mwezi March lakini tabia hii inaendelea, na hapa sijamuoa tunaishi tu sasa nikimuoa rasmi itakuweje?
Hivi wadau massage ina ubaya gani hadi nionekane kama vile nimeua mtu? Hadi leo hii sizungumzishwi ndani sasa kosa langu ni nini?