Kanidanganya kasafiri kumbe yupo na mwanamke mwingine

kirue

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
273
83
Mimi nilikuwa nasubiri pakuche nimalizie stress zangu hapa. Valentine day yangu ilikuwa mbaya mpaka na pete ya uchumba nimerudisha. My boyfriand anaishi Arusha ndiko alikoajiriwa mimi niko Dar es salaam,yaani sio boyfriand ni mchumba rasmi na mahari ilishatolewa. Sasa last week tuliongea kuhusu Valentine day na tukakubaliana kuwa yeye aje Dar es salaam na flight ya asubuhi jumamosi.

Then tutaenda kupata lunch somewhere baada ya hapo tutakuwa tu home kwangu hakuna kutoka na house girl wangu nikamdispatch kwa muda nikampeleka kwa mama yangu Kimara nikamwambia kuwa nitamfuata jumapili jioni nikitoka kumsindikiza bwana airport.

Sasa hiyo jumamosi mwanamke nimepamba chumba nimeenda namanga, binti nimenunua maua ya maana moja limekaa room na lingine sitting room, tafuta wine, korosho karanga popcorn yaani nilijitahidi kuyafanya mazingira yawe fresh na mapya kwangu na kwake.

Ilikuwa aje na flight ya saa tatu ndo inatoka Arusha, nikamwambia atakapokuwa anaenda airport anijulishe ili na mimi nianze kujisogeza airport maana nakaa tegeta. Kufika saa tatu akapiga simu akasema yuko airport ila flight imeahirishwa mpaka saa tano, nikamwambia poa nitafanyaje, kufika saa tano akatuma sms akasema wameambiwa ndge imekwama mwanza so mpaka saa tisa.

Ghafla machale yakanicheza, nika muuliza anasafiri na Fast jet au Prec, hakujibu, nikampigia akanikata akaniambia atapiga kuna maelekeze wanapewa nisubiri. Nikawa mpole, baadae nikampigia tena hakupokea hapo ni saa tisa kama na nusu hivi, nikamtumia message nikamwambia piga picha ya ticket then nitumie watsap, hakujibu nikaamua kuwapigia simu Prec wakasema hakuna flight iliyoahirishwa same applies to Fast jet, hapo nikajua nimeachwa kwenye mataa.

Hasira zikaanza nikipiga simu haipokelewi then anatuma sms anaandika "just message" which means hataki nimpigie ila nimtumie message, nyege zote zikaisha ghafla hasira ikasimama nikaanza kufakamia pombe mpaka nikazima nimeshtuka jana asubuhi nimelala chini sitting room naumwa kichwa haswa halafu janaume halikupiga wala kutuma sms kwangu. sasa nilipopata nguvu nikaenda mbezi kwa my mamy kumchukua house girl wangu.

Nikiwa naenda nikaingia Mlimani City kutoa hela mara nikakutana na mama mkwe mama yake na boyfriand aliyeniacha solemba Valentine day, baada ya kusalimiana akaniuliza mbona uko mwenyewe mwenzio yuko wapi, nikamuuliza nani akasema J ambaye ndio mchumba nikamuuliza kwani si yuko arusha, mama akashangaa akasema mbona jana alikuja nyumbani mchana akasema ndo ametoka airport amekuja kukusuprise.

Yaani yule mama angekuwa mjanja asingeniambia vile ila nikasema afadhali siri imefichuka kumbe jitu liko mjini kwa mwanamke mwingine mimi limenichunia na kunidanganya, nilichofanya nilivua pete yake nikampa mama yake ampelekee. Hivi ninavyoandika hapa niko Morogoro kwa rafiki yangu nimekuja jana jioni na simu zote nimezima anayejua niliko ni mama yangu tu hata baba hajui niko wapi.

Ofisini nimetuma email ya kuomba one week emergency leave. Yaani wanaume wa bongo ni noma mashauzi yote yamenikatika na hata hiyo ndoa siitaki maana tayari anamichepuka anayoipenda na kuithamini kuliko mimi, siko tayari kuingia kwenye ndoa na machozi. Hiyo ndio my 2015 Valentine day story.
 
Mh! Pole mpendwa hata lulu alipoandika wanaume wote wamezaliwa na usaliti hapa ndo tunaona ukweli halisi.
 
Hii story kuna mahali niliiona, ila ulifanya jambo la busara sana manake maisha yako ingekuwa ni majonzi tu. Ninachojiuliza ni kwa nini mwanaume anachumbia / kuoa mwanamke asiyempenda. Naombeni mwenye jibu tafadhali
 
UNGEPANGILIA AYA UZURI NA KUCHOMBEZA WITH SOME ENGLISH TERMINOLOGIES,I could have said another lara 1 in the making..

Hivi ninavyoandika hapa niko morogoro kwa rafiki yangu
nimekuja jana jioni na simu zote nimezima anayejua niliko ni
mama yangu tu hata baba hajui niko wapi. Ofisini nimetuma
email ya kuomba one week emergency leave.
naona unaishi kwa hisia sana...habari imeshasambazwa kwenye social network ...worse enough, you made the situation to be your worst nightmare based on assumptions..You could prove beyond reasonable doubts,contrary to the case...
 
Kirue hayo ni mapito tu haijarishi amekuumiza kiasi gani. shetani hakimbiwi komaa tu namaanisha endelea na shughuli zako yani asikufanye ukasimamisha shughuli zako za maendeleo ukaenda kwa friend kukaa tu ukimtafakari yeye ukiwa kazini ukichangamana na watu mawazo pia yanapungua kuliko ukijifungia peke yako.
 
The question is, utaweza kuushikilia msimamo wako wa kutokurudiana nae? Hivi sasa yupo anapanga silaha za msaada kukurudisha kundini....akija na please na sorry siku mbili unamvulia nguo ya ndani,u eti "unarudisha moyo nyuma".

Usifanye huo upuuzi.
 
sonnita

Ms Sonny, Niamani hakuna kilichoharibika, hiyo painfull ya kirue inawezekana ilikuwa mshtuko wa kwanza maishani!! Lakini matengenezo (repair) yanawezekana vizuri kbs! (visa hivi vipo sana kati yaetu "me/ke") kukimbia siyo solution tena.
Naomba tusikie upande wa pili - Tusijudge simpathy!!
 
Last edited by a moderator:
Hizo ni hasira tu....
Subiri jamaa aje akupige sound + am sorry nyingi + vikao vya familia.

Utarudi tu.
 
Back
Top Bottom