Kaniboa sana, ushauri tafadhali

Kaniboa sana, ushauri tafadhali

hili ndo tatizo la kuendekeza ngono
na kufanya ngono ndo kila kitu
hata mengine huwazi
 
Me naomba nikuulize mkuu huyo ni mchumba kweli au mdada tu ulikutana nae hapo stand ukaanza kuimbisha mpaka nauli kumlipia?
 
Unaumli gani ww?? unasumbua watu, ndio nn sasa,
 
Mlipanga nini sasa kwenye bus we mpuuzi nini? Amekukorifisha kipi amekataa kipi ulichotaka akifanye fara kweli msiletage upuuzi humu si ongea nae sasa
 
Basi mwenyew ukawa unajiona mjanja upo na Bebi na kasuluari kako ka kuchanika chanika magotini
 
Hakuna hoja ya msingi...lazima ujue, wengine hata kutapika wangetapika.Inategemea na maumbile ya mtu.
Labda kama unatafuta hoja ya kumtemesha tu.
 
iko ki
Wakuu,

Nina mgogoro wa nafsi hapa naona bora niwashilikishe kwa mawazo yenu.
Mchumba/kidoshodosho wangu kanikwaza kweli leo.Tulisafiri wote kutoka Mtwara kuja Dar na basi ya Tashrif.

Tulipanga mengi ambayo tutayafanya tukiwa safarini ili kufanya penzi letu liwe mubashara hadi nilishikwa na mchecheto na kumlipia na nauli.

Nilichokishuhudia baada ya kuanza safari ndo kimenileta kwenu wakuu hapa,ile tumetoka hata Mikindani hatujafika kwa wenyeji nahisi mnaelewa, alidondosha usingizi pono anasingiziwa nilimuacha labda nilijua uchovu wa jana na kazi za kwao lakini hadi Lindi hollah hajaamka.

Tulivyofika Kilanjelanje bado anambonjika tu namuamsha anachokisema hakieleweki, tumefika hotelini Starcom-Nangurukuru nimenunua mapochopocho ili nikajichane na mtoto eti kula akagoma anasema akila njiani anatapika daah wakati aliniahidi hadi kunilisha.

Kidume nikafakamia menu ya wawili hadi imeisha yeye ni analala tu hadi nimeshuka Mbagala sijaambulia chochote zaidi ya mimate yake iliyokuwa yamchuruzika alivyolala. Hata stori hatujapiga safari yote daaah, hapa najiuliza kwanini aliniaminisha yote yale? Nidai nauli yangu au nivunje bond kabisa?

Ushauri wenu tafadhali
toto saana mi nashindwa kukomenti chochote
 
Back
Top Bottom