Kaniacha baada ya kumtoa kimaisha

Kaniacha baada ya kumtoa kimaisha

Umeanza vizuri lakin umemaliza vibaya kwakushindwa kubalance hiv ni wanaume wangapi wamesomesha wakaachwa? Tena hiyo tabia ndo ya kike na anayezungumziwa hapo ni mwanaume mwenye tabia za kike otherwise mwanamke mwenyewe alianza kutumia nafasi vibaya huenda kwa sababu kamuwezesha basi yy ndo akawa mume anamuendesha vibaya hapo lazima aachwe shida zikiisha
Hapo unaposema nimekosea nimeedit muda mbona baada ya kuona hili si janga la jinsia moja. Karudie kusoma Mkuu

Hivyo usijali Mkuu tupo pamoja.
 
Pole sana ,hata kama alikuwa hakupendi asingefanya hivyo kabisa.
 
Mimi ni Mama wa watoto watatu, kabla ya kuoana na mume wangu nilikua na mwaaume mwingine ambaye tulikaa kwenye ndoa kwa miaka sita akafariki dunia, mimi nimemzidi mume wangu miaka mitatu, kabla ya kuoana tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi sita, nilipoona nazidini nikaamua nimuambie kuwa anioe. Alikubali kweli akanichumbia na kunioa, Mama yake hakutaka kwa madi kubwa mwanae bado mdogo na kuona kama vile namlazimisha.

Kipindi hicho alikua akiishi kwake kapanga lakini alikua hana kazi maamu, kwakua mimi nimejenga naishi kwangu mume wangu alihamia kwangu tukawa tunaishi vizuri tu na tukapata watoto wawili. Nilimtafutia kazi ikashindikana nikamfungulia biashara ambayo sasa imekua kubwa na anaweza kujitegemea. Tatizo nikuwa baada ya kumpa mtaji, kumsimamia mpaka akwa na epsa zake amekua akifanya mambo yake kimya kimya, amekua hanishirikishi, amejenga bila kuniambia, kanunua gari kimya kimya bila kuniambia.

Nikimuuliza ananiambia kuwa hanitaki, anataka kuoa mwanamke wa umri wake mwanamke anayempenda, anadai kuwa kipindi namuambia anioe ni kama nilimdanganya akilia hana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Anataka kuniacha lakini Baba yake hataki hivyo ananiambia kuwa kilichoshikilia ndoa yetu ni Baba yake tu. Nimechanganyikiwa, ana wanawake wengine na ananionyesha dhahiri hata hafichi, kibaya zaidi nasikia anataka kuoa mwanamke mwingine, nimechanganyikiwa kwani nimemtoa mbali, nishauri nifanye nini?
Pole sana dada, mapenzi kwa wengi huwa hayana akili. Huyo ni mumeo tayari huna budi kuvumilia hadi wakati wa BWANA, muombe Mungu tu, lakini ni wazi kuwa ulifanikiwa kumpata kwa kuwa alikuwa anatafuta maisha na umri wake ulikuwa mdogo so hakuwa na namna.

Kwa sasa muombe Mungu ili ajittambue na kurudi nyumbani.

Vv
 
Siwezi chezea hisia za mwanamke kiwango hicho.
Labda hajui wanawake huyo kaka.
Kwani hao wadogo ndio wana k. Tam kuliko ya kwako??? Ila mwache kwanza ajifunze
 
Hli simulio lingekuwa tamu mtu angepata upande wa pili wa shilingi kuliko kufarijiana tu na upande mmoja. Huwa siamini ktk hili kuwa from no where jamaa kaanza maisha kivyake. Kwanza najiuliza inafikiaje mwanaume unaenda kuishi nyumba aliyojenga marehemu ambaye alikuwa mume wa huyu msimulizi. Umekuta ana watoto watatu tayari unaenda kulala kwake na msimukizi amejiamini kabisa kapata mume. Mmefahamiana miezi sita tu. Huyu aliyekuoa sasa umemzidi miaka mitatu tu. Ila ulishadumu kwenye ndoa ya kwanza miaka sita! Bado nazidi kuleta picha. Kuna maisha ya leo na kutokuwepo kesho. Hivi ukiondoka leo maana kila mtu ataondoka watoto wa marehemu watafurahia mali za baba yao mzazi utakazoacha amabazo anaishi mwanaume mwingine ndani ya hiyo nyumba? Kua maswali zaidi ila nilishaona kesi kama yako mwanamke alimleta/alimuoa mwanaume mwingine kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na marehemu mumewe kilichofuata watoto walifukuzwa kama mbwa baada ya yule mama kutangulia mbele ya haki. Ungeanza maisha upya na yeye kuanzia nyumba nk walau unaweza kujihakikishia usalama kwako na wanao uliozaa kabla.
 
Siwezi chezea hisia za mwanamke kiwango hicho.
Labda hajui wanawake huyo kaka.
Kwani hao wadogo ndio wana k. Tam kuliko ya kwako??? Ila mwache kwanza ajifunze
Inaweza ikawa mihemko mkuu na sisi wanaume kuna wakati tunajua kuharibia wenzetu ujue sasa kama kitaa amekuwa story waanze kumwambia unaoaje mwanamke mwenye umri mkubwa kuliko ww, na utakuta alivumilia mwanzoni kisa hali ya maisha tu sasa kapata maneno yanamshinda afu unajua sisi hatunaga umbeya mtu anasemwa akiwepo hapo yaani ka utani ila utani ukweli, kama juzi nimekutana na maada huku kuwa wanaume wanao oa mwanamke asiye bikira ni wajinga tu, kwa mwenye akili fupi si lazima afukuze mke mkuu,
 
Ni kweli ila tunatofautiana, mimi navutiwa sana na mtu mzima hasa kama na yeye atakuwa huru kwangu huwa najiachia sana
Inaweza ikawa mihemko mkuu na sisi wanaume kuna wakati tunajua kuharibia wenzetu ujue sasa kama kitaa amekuwa story waanze kumwambia unaoaje mwanamke mwenye umri mkubwa kuliko ww, na utakuta alivumilia mwanzoni kisa hali ya maisha tu sasa kapata maneno yanamshinda afu unajua sisi hatunaga umbeya mtu anasemwa akiwepo hapo yaani ka utani ila utani ukweli, kama juzi nimekutana na maada huku kuwa wanaume wanao oa mwanamke asiye bikira ni wajinga tu, kwa mwenye akili fupi si lazima afukuze mke mkuu,
 
Anakuacha kwasababu huna tena lakumpatia kwenye hiyo relation yetu.

Alikuwa anataka pesa na wewe uliweza kumpatia sasa amekamata za kwake kwanini aendelee kuwa na wewe?

Hii ni rahisi tu kugundua.

Relationship yenu wakati mnaanza mliijenga juu ya fedha na si upendo.

Nakushauri endelea kutafuta pesa zaidi.

Hapo ulipo energy yako ipo very low. Hata ukimshawishi vipi ngumu kuwa kama mwanzo.

Elelekeza nguvu zako kwenye kutafuta hela na watoto wako.

Taratibu low energy vibrations itakuondoka na utakuwa normal.

Learn to let go of things and people that no longer serve you well. There no guarantee in life.
 
Enewei sijui nawe kama una matatizo gani, ila all in all inauma sana, maisha haya jinsi yalivyo magumu, hata ndugu hawakusaidii, marafiki sio msaada kwako, jamaa zako hawaeleweki ghafla anatokea mtu from nowhere anakupa maisha yaani mchongo wa kutengeneza utajiri wako mwenyewe, mambo yako yananyooka, ndoto zako zinaanza kumea, amani ya moyo inakujaa, unaanza kujihisi ndio wewe ni mwanaume miongoni mwa wanaume, unasahau machungu ya taabu zako, unaanza kuheshimika kwenye jamii hadi maadui zako wanakuheshimu, ghafla bin vuu unaanza kumuona shujaa wako aliyekufikisha hapo hakufai, aiseee. Inauma sana. Pole sana, let the nature decide!
 
Shida ni kuwa sio waname tu wanawafanyia wanawake bali hata wanawake wanawafanyia wanaume tena huko ndio wengi!! wengine wamesomesha, wengine wametoa mitaji ya biashara, wengine wamejena mpaka mamansion! wengine mpaka**** lakini wapi inafika siku mtu anaambiwa sikutaki. Hiyo yote ni sababu ya maandalizi ya kutafuta wachumba watu wanaendeshwa na mihemko ya miili na siyo utashi wa upendo. Pili misukmo ya jamii inayotuzunguka kama marafiki, ndugu n,k. na mwisho kubwa kuliko ni Ibilisi ambaye yuko kazini akiona ndoa iko salama lazima atafute ufa ili aingie na akishafanya makao hapo ukuta lazima ubomoke;. mfano tangu mmefunga ndoa manaom ba pamoja mara ngapi kwa week ( inatakiwa asubuhi na jioni kabla ya kulala) mnaanza na familia nzima halafu peke yenu chumbani mnaombea ndoa yenu!!! maadui wapo. yatosha
angeyafanya yote hayo nadhani asingeleta hapa uzi namna hii
 
Pole. Huu mtihani wako umenikumbusha mkasa wa Dada mmoja ambaye tunafanyakazi wote. Huyu dada aliolewa na mwanaume ambaye ni Dereva taxi, alichukuwa mkopo kazini milioni 15, akamkabidhi mumewe ili waanze ujenzi wa nyumba yao, kwakuwa mwenye nyumba walipopangisha alikuwa mtata sana. Kilichotokea ni kwamba mume alitoroka na ela zote za mkopo, kamuacha mke na mtoto mdogo wa miezi 8.
Kulaleki walahi
 
Duh pole sana my sister kwa yote yaliyokukuta ila yakupasa kukubali yaliyotokea kisha you must forget the past and remember the lesson from this situation kwan mtu akipunguziwa mitihani pia atapunguziwa na ukamilifu vile vile
 
Aikua lazima kubaki nae,bora ukae mwenyewe muhimu nenda nyumba ya ibada toa sadaka ya shukrani mshukuru Mungu kwa yote then chapa mwendo usigeuke nyuma usijaribu kuzungumzia ilo swala.Maisha bila mume/mke yanawezekana tafuta company mnakutana meza ndefu huku ukichapa kazi kwa juhudi,nikuakikishie jamaa hatokusau ktk maisha yake.
 
Kwa hiyo una watoto watanoo ...duh....ningemrithi jamaa lakini duh mi mwenyewe nina watoto kibao....
 
Tafuta namna umfilisi kiburi chote kitaisha.
 
Unaonekana ni mwanamke unayejua kupambana na maisha, pambana na maisha yako mwache afanye yake and iko siku atakupigia magoti kuomba msamaha. Although, its hard but it will give you a peace of mind na utaweza fanya makubwa zaidi ya hayo.

Kuhusu ulichotoa, amini umetoa sadaka na mungu atakulipa maradufu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom