Kaniacha baada ya kumtoa kimaisha

Kaniacha baada ya kumtoa kimaisha

hurrem_sultana

Senior Member
Joined
Sep 6, 2018
Posts
136
Reaction score
361
Mimi ni Mama wa watoto watatu, kabla ya kuoana na mume wangu nilikua na mwaaume mwingine ambaye tulikaa kwenye ndoa kwa miaka sita akafariki dunia, mimi nimemzidi mume wangu miaka mitatu, kabla ya kuoana tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi sita, nilipoona nazidini nikaamua nimuambie kuwa anioe. Alikubali kweli akanichumbia na kunioa, Mama yake hakutaka kwa madi kubwa mwanae bado mdogo na kuona kama vile namlazimisha.

Kipindi hicho alikua akiishi kwake kapanga lakini alikua hana kazi maamu, kwakua mimi nimejenga naishi kwangu mume wangu alihamia kwangu tukawa tunaishi vizuri tu na tukapata watoto wawili. Nilimtafutia kazi ikashindikana nikamfungulia biashara ambayo sasa imekua kubwa na anaweza kujitegemea. Tatizo nikuwa baada ya kumpa mtaji, kumsimamia mpaka akwa na epsa zake amekua akifanya mambo yake kimya kimya, amekua hanishirikishi, amejenga bila kuniambia, kanunua gari kimya kimya bila kuniambia.

Nikimuuliza ananiambia kuwa hanitaki, anataka kuoa mwanamke wa umri wake mwanamke anayempenda, anadai kuwa kipindi namuambia anioe ni kama nilimdanganya akilia hana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Anataka kuniacha lakini Baba yake hataki hivyo ananiambia kuwa kilichoshikilia ndoa yetu ni Baba yake tu. Nimechanganyikiwa, ana wanawake wengine na ananionyesha dhahiri hata hafichi, kibaya zaidi nasikia anataka kuoa mwanamke mwingine, nimechanganyikiwa kwani nimemtoa mbali, nishauri nifanye nini?
 
Pole sn Dada huyo inaonekana hajawahi kukupenda ht siku moja alikubali tu kuwa na ww sababu ya shida za kimaisha ila kwa kuwa ss hv shida zimeisha ndo maana hakutaki anahitaji mtu wa ndoto zake.Hiyo ni kawaida ttz ww hukujua mapema tu ungeweza kuepuka hiyo kadhia.Jiandae tu kisaikolojia kuishi peke yk "single" ulee watoto wk maana hao ndo faraja yk usitarajie mapenzi motomoto kama umri umeshakutupa mkono.
 
Mimi ni Mama wa watoto watatu, kabla ya kuoana na mume wangu nilikua na mwaaume mwingine ambaye tulikaa kwenye ndoa kwa miaka sita akafariki dunia, mimi nimemzidi mume wangu miaka mitatu, kabla ya kuoana tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi sita, nilipoona nazidini nikaamua nimuambie kuwa anioe. Alikubali kweli akanichumbia na kunioa, Mama yake hakutaka kwa madi kubwa mwanae bado mdogo na kuona kama vile namlazimisha.

Kipindi hicho alikua akiishi kwake kapanga lakini alikua hana kazi maamu, kwakua mimi nimejenga naishi kwangu mume wangu alihamia kwangu tukawa tunaishi vizuri tu na tukapata watoto wawili. Nilimtafutia kazi ikashindikana nikamfungulia biashara ambayo sasa imekua kubwa na anaweza kujitegemea. Tatizo nikuwa baada ya kumpa mtaji, kumsimamia mpaka akwa na epsa zake amekua akifanya mambo yake kimya kimya, amekua hanishirikishi, amejenga bila kuniambia, kanunua gari kimya kimya bila kuniambia.

Nikimuuliza ananiambia kuwa hanitaki, anataka kuoa mwanamke wa umri wake mwanamke anayempenda, anadai kuwa kipindi namuambia anioe ni kama nilimdanganya akilia hana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Anataka kuniacha lakini Baba yake hataki hivyo ananiambia kuwa kilichoshikilia ndoa yetu ni Baba yake tu. Nimechanganyikiwa, ana wanawake wengine na ananionyesha dhahiri hata hafichi, kibaya zaidi nasikia anataka kuoa mwanamke mwingine, nimechanganyikiwa kwani nimemtoa mbali, nishauri nifanye nini?
Mlipendana au ulimnunua? Na kama mtu hakupendi basi hakupendi tu.
 
Shida ni kuwa sio waname tu wanawafanyia wanawake bali hata wanawake wanawafanyia wanaume tena huko ndio wengi!! wengine wamesomesha, wengine wametoa mitaji ya biashara, wengine wamejena mpaka mamansion! wengine mpaka**** lakini wapi inafika siku mtu anaambiwa sikutaki. Hiyo yote ni sababu ya maandalizi ya kutafuta wachumba watu wanaendeshwa na mihemko ya miili na siyo utashi wa upendo. Pili misukmo ya jamii inayotuzunguka kama marafiki, ndugu n,k. na mwisho kubwa kuliko ni Ibilisi ambaye yuko kazini akiona ndoa iko salama lazima atafute ufa ili aingie na akishafanya makao hapo ukuta lazima ubomoke;. mfano tangu mmefunga ndoa manaom ba pamoja mara ngapi kwa week ( inatakiwa asubuhi na jioni kabla ya kulala) mnaanza na familia nzima halafu peke yenu chumbani mnaombea ndoa yenu!!! maadui wapo. yatosha
 
Hapo huna chako.
Achana naye tafuta maisha yako.

Siku zote ukitaka kujua tabia halisi ya mwanadamu ni pale anapofanikiwa kupata fedha au umaarufu.
Fanya mpango utafute maisha yako.

Pole sana.
 
Pole. Huu mtihani wako umenikumbusha mkasa wa Dada mmoja ambaye tunafanyakazi wote. Huyu dada aliolewa na mwanaume ambaye ni Dereva taxi, alichukuwa mkopo kazini milioni 15, akamkabidhi mumewe ili waanze ujenzi wa nyumba yao, kwakuwa mwenye nyumba walipopangisha alikuwa mtata sana. Kilichotokea ni kwamba mume alitoroka na ela zote za mkopo, kamuacha mke na mtoto mdogo wa miezi 8.
 
Pole mwaya inaumiza ila ndio hakuna jinsi sababu kwa ulivyoandika ni dhahiri kwamba hana hata chembe ya mapenzi kwako na kiunganishi kilikuwa shida zake tu na kwa kuwa zimekwisha basi huna thamani tena.

Mie nionavyo Chukulia hiyo ni Changamoto katika maisha hivyo huna budi kusonga mbele na kuangalia maisha yako wewe na wanao na si kurudi nyuma.

Ila baadhi ya binadamu Mungu anawaona aisee Maana waeza kuta mtu kajitolea kwa kila hali ili tu mtu usimame lakini mwisho wa siku yule aliyemsimamisha sasa anaonekana si lolote si chochote. Aiseeeeee tuachage hizi tabia sababu hata na sisi Ke tunazo sana tu.
 
Duuh. Ama kweli pesa mwana haramu yaani jamaa alisahau yote mazuri kisa pesa tu na waeza shangaa hata hazikumsaidia kitu zaidi ya kuzifuja mpaka zikaisha.

Sababu ni za dhulma.
 
Mimi ni Mama wa watoto watatu, kabla ya kuoana na mume wangu nilikua na mwaaume mwingine ambaye tulikaa kwenye ndoa kwa miaka sita akafariki dunia, mimi nimemzidi mume wangu miaka mitatu, kabla ya kuoana tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi sita, nilipoona nazidini nikaamua nimuambie kuwa anioe. Alikubali kweli akanichumbia na kunioa, Mama yake hakutaka kwa madi kubwa mwanae bado mdogo na kuona kama vile namlazimisha.

Kipindi hicho alikua akiishi kwake kapanga lakini alikua hana kazi maamu, kwakua mimi nimejenga naishi kwangu mume wangu alihamia kwangu tukawa tunaishi vizuri tu na tukapata watoto wawili. Nilimtafutia kazi ikashindikana nikamfungulia biashara ambayo sasa imekua kubwa na anaweza kujitegemea. Tatizo nikuwa baada ya kumpa mtaji, kumsimamia mpaka akwa na epsa zake amekua akifanya mambo yake kimya kimya, amekua hanishirikishi, amejenga bila kuniambia, kanunua gari kimya kimya bila kuniambia.

Nikimuuliza ananiambia kuwa hanitaki, anataka kuoa mwanamke wa umri wake mwanamke anayempenda, anadai kuwa kipindi namuambia anioe ni kama nilimdanganya akilia hana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Anataka kuniacha lakini Baba yake hataki hivyo ananiambia kuwa kilichoshikilia ndoa yetu ni Baba yake tu. Nimechanganyikiwa, ana wanawake wengine na ananionyesha dhahiri hata hafichi, kibaya zaidi nasikia anataka kuoa mwanamke mwingine, nimechanganyikiwa kwani nimemtoa mbali, nishauri nifanye nini?
Usichanganyikiwe kisa umemtoa mbali changanyikiwa kisa unampenda japo ukweli unauma lakin huyo mtu amesema ukweli so angalia ww unapokosea ujirekebishe ikishindikana basi let him go it was not made to be ni shida ndo zilimleta sio mapenzi
 
Mimi ni Mama wa watoto watatu, kabla ya kuoana na mume wangu nilikua na mwaaume mwingine ambaye tulikaa kwenye ndoa kwa miaka sita akafariki dunia, mimi nimemzidi mume wangu miaka mitatu, kabla ya kuoana tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi sita, nilipoona nazidini nikaamua nimuambie kuwa anioe. Alikubali kweli akanichumbia na kunioa, Mama yake hakutaka kwa madi kubwa mwanae bado mdogo na kuona kama vile namlazimisha.

Kipindi hicho alikua akiishi kwake kapanga lakini alikua hana kazi maamu, kwakua mimi nimejenga naishi kwangu mume wangu alihamia kwangu tukawa tunaishi vizuri tu na tukapata watoto wawili. Nilimtafutia kazi ikashindikana nikamfungulia biashara ambayo sasa imekua kubwa na anaweza kujitegemea. Tatizo nikuwa baada ya kumpa mtaji, kumsimamia mpaka akwa na epsa zake amekua akifanya mambo yake kimya kimya, amekua hanishirikishi, amejenga bila kuniambia, kanunua gari kimya kimya bila kuniambia.

Nikimuuliza ananiambia kuwa hanitaki, anataka kuoa mwanamke wa umri wake mwanamke anayempenda, anadai kuwa kipindi namuambia anioe ni kama nilimdanganya akilia hana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Anataka kuniacha lakini Baba yake hataki hivyo ananiambia kuwa kilichoshikilia ndoa yetu ni Baba yake tu. Nimechanganyikiwa, ana wanawake wengine na ananionyesha dhahiri hata hafichi, kibaya zaidi nasikia anataka kuoa mwanamke mwingine, nimechanganyikiwa kwani nimemtoa mbali, nishauri nifanye nini?
Mwache aende Mungu atakupa mwingine, hata ukikaa nae kwa sasa atakuumiza tu
 
Pole mwaya inaumiza ila ndio hakuna jinsi sababu kwa ulivyoandika ni dhahiri kwamba hana hata chembe ya mapenzi kwako na kiunganishi kilikuwa shida zake tu na kwa kuwa zimekwisha basi huna thamani tena.

Mie nionavyo Chukulia hiyo ni Changamoto katika maisha hivyo huna budi kusonga mbele na kuangalia maisha yako wewe na wanao na si kurudi nyuma.

Ila baadhi ya binadamu Mungu anawaona aisee Maana waeza kuta mtu kajitolea kwa kila hali ili tu mtu usimame lakini mwisho wa siku yule aliyemsimamisha sasa anaonekana si lolote si chochote. Aiseeeeee tuachage hizi tabia sababu hata na sisi Ke tunazo sana tu.
Umeanza vizuri lakin umemaliza vibaya kwakushindwa kubalance hiv ni wanaume wangapi wamesomesha wakaachwa? Tena hiyo tabia ndo ya kike na anayezungumziwa hapo ni mwanaume mwenye tabia za kike otherwise mwanamke mwenyewe alianza kutumia nafasi vibaya huenda kwa sababu kamuwezesha basi yy ndo akawa mume anamuendesha vibaya hapo lazima aachwe shida zikiisha
 
It seems ulitumia influence ya hela kumpata na yeye alitaka ku kutumia Ili afanikiwe usiumie wala kumforce arudi huyo hakukupenda from begining tulia ulee wanao maumivu yakipoa tafta mtu mzima aliyefiwa na mke akuzidi umri uta enjoy life. Pole sana hasa ukiwekeza upendo na nguvu. Nakuombea Mungu akufanyie wepesi
 
katika haya maisha nimegundua kitu kimoja kama ni kuinuka kimaisha jiinue mwenyewe. fanya maendeleo yote kwako ila kama utamsaidia mtu toa tu sadaka ambayo hata binafsi haitakuumiza. binadamu ni watu wa ajabu sana pole sana dada.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom