Kangi Lugola unalijua hili!?

Kangi Lugola unalijua hili!?

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
43,279
Reaction score
51,700
Inaandikwa katika JF Ajali: Mabasi ya Kampuni ya Newforce Enterprises yagongana maeneo ya Ruaha Mbuyuni - JamiiForums

Mabasi mengi sana yanapakia abiria zaidi ya viwango vilivyoidhishwa na hakuna askari wa usalama barabarani wanaolisimamia hilo yawezekana kwasababu ya rushwa au urafiki na madereva wa mabasi husika

Naomba kujua mikanda ya usalama inayosisitizwa kwa kila abiria kufungwa wawapo safarini ipo wapi kwa abiria hawa?
20181012_091304.jpg


Au kikosi chako cha usalama barabarani kipo kwenye maigizo, ningekuwa mimi, moja ya maeneo ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza ingekuwa kwenye mabasi ili niwanusuru wasafiri wa aina hii, kutokana na ukaguzi huo ningebaini askari wa usalama wa barabarani wazembe kwa kuwahoji kama wameona ujazaji huo au la, je wamechukua hatua gani baada ya kuona.

Kiukweli abiria hawa huwa hawana tiketi, fedha inayopatikana haikatwi kodi hivyo serikali inapata hasara kibwa kutokana na hilo, lakini pia ukitazama picha za ajali ya mabasi ya New Force utaelewa kitu tunachokutahadharisha nacho hapa.

Nawasilisha
 
Halafu hawa NEW FORCE hawajafunga GAVANA,bado wanakimbia vile vile sijui hawaonwi!!!!!
 
Halafu hawa NEW FORCE hawajafunga GAVANA,bado wanakimbia vile vile sijui hawaonwi!!!!!

Yawezakana kabisa kuna kitengo kimezembea, ama rushwa bado ipo kazini, hapa ndipo vyombo vya habari vingekuwa vinawafuata wahusika na kuwahoji juu ya hizo double standards
 
Yawezakana kabisa kuna kitengo kimezembea, ama rushwa bado ipo kazini, hapa ndipo vyombo vya habari vingekuwa vinawafuata wahusika na kuwahoji juu ya hizo double standards
Naww unaamini hawajafunga!?
 
Haya Mabasi ya New Force kwani yanamilikiwa na nani hadi yaogopwe kuchukuliwa hatua za kisheria?

Kila leo kuna malalamiko dhidi yao ila sijawahi kusikia hatua stahiki dhidi yao.
 
Jibu safi sana hili,tunaona magari mengine tukipanda hayana mwendo kabisa,lakini New Force wanatupita kama tumepaki.


Mkuu ukiona mtu anashupalia kupinga jambo linaloshuhudiwa na wengi ujue ama yeye ni mhusika au ana mtu wake wa karibu anhusika na kukiukwa kwa sheria
 
Haya Mabasi ya New Force kwani yanamilikiwa na nani hadi yaogopwe kuchukuliwa hatua za kisheria?

Kila leo kuna malalamiko dhidi yao ila sijawahi kusikia hatua stahiki dhidi yao.


Nasikia ni wachina wapo Dar, yawezekana wametempana systems za ving'amuzi vya mwendo mkuu
 
Ni kweli tunatofautiana sana mitazamo, lakini mwisho wa siku tunakuwa wamoja linapotokea janga
Yes likitokea janga.
Lakini utashangaa siku 1 na wewe ukatamani ukae hapo au usimame kwenye bus ili tu usafiri muda huo.
 
Back
Top Bottom