GE2025 Kangi Lugola: Samia ni jembe si jembe?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwibara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Alphaxard Kangi Lugola amepanda jukwaani kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Mara waliojitokeza kumpokea Mgombea Mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi leo Agosti 30, 2025 mara baada ya kuwasili mkoani Mara.

Kama kawaida, yake Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa zamani, amewauliza mara kadhaa Wana-Mara: “Rais Samia ni jembe, si jembe?” Umati wa watu ukawa unaitikia; “Ni jembe.”

Dkt. Nchimbi ambaye anamnadi mgombea urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan na ilani ya uchaguzi ya chama hicho, katika msafara wake mkoani Mara ameambatana na wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali ya mkoa huo; Dkt. Charles Mahera (Butiama), Profesa Sospeter Muhongo (Musoma Vijijini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Boniphace Getere (Bunda Vijijini) na Mgore Kigera (Musoma Mjini).

Soma Pia:
 
Huyu mzee simpendi kichizi yan toka enzi za Magufuli ana mambo ya kiwaki
 
Nikikumbuka ile siku Lugumi amejibanza kwenye kachocho kadogo anawatafuta marafiki zake Kangi kwa simu wamwambie wakutane ata nje ya nchi apokee 200m+ ili afute kauli amri ya kutaka Lugumi atiwe ndani.

Nimeamini kweli Kangi na mama nyie ni marafiki na mmetoka mbali sana; hii nchi ina wanasiasa matapeli na wanafiki kwa kiwango cha juu sana hapa Duniani.
 
Back
Top Bottom