Kangi Lugola: Nitamshangaa mbunge wa CCM atakayepitisha bajeti hii ya maji

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,941
19,130
Mbunge mtata Kangi Lugola ameanza kwa kumfagilia rais Magufuli, kisha akaanza kumvaa waziri wa maji kwa kupunguza bajeti na kutokuweka fedha ya tozo ya maji na kumwambia asipoweka basi ajiandae kugeuzwa maji na Magufuli kwani rais aliahidi hivyo.

Amesema wabunge watakaopitisha bajeti hiyo wakati haijaongezwa pesa ya tozo ya shilingi 50 basi ataitisha mwenge kuwaelezea wananchi usaliti wao na kuwaambia waache ushabiki kwenye bajeti hiyo na kupitisha bajeti ambazo hazitekelezeki

Bajeti hii ya maji ni mbovu kabisa..

Haielezi Mipango ya kuondoa shida ya maji kwa mamilioni ya Watanzania.

Ovyo kabisa.
 
Mbunge mtata Kangi Lugola ameanza kwa kumfagilia rais Magufuli, kisha akaanza kumvaa waziri wa maji kwa kupunguza bajeti na kutokuweka fedha ya tozo ya maji na kumwambia asipoweka basi ajiandae kugeuzwa maji na Magufuli kwani rais aliahidi hivyo.
Amesema wabunge watakaopitisha bajeti hiyowakati haijaongezwa pesa ya tozo ya shilingi 50 basi ataitisha mwenge kuwaelezea wananchi usaliti wao na kuwaambia waache ushabiki kwenye bajeti hiyo na kupitisha bajeti ambazo hazitekelezeki

huyu inaonekana hataki gari la wagonjwa, shauri yake
 
Kwa zaidi ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika wananchi hawapati huduma ya Maji wala umeme upatikanaji wa huduma za afya za Usalama wa raia bado ni shida kubwa sana! Zahanati za karibu na makazi ya Watu hakuna hadi kwenda Hospitali ya Wilaya ndo unaweza mpata daktari nako vifaa Tiba hakuna! Kila mwaka bajeti za Maji zinapitishwa lakini wananchi hawapewi huduma za Maji miaka nenda rudi! Imaeshikana kulifanya Jiji la Dar kuwa mfano Kwa mikoa mingine kwamba ukiwa Dar popote Maji yanapatikana Kwa urahisi? Huduma za vyoo ni mbaya usafi ktk kuandaa vyakula migahawani ni wa mashaka sababu ya shida ya Maji ! Ni risk kununua Maji ya madumu jamani! Vituo vya polisi viko mbali Na makazi ya Watu wengi , mwizi akikamatwa eti raia unatakiwa utoe hela Kwa mtendaji wa kijiji akupe barua, uwalipe wagambo hela ya kukukatia mtuhumiwa Na hela ya usafiri wa kumpeleka kituo cha polisi, Wazungu wanastahili kutudharau! Ni Kama time proof failure! Kuna ndugu yangu yuko Dar alipo ni mita chache tu kulipo Bomba kubwa la Maji la Ruvu chini lakini miaka nenda wakienda Dawasco kufuatilia hadi leo si Simba si yanga! Bilabila!
 
Mbunge mtata Kangi Lugola ameanza kwa kumfagilia rais Magufuli, kisha akaanza kumvaa waziri wa maji kwa kupunguza bajeti na kutokuweka fedha ya tozo ya maji na kumwambia asipoweka basi ajiandae kugeuzwa maji na Magufuli kwani rais aliahidi hivyo.

Amesema wabunge watakaopitisha bajeti hiyo wakati haijaongezwa pesa ya tozo ya shilingi 50 basi ataitisha mwenge kuwaelezea wananchi usaliti wao na kuwaambia waache ushabiki kwenye bajeti hiyo na kupitisha bajeti ambazo hazitekelezeki

Wataitwa hao kesho watakalishwa chini,juma 3 wataipitisha.
Wabunge wetu tunawajua wala sio wageni kwetu
 
Kitila ubunifu wako hapo unahitajika, ukwamue jahazi.
Maji safi na salama ni Afya, afya ni maendeleo. Nchi yetu haiwezi kuendelea ikiwa na walipakodi wagonjwawagonjwa...
Sio UBUNIFU.
Hivi mnadhani Mbawala ni MBUNIFU?
Wizara ikipewa hela lazima itafanya kazi.Hata JPM mlimuona anafanya kazo kwakua alikuwa akipewa hela pale WIZARANI.Ndio maana hata MV DSM aliweza kuinunua.
Sasa wizara haipewi hela mtamlaumu WAZIRI?
 
Kwa zaidi ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika wananchi hawapati huduma ya Maji wala umeme upatikanaji wa huduma za afya za Usalama wa raia bado ni shida kubwa sana! Zahanati za karibu na makazi ya Watu hakuna hadi kwenda Hospitali ya Wilaya ndo unaweza mpata daktari nako vifaa Tiba hakuna! Kila mwaka bajeti za Maji zinapitishwa lakini wananchi hawapewi huduma za Maji miaka nenda rudi! Imaeshikana kulifanya Jiji la Dar kuwa mfano Kwa mikoa mingine kwamba ukiwa Dar popote Maji yanapatikana Kwa urahisi? Huduma za vyoo ni mbaya usafi ktk kuandaa vyakula migahawani ni wa mashaka sababu ya shida ya Maji ! Ni risk kununua Maji ya madumu jamani! Vituo vya polisi viko mbali Na makazi ya Watu wengi , mwizi akikamatwa eti raia unatakiwa utoe hela Kwa mtendaji wa kijiji akupe barua, uwalipe wagambo hela ya kukukatia mtuhumiwa Na hela ya usafiri wa kumpeleka kituo cha polisi, Wazungu wanastahili kutudharau! Ni Kama time proof failure! Kuna ndugu yangu yuko Dar alipo ni mita chache tu kulipo Bomba kubwa la Maji la Ruvu chini lakini miaka nenda wakienda Dawasco kufuatilia hadi leo si Simba si yanga! Bilabila!
Nchi kubwa hii wazee. Hata hivyo Tunakwenda sio mzaha. Jaribu kulinganisha nchi zingine zilizopiga hatua kimaendeleo barani kwetu na hali halisi ya maisha yao. Mfano Kenya ni kweli wako na mambo mengi waliyopiga hatua ila maskini wa kenya sio sawa na wa Tanzania. Ni Tanzania pekee unaweza ukalala leo maskini na kesho tajiri alimradi ujitume kwa bidii. Kwa wenzetu hilo ni ndoto. Kinachotuponza sisi ni uvivu na ulalamishi.kutwa nzima Utakuta vijana wamekaa kijiweni. Kenya hiyo kitu haipo.
 
Back
Top Bottom