Kangaroo court…..

Hivi, kwa kilichotokea leo kwenye kesi ya Lissu, hiyo mahakama nikiita ni kangaroo court nitakuwa nimekosea?
Nimesema Mahakama ni tatizo kuliko Katiba miaka zaidi ya 10! Kama kuna taasisi imeoza na inahitaji kufanyiwa marekebisho ni Mahakama. Watu walipumbazika na kuzubaa kwa kudhani akina Nyalali, Samata, Kisanga wapo kila siku.

Mahakama husema si kazi yake kutoa haki isyoombwa. Kesi ya Uhani ya Lissu kwa mujibu wa hati ya mashtaka imefanyiwa ''amendment '' kwa vifungu vinavyoipa Mahakama ruhusa ya ku relagate kosa la Uhani hadi uchochezi.

Yaani Mahakama inatafuta mashtaka halafu inayajadili na kutolea hukumu! bila kuombwa na upande wa mashtaka au kumtaka mshtakiwa ajitetee. Majaji kwa mwezi mzima wapo bize kutafuta vifungu vya kumhukumu TL

Katuga aliomba Mahakama ''si lazima itoe hukumu ya kunyongwa' bali nyingine ndogo. Mahakama imefanya exactly alichosema wakili wa Serikali Katuga. Sidhani kama ni bahati mbaya au coincidence!

Mahakama haikupitia hoja za mashtaka na za Lissu kama zilizvyoletwa Mahakamani, ikaingia katika hisia

Nchi ipo pabaya sana! ikiwa wananchi wanakata tamaa na mfumo wa utoaji haki hawana chaguo au cha kupoteza. Watu wamesahau tulifikaje Oct29! Nchi imepooza si kwa kifungo cha Lissu but a travesty of Justice.

Kikundi kidogo cha sycophants na imbecil kinashangilia kikisahau mamilioni wapo kimya wamebeba hisia,hasira na chuki vifuani ! wanatafakari wapi wakimbilie kuipata haki maana Mahakama imepoteza credibility na integrity!

JokaKuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…