Kanda ya Ziwa vs Kaskazini


Magufuli hafai
 
Wewe ndio unaleta mambo ya ukanda hapa kama mko wengi unadhani wote wamepiga kura au watapiga kura Tanzania inahitaji mabadiliko iliyokosa miaka 53 hamka chagua kiongozi sahihi achana na ukanda mlianza na udini sasa mmekuja ukanda kama wewe unaona sifa kuwa kiongozi kutoka kanda yako alafu maisha kuwa magumu vile vile hongera
 
Sijaona mtu wa Kaskazini aliyejitokeza kumtetea Lowassa zaidi ya Mzee Kingunge, mh. Nchimbi, mama Sofia Simba na mh Adam Kimbisa. Hivyo kwa mtazamo wako, hawa ndiyo wanawawakilisha watu wa Kanda ya Kaskazini.
 
Sijaona mtu wa Kaskazini aliyejitokeza kumtetea Lowassa zaidi ya Mzee Kingunge, mh. Nchimbi, mama Sofia Simba na mh Adam Kimbisa. Hivyo kwa mtazamo wako, hawa ndiyo wanawawakilisha watu wa Kanda ya Kaskazini.

Wafuasi wote wa Chadema watokao Kaskazini walishahamia Kwa Edo, Coverage kubwa Edo aliipata toka vyombo vya habari vya IPP. Alipendelewa kuliko wagombea wote. Jerry Silaa pia alıkuwa kwa Edo, hata baadhi ya viongozi wa CDM.
 
wewe mueka mada ni mbaguzi' tena ni mbaguzi sana ufai ata kidogo kuweka uchambuzi wakibaguzi ni kuwagawa watanania nasisitiza we ufai na watao kusapoti kwenye hili na wao awafai
 
Wafuasi wote wa Chadema watokao Kaskazini walishahamia Kwa Edo, Coverage kubwa Edo aliipata toka vyombo vya habari vya IPP. Alipendelewa kuliko wagombea wote. Jerry Silaa pia alıkuwa kwa Edo, hata baadhi ya viongozi wa CDM.

Doh, mpaka wa CDM walihamia kwa Edo! Sababu ya mapene nini?
 
Kwa wanaccm waliojitokeza kuomba kugombea urais kwa tiket ya ccm Dr Magufuli alikuwa ndo the best
 
Hivi CCM mko tayari kutumia hata njia haramu ili mpite kama mlivyozoea? Huu ubaguzi mnaohubiri hata kama siyo utakuwa na madhara kwa Taifa kesho.

Hebu tuambie, rais akitoka kanda ya ziwa kaskazini watakosa nini? Vivyo hivyo akitoka kaskazini kanda ya ziwa wanakosa nini? Je, vipi na kanda zote zilizobaki?

CCM kuweni makini, msiwabague Watz
 
Ulaaniwe ewe unayewaza kuvuruga umoja wa watanzania kwa kutumia propaganda za ukabila, udini, rangi na mengine kama hayo. Katu Watanzania tusikubali kuhujumiwa na baadhi ya wafuasi wa CCM, ACT, ama chama chochote wenye nia ya kuvuruga umoja wa Watanzania na Waafrika kwa ujumla wetu. Mwanzisha mada ni mmoja wao.
 
Mkuu Ngokongosha, japo siungi mkono aina yoyote ya ubaguzi, uwe wa kidini, jisia, ukabila, ukanda, rangi, kipato ahata umri, etc, na wengi watakuona wewe ni mbaguzi, sisi waumini wa ukweli halisi jinsi vile ulivyo, tumekuelewa!.

Tukubali tukatae, kuna udini mkubwa kwenye siasa zetu!, huu ni ubaguzi!, namna ya kuufuta sio kuunyamazia, bali kuuzungumzia wazi wazi kinaga ubaga, na ikibidi kuuzuia kwa makusudi kabisa!. Kuna watu wanadhani jina la Magufuli limeingia kwa bahati mbaya tuu!. Kuna vitu kuna watu waliviangalaia na waliisha amua kabla, hivyo wakaamua 2015 ni Magufuli. Bahati nzuri mimi ni mmoja wa watu tuliodokezwa kuhusu Magufuli, na niliwaeleza watu humu Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!. kuna sababu zilitolewa why ni Magufuli!.

Nimefurahi ulipozungumzia kukubalika kwa Magufuli kama John Pombe Magufuli na sio eti kwa sababu anatoka Kanda ya Ziwa, kwa sababu ingekuwa watu wa Kanda ya Ziwa wanaukabila kihivyo, wangemchagua Cheyo kwa sababu amewahi kugombea urais!!, kitu ambacho ni ukweli kabisa Magufuli anakubalika kwa sababu ni Jembe la ukweli!.

Kule nyuma sii mara moja wala mbili, nimewahi kuuliza humu kuhusu mambo haya haya ya ukabila, udini na ukanda, nikaishia kunyooshewa vidole kuitwa mbaguzi, lakini huu ndio ukweli wenyewe, watu makini wanaoijua sayansi ya siasa, hili wanalijua ndio maana wakaja na jina la John Pombe Magufuli.

Kanda ya Ziwa ndio determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, kitendo cha CCM kumteua Magufuli, kitapelekea mgombea wa CCM sio tuu kupata ushindi wa kishindo cha ajabu, bali pia atayarejesha CCM, yale majimbo yote ya kanda ya Ziwa yaliyoshikwa na Wapinzani!.

Mimi kwa sababu siku zote ni muumini wa ukweli jinsi ile ile ulivyo, sipati taabu kuitwa mbaguzi kwa kuusema ukweli, wale unaopenda kuujua ukweli huu ninaozungumzia hapa, mnaweza kupitia nyuzi zangu hizi.
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?

Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!
Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika Siasa za Tanzania?!.

Pasco.
 
Kamanda naona mmechanganyikiwa toka CCM wampitishe Dr.Magufuli.

Sasa ACT wanahusika vipi na migogoro yenu UKAWA unataka kuniambia Lowassa leo kageuka malaika Chadema...

Teh teh teh
 
Ni kweli siasa zimeanza kutugawa kikanda nachukia saaana!!tutaenda mpk kwa makabila
 
Waenezi Wa kugawa watu ni ccm na ndio WANa injini ya kuinjinia huyu mdini,huyu mkristo,huyu mwislam,huyu mkatoliki,huyu mpemba,huyu kaskazini,wamebakiza tu kusema huyu Wa mbinguni,bahati mbaya sana wajinga wapo wanaowasikiliza na kucheza na Ngoma Yao kama kana kwamba kuna ukweli kumbe ni kutaka kbki madarakani
 
Ilifikia hatua hadi wafuası wa CDM wakaanza kumuunga mkono Lowasa licha ya ukweli kwamba ndio walipga kelele kuwa nı fisadi.Na wengi wa hawa ni wa Kaskaz.Tuko nao mitaani, tunawaona.Watu wa Kaskaz wabinafsi sana.

wanakwambia Lowassa ana maamuzi magumu, ukiwauliza ni maamuzi gani hayo magumu... hawana jibu...
 

Ni kweli kiongozi mambo yatachafuka tukiendelea kuliongelea hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…