I support CHADEMA and the opposition in general, lakini kama Wapinzani mtaendelea kufanya siasa zenu ktk mtindo huu wa kutegemea hisani kutoka CCM, basi itawachukua miaka 100 kuingia ikulu. Let's be honest here, ili chama chochote kiweze kushinda uchaguzi kinapaswa kuwa flexible, kibadilike kuendana na hali halisi ya kisiasa ilivyo.
Kuna mahali CHADEMA wamejifunga pingu, sasa wanategemea hatima kufikia malengo yao, hakuna mikakati wala plan B. CHADEMA walishaamua Dr Slaa awe mgombea wao iwe isiwe, sababu wanayotoa ni kwamba alifanya vizuri ktk uchaguzi wa mwaka 2010. Sote tunajua kwamba Dr Slaa alifanya vizuri mwaka 2010, but things are changing over a course of time, na tunafahamu fika kwamba hali halisi ya kisiasa imebadilika sana mwaka huu tangu CCM wamchague Dr Magufuli.
Tunajua fika kwamba kete kubwa (talking point) ya Dr Slaa ingekuwa ni ufisadi, sasa anapokwenda hoja ya namna hii kwa wananchi dhidi ya mtu kama Dr Magufuli atapuuzwa kiaina, kwasababu wananchi nao wanaamini Dr Magufuli ndio suluhisho la ufisadi nchini.
Sasa basi, CHADEMA na UKAWA walipaswa kuja na plan B, nayo ni Tundu Lissu, mwenye hoja ya katiba mpya, Tundu Lissu akiingia ktk uchaguzi na hoja ya rasimu ya Warioba, wananchi wanaweza kubadilisha mawazo yao na kuwafanya waanze kufikiria tena kuhusu chaguo lao la urais.
Right now wananchi washasahau kabisa kuhusu suala la katiba mpya, wao wanachoamini ni kwamba Dr Magufuli atainyoosha nchi kutokana na misimamo yake. Ni vyema UKAWA wakaingia ktk uchaguzi na Tundu Lissu huku akiibeba ajenda yake ya katiba mpya aliyoipigania akiwa bungeni, katiba mpya bado ni kete muhimu ya kisiasa ya Upinzani, na CCM waliamua kuachana na mchakato wa kura za maoni kwasababu waliogopa wangeshindwa kwa aibu wakati wa kura za maoni.
Kila kitu kina zama zake, Dr Slaa na slogan yake ya ufisadi (2010) na ilikuwa na nguvu sana. Naye Tundu Lissu na katiba mpya, hii ina nguvu sana japo UKAWA hamuonekani kutambua.