Ngokongosha
JF-Expert Member
- Feb 9, 2011
- 3,400
- 7,610
Nimesoma comment nyingi sana zikilaumu Kanda ya Ziwa kwamba wamekuwa wasaliti na ukabila, hii naona kama ni silaha inayotumiwa na wanachama wa CHADEMA ili kuwatisha wale wenye mpango wa kumpigia kura Magufuli waonekane wakabila na wasaliti.
Lowassa anatoka Kaskazini, kipindi anahonga pesa watu walikuwa kimya wanasema huyu ndie rais, na walisahau kwamba wao kipindi cha nyuma walisema CCM hakuna msafi ila kwa Lowassa wakawa kimya, kwa sababu nia yao ni rais atoke Kaskazini, ndio maana alipoangukia pua ikawa kaonewa na sasa wanamkaribisha kwenye chama chao, ingawa hilo sijui kama litatokea.
Kwa kifupi kwa watu wa Kaskazini, Magufuli ni mchafu na Lowassa ni msafi.
Huko kunakoitwa kwa wabaguzi ndio kuna wabunge hadi wenye asili ya Kaskazini, tofauti na huko Kaskazini ambako asilimia kubwa ya wabunge ni wenyeji wa huko.
Imefikia hatua watu wanasema Lowassa akija CHADEMA anakuwa rais, Mbowe Waziri Mkuu, Slaa Waziri wa fedha, Mbatia, Mnyika.
Huu sio ubaguzi wa kikanda jamani?
Wanasema Magufuli hawezi fanya lolote kwa sababu ya system ya CCM, je, huyo Lowassa angepitishwa yeye angetumia system ipi?
Sitaki kuamini sana mambo haya kwamba ni ubaguzi ila naamini kama watu wa Kanda ya Ziwa wameamua kumuunga mkono Magufuli, labda kuna mazuri wameyaona, ingekuwa ni ukanda Jonh Momese Cheyo angekuwa rais toka zamani tu.
Mtu kukubalika eneo atokako ni kitu cha kawaida popote pale duniani, hata angepita Mwandosya watu wa Nyanda za Juu wengi wangemuunga mkono.
Angepita Ngeleja watu wasingekuwa wanasema kuhusu ukabila bali wapinzani wangeshangilia maana hana mvuto hata kule atokako pamoja na kwamba ni wa Kanda ya Ziwa.
Uchaguzi wa Uingereza mwezi May mwaka huu watu wamegombea mara moja wakashindwa wakajiuzulu, Tanzania watu wanagombea walewale miaka nenda rudi, halafu wanajiita wanademokrasia.
Ni hayo tu.