Kanali mstaafu kugombea ubunge Tarime kupitia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kanali mstaafu kugombea ubunge Tarime kupitia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Jan 9, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Date::12/5/2009Kanali mstaafu atangaza kugombea ubunge Tarime kupitia CCM[​IMG]Na Samson Chacha, Tarime
  KANALI Mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mahende Kichonge (65)ametangaza kugombea Ubunge katika Jimbo la Tarime mwakani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

  Kichonge alitangaza nia hiyo wakati wa mazishi ya kaka yake aliyewahi kuwa Ofisa Utumishi Tawala wa Kwanza katika Wilaya ya Tarime na Mkaguzi wa Mahakama za Mwanzo nchini, Kichonge Mahende aliyefariki Novemba 30, mwaka huu na kuzikwa Desemba 4, mwaka huu kijijini kwake Kemakorere Kata ya Nyarero.

  Katika mazishi hayo, alikuwepo kanali Raphael Isarra Chacha na kijana mkubwa wa marehemu Kichonge Luteni Kanali David Kichonge,na mamia ya waombolezaji, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ryoba Kangoye Masero ambaye ni ndugu wa marehemu.

  Akitoa kauli hiyo katika umati mkubwa wa waombolezaji waliofika katika mazishi hayo, Kanali Mahende alisema kuwa

  "Mimi kama mwana Tarime ninayo haki ya kugombea Ubunge katika Jimbo langu hili la Tarime mwakani kupitia chama changu ambacho sitakihama daima cha CCM na ninazo sababu za kuwania kiti hicho, kwanza kuwaunganisha Jamii ya Kabila la Wakurya na kuwa kitu kimoja na kuondoa dhana potofu za mila zilizopitwa na wakati za kubaguana, kuwashirikisha wazee wa mila wa koo zote za kabila la Wakurya na kukomesha wizi wa mifugo kwa kushirikiana na Sungusungu,” alisema.


  Kanali Mahende alisema endapo atachaguliwa atahakikisha barabara zote ambazo hazipitiki kwa urahisi zinafanyiwa matengenezo, kukamilisha madarasa na nyumba za walimu na kwamba ataiomba serikali kuongeza walimu katika shule za Sekondari za kata kutokana na kuwepo kwa tatizo la walimu.

  HIVI HAWA MAKANALI HUWA NI MAKADA WA CCM HUKO JESHINI????
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu vipi wanajeshi wamekosa nini kwani? Au wao sio wananchi wenye haki sawa na wengine ya kuamini chama wanachokitaka?

  Respect.


  FMEs!
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  waende zao siasa na kushika bunduki ni vitu tofauti ndo maana tunawaona wakina Mkuchika wanakurupuka sasa
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu hii ni kwa mujibu upi hasa wa katiba ya jamhuri au?

  Respect.


  es!
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Nimetafuta sana ndani ya katiba yetu kama kuna kipengele kinachomkataza mwanajeshi au mtumishi yeyote mstaafu asigombee nafasi yeyote ya kisiasa nyumbani TZ,lkn sijakiona!

  Sheria inakataza tu kwa mtumishi wa UMMA kujihusisha na siasa akiwa bado ni mtumishi wa serikali;kikomo chake cha kutoshiriki siasa kinagota pale ama anapoamua kuacha kazi kwa hiari yake mwenyewe ili ajitumbukize kwenye siasa au anapostaafu kazi!

  Kwa maana hiyo basi ni haki yake ya msingi na ya kikatiba kwa Kanali huyu mstaafu kugombea;kama wana Tarime watamuona anafaa atashinda;then ataapishwa kuwa mbunge halali wa Tarime bila pingamizi lolote la kikatiba!
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Agombee tu aone kama Chadema hawajamshinda! asije na bunduki tu.
   
 7. a

  alles JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2010
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ana Haki ya kugombea, ila umri wake(65) ndio unaonitisha.
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimebaini kumbe huyu jamaa alisindwa kwenye kura za maoni mwaka 2005. Alikuwa anataka kugombea kwa tiketi ya CCM pale Kinondoni. Nchi hii inaendeshwa kijeshi.Hii ni baadhi tu ya mafisa waandamizi Jeshini ambao naongoza/wamewahi kuingoza hii nchi katika awamu ya 4:
  1. Luteni Kanali J.M Kikwete
  2. Capt. J. Chiligati
  3. Capt.G. Mkuchika
  4. Luteni Y. Makamba
  5. Maj. Gen S. Kalembo
  6. Kanali F. Massawe
  7. Generali T. Kiweru
  8. BRIG. GEN.E. Balele
  9. Kanali Anatori Tarimo
  10. BRIG. GEN.A . Ramadhani
  11. Kanali Enos Mfuru
  12. Kanali Issa Machibya
  13. Kanali Joseph Simbakalia
  14. Kanali Madaha
  15. Kanali Issa Njiku
  16. Kanali mstaafu Ayub Kimbau
  17. Kanali Elmon Mahawa
  18. Kanali Samwel Ndomba
  19. Luteni Kanali Serenge Mrengo
  20. Kanali Edmund Mjengwa
  21. captain Jaka Mwambi
  22. Comm. A. Rajabu
   
 9. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimebaini kumbe huyu jamaa alisindwa kwenye kura za maoni mwaka 2005. Alikuwa anataka kugombea kwa tiketi ya CCM pale Kinondoni. Nchi hii inaendeshwa kijeshi.Hii ni baadhi tu ya mafisa waandamizi Jeshini ambao naongoza/wamewahi kuingoza hii nchi kisiasa katika awamu ya 4:
  1. Luteni Kanali J.M Kikwete
  2. Capt. J. Chiligati
  3. Capt.G. Mkuchika
  4. Luteni Y. Makamba
  5. Maj. Gen S. Kalembo
  6. Kanali F. Massawe
  7. Generali T. Kiweru
  8. BRIG. GEN.E. Balele
  9. Kanali Anatori Tarimo
  10. BRIG. GEN.A . Ramadhani
  11. Kanali Enos Mfuru
  12. luteni Kanal John Mzurikwao
  13. Kanali Issa Machibya
  14. Kanali Joseph Simbakalia
  15. Kanali Madaha
  16. Kanali Issa Njiku
  17. Kanali Ayub Kimbau
  18. Kanali Elmon Mahawa
  19. Kanali Samwel Ndomba
  20. Luteni Kanali Serenge Mrengo
  21. Luteni Kanali Benedict Kitenga
  22. Kanali Edmund Mjengwa
  23. Kapteni James Yamungu
  24. Luteni Kanali John Mzurikwao
  25. Kapteni Geoffrey Ngatuni
  26. Kapteni Assary Msangi
  27. Luteni Winfrid Ligubi
  28. Kapteni John Barongo
  29. Kapteni Malle
  30. Kapteni Evans Balama
  31. Kapteni Seif Mpembenwe
  32. Kapteni Mwapinga
  33. Luteni Abdallah Kihato
  34. Luteni Chiku Gallawa
  35. luteni Edward Ole Lenga
  36. Kapten John Komba
  37. Kapteni John Henjewele
  38. Luteni Chiku Gallawa
  39. Luteni Kanali Leopald Kalima
  40. Kapteni Seif Mpembenwe
  41. captain Jaka Mwambi
  42. Comm. A. Rajabu
   
Loading...