Kanali feki atapeli vijana 62 kwenda jeshini

KingKacha

Senior Member
Jun 15, 2016
118
119
Kundi la vijana zaidi ya 62 kutoka Mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa wameingizwa mkenge na mtu ambaye jina lake halijafahamika mara moja, aliyejipa cheo cha ukanali kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), aliyewaahidi kuwafanyia mpango wa kujiunga na jeshi hilo baada ya kila mmoja wao kutoa shilingi 200,000.

Akizungumza na gazeti hili Ijumaa iliyopita juu ya tukio hilo, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Abdulkarim Shah akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya Skauti Tanzania, Upanga, Dar alisema waliwapokea vijana hao walioambatana na kamishna wa skauti kutoka Njombe aliyewaombea hifadhi kwa matarajio ya kwenda jeshini.

“Kwa kuwa skauti ni wamoja tulikubali kuwahifadhi hao vijana, lakini jambo la kushangaza siku zilizidi kukatika wakiwa bado kituoni kwetu na kila tulipokuwa tunaulizia tulijibiwa kuwa mipango ilikuwa inaendelea na jambo la kushangaza vijana hao walizidi kuongezeka mpaka wakafika 62 ndani ya muda wa siku chache tu,” alisema.

Akaongeza: “Jambo hilo lilitushangaza, pia tulijiuliza vijana wengi kiasi hicho wanawezaje kwenda jeshini kinyemela bila kupitia kwenye ngazi za wilaya na mikoa, tukakosa jibu huku tukiogopa wasije kuwa vijana wanaoandaliwa kwa ugaidi. Ikabidi tufanye jitihada za kumpata yule kanali na alipopatikana na kubanwa tuligundua alikuwa ni tapeli, tukamfikisha kwenye Kituo cha Polisi Salenda Bridge ili aweze kushughulikiwa.”

Kwa upande wa Dany Mwinda ambaye ni mmoja wa vijana hao anayetokea Makambako, Njombe alisema kuwa ni kweli jambo hilo liliwatokea na kuna vijana zaidi yao wako katika nyumba za kulala wageni jijini, hata hivyo, kwa kuwa suala lao lilifikishwa kwenye vyombo vya sheria imebidi wawe wapole kusubiri hatima yao.

Gazeti hili lilishuhudia vijana hao wakiwa wamezagaa kwenye ofisi za skauti wakiwa na vipara na lilifanya pia jitihada za kumtafuta kamishna wa skauti Njombe aliyewakusanya ambaye pia ndiye aliyekusanya pesa zao na kumpatia kanali feki lakini hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi.

Baadhi ya maofisa wa polisi wa Kituo cha Salenda Bridge walithibitisha kukamatwa kwa mtu huyo, hata hivyo hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa wao siyo wasemaji.
 
Hapo ni kukamata na hao vijana wote mahakamani, mtoa rushwa na mpokea rushwa wote wana hatia. Kijana umemaliza form four bado hujui utaratibu wa malipo wa serikali? hata kama ni kilaza namna gani ukimaliza form four unakua unajua kwamba unapolipia huduma yeyote serikalini ni lazima upewe risiti.
 
Ili chain na tunaweza kuona na uyo tapeli na yeye katapeliwa ndio maana simu zake akuzizima labda alikuwa na uhakika na kazi yake
 
City
Ati wanashangaa "inawezekanaje vijana wengi hivyo wajiunge Jeshi kinyemela?" Wamezoea wachache!..Imekuwa kawaida watu kwenda jeshini kwa 'mipango'
Nimetakauliza hilohilo kumbekimemshtua idadi lakini hizo michango kweli zipo inaonekana
 
Kuna Mtu Kaambiwa Atapewa Ajira Jeshini Yupo Manyovu Buhigwe Kaambiwa Alipe 500000/-
Mwezi Wa Saba Anakwenda Tabora Kwenye Usaili
Naye Kaliwa Mchana
Tena Nilimtahadhalisha Haraka
 
Poleni sana hata mm kuna mjinga alinitapeli kitambo ila tulisafisha nyumba yake yoe yupo umu umu jamii forum ni mtu kutoka bukoba ila tulimtia adabu yote n njia za maisha 2 poleni na hongera kanali feki umepata pesa ya supu
 
Poleni sana hata mm kuna mjinga alinitapeli kitambo ila tulisafisha nyumba yake yoe yupo umu umu jamii forum ni mtu kutoka bukoba ila tulimtia adabu yote n njia za maisha 2 poleni na hongera kanali feki umepata pesa ya supu
Mteja tumjue na alikutapeli ishu kama hii mkuu?
 
Kanali feki dah kwahiyo kapanda vyeo vyote from koplo to kanali hatari Sana. Bado Kuna maafisa usalama taifa feki .
 
Hizi habari za kujidai wewe unafight ufanikiwe kwa njia zisizo halali matokeo yake ni haya. Mtoto kafeli mpeleke sehemu anayostahili unaanza kupenyeza vi laki mbili kwanini wenye midomo wasile?
 
Huyo kweli kanali feki,katapeli watu wote hao lakini kakamatwa kirahisi.
 
Mm alinitumia hii SMS

"HABARI ZA LEO NDUGU,SASA ILE NAFASI ULIYONIOMBA YA KIJANA WAKO KUJIUNGA NA JESHI IMEPATIKANA. VIPI BADO UNAHITAJI!? NI ZAHARAKA NAOMBA TUWASILIANE KAMA BADO"(Nambake: 0766061108)

Nikajaribu kutafakuri ni lini niliwahi kuongea na Mtu ishu kama hizo, na wala sikuwa na uhitaji wa Mm au hata Ndugu yangu kujiunga na Jeshi.

Moja kwa Moja nkajua kuwa hawa ni Matapeli wanaotaka kuwaingiza Mkenge Watu walio na ukosefu wa ajira.

Tuwe Makini jamani. Saivi utapel
umekithiri. Ukipata SMS kama huielewi, washirikishe Watu zaidi ya Mmoja ili uweze kupata Ushauri toka kwao.
 
Siku zote wajinga ndiyo waliwao. Unadhani mababu zetu walikosea kusema hivi? La hasha hawakukosea. Kuwa makini kijana.
 
Shenzi kabisa....Vijana wa Njombe mnatutia aibu hivi mnatapeliwaje kijinga hivyo?
 
Back
Top Bottom