Kamwe sintasahau Ijumaa 13th April 2001.

Maisha mengine hutupitia ili tujifunze ingawa yanakuwa sio part of our lives
Ila ni mafundisho tu
Pole sana you are not alone
Halafu Friday 13th
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
duuh jamaa umenitia huzuni ya gafla,sema huwez kujihukumu kwan ilikua akila za utoto am sure as for now usingeweza kumfanyia ivo

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hicho ni kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza na kunifanya mara nyingine naamka usiku nawaza hivyo. Mara nyingine natamani ningeongea naye vizuri hata dakika 1 ile siku ananiaga.
Daaah hiyo inauma kimyama asikuambie mtu.halafu kitu kingine ni kwamba endapo ungemkubalia apafahamu kwenu arusha, angekuja kukaa na aunt yake wakati wa likizo na pengine hiyo ajali ingemkosa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini Wadau,

Leo nimeamua tu nieleze tukio/ uzoefu mdogo nilioupata katika uhusiano wa Mapenzi wakati nikiwa mdogo kiasi.

Lakini zaidi natamani sisi kama Wanaume tuwathamini sana wanawake wanaoonesha moyo wa kutupenda KWELI na tuthamini upendo wao kwetu.

Ni hivii:

Nakumbuka tangu siku ya kwanza kujoin shule moja maarufu ya sekondari iliyopo Monduli huko Arusha nilikuwa Mtukutu na tangu form One nilikuwa na vikundi vya wanafunzi wahuni kweli tulikuwa tunaita (Mobb) na tuliipa jina kundi letu japo tulikuwa tunafanya vizuri kimasomo, Tulishaapa kutokuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti yeyote na kama ikitokea binti akajirahisisha kwetu tunampiga...hiyo ilikuwa kama kauli mbiu na tuliona huo ndio Uanaume Haswaa!

Kila jumatatu ilikuwa ni siku rasmi ya kuimba wimbo wa Taifa na wa Shule kwa adabu, kupandisha Bendera ya Taifa na kukaguliwa usafi wa mwili na mavazi.

◆ Sasa nakumbuka jumatatu moja asubuhi tunatoka kwenye Parade tunaelekea darasani nikawa naongozana na binti mmoja mgeni bila kujua anakuja darasani kwetu.

Mara ghafla nikashangaa palepale ninapokaa katika siti yangu akaja kukaa yule binti, na kiukweli alikuwa mzuri ila sikutaka anizoee. Aisee alikuwa yuko sharp kujibu maswali na kimombo kilikuwa kinapanda kwsbb kalitoka English Medium school huko Dsm wakati sisi ni wa St. Kayumba. Kiukweli ile hali ilikuwa inaniboa sana nilimwona ana kiherehere sana...japo alikuwa ananiokoa na fimbo sometimes kwa kunisaidia masomo darasani.

Nilikuwa kila nikienda Bwenini wenzangu wananiambia " Naona umeletewa mrembo, bibie mlainii " aisee kweli hisia hazifichiki, kumbe Hellen alinipenda sana japo nilikuwa rafu mno hadi kimavazi. siku zilivyozidi kwenda nikaanza kuona umuhimu wa yule binti haswa tulivyoingia form 2 kuelekea 3, alikuwa ananisaidia kwa vingi mno japo sikujali na nilikuwa namsema vibaya kwa wenzangu.

● Kwa Mfano, vitu ninavyokumbuka kutoka kwake :~

Tulikuwa na ratiba ya kuchunga ng'ombe za shule kila jumamosi kwa form One wavulana, ikifika zamu yangu alikuwa anafua nguo zake mapema then anakuja kushinda na mimi katika kuchunga bila kujali hadi jioni napoenda kuchukua nusu lita yangu ya maziwa kama kawaida.

Nakumbuka siku ile alipoenda kuchukua kitabu cha nyimbo cha kilutheri, wakati huo kikiitwa "MWIMBIENI BWANA" cha mama yake akafuta jina la mama yake kwenye kitabu na Biblia akajaladia na kunipa mimi ili nisiadhibiwe na Mwl. wa UKWATA kwa kupoteza hivyo vitabu.

Nakumbuka Visiting days, alikuwa akitembelewa na wazazi wake na gari binafsi kutokea Dsm ananiita mimi na rafiki yake mmoja wa kike nawasalimia wazazi wake...na baadae jioni ananigawia kuku, viepe, juice na matunda ya kutosha napata na kupeleka Dom kisha tunatumia na wenzangu ila bado namsema vibaya kwa wenzangu (lakini moyoni nimeanza kumpenda haswa Hellen)

Nakumbuka jumapili tunaenda kanisani KKKT Monduli mjini, kisha tukirudi tunakaa uwanja wa mpira karibu na goli flani hata mpaka jioni...mara nyingine ananiegemea mpaka anasinzia mtoto wa watu...huku ameleta juice ya Fruto ile ya manjano na biskuti za Marie tunakula.

Nakumbuka alimwambia mama yake "Tukimaliza shule tutaoana na.........(mimi)"

Kwakweli alikuwa ananihadithia habari za kuchekesha za nyumbani kwao zoote kuhusu Wazazi wake, mdogo wake hadi dereva wao aliyekuwaga anakuja na wazazi wake shuleni na ambaye hadi mimi jamaa alinizoea sana na kunipenda hadi jina namkumbuka (Misana) tall hivi ni Msukuma.

■ KUHUSU SUMMER SEASON:

Kulikuwa na Wazungu wanakuja kiila mwaka pale shuleni kutoka USA, Denmark na Sweden na wanawachagua wale wanafunzi brighter zaidi na kuishi nao na kufanya nao tour za mara kwa mara na baadae wengine wanaenda aidha USA, Denmark au Sweden...Hellen nae akachaguliwa kwajili ya lugha na performance darasani.

Siku moja wazungu wawili ambao walikuwa wapenzi wakatuona kila mahali nipo na Hellen mmoja akasema wao akasema

" These two will marry each other "

Kuna masweta mazuri na mazito yalikuwa yanaletwa na hao wazungu yameandikwa "Power to the Bauer" la Hellen nikachukua nikawa navaa mimi...na akiniona nimevaa anafurahi mno. LAKINI, Kumbuka hapo bado nikiwa na wenzangu natalk shit kwake japo simwambii lakini huku naumia moyoni kumsema vibaya.

■ NISICHOKISAHAU KAMWE ■

Mwezi April tukikaribia kufunga shule kwajili ya Pasaka, Hellen alikuwa ananiambia anataka kupajua kwetu Arusha, kabla hajaenda kwao kwsbb kuna shangazi yake anaishi Sakina Arusha, hivyo atawaambia wazazi wake kuwa atabaki kwa Aunt yake...Sikumjibu chochote zaidi ya kumwangalia tu kwsbb nilikuwa na wenzangu na sikutaka kuonesha kuwa namjali. Najua aliumia kweli na hata mimi niliumia sanaaa.

Akaja tena kuniambia basi nipaki mizigo yangu halafu watanipeleka mpaka Arusha mjini waniache mimi wao waendelee na safari hadi Dsm tena akaniambia wazazi wake hawana shida yeye atawaambia nikamkatalia akachukia tena.

Siku ya Alhamisi kuamkia ijumaa siku ya kufunga shule nakumbuka akachukua daftari langu jipya halafu nyuma ya daftari akachora picha ya Bwana harusi na Bibi harusi akaandika majina yetu.

Chini akaandika wimbo wa ROXETTE

It Must have been in Love" ......but its over now.

Nikamuuliza kwanini anaupenda huo wimbo akaniambia tu yeye na dada yake wanaupenda sana. Baas

■ BAADA YA KUFUNGUA SHULE

Nakumbuka kwenye jumatatu au jumanne, tukiwa kwenye groups tunachambuliwa kitabu cha "No Longer at Ease" na Mwl. Madam Mbise (maarufu kama May Be) hiyo ni form three...mwalimu wakati anamalizia ili aondoke akatuambia tu straight away kuwa Halafu kuna mmoja wenu amefiwa na wazazi wake wote wawili na yeye ameumia sana pia. Wanafunzi kimyaaa tukaanza kuangalia ni kina nani bado hawajarudi.

Ghafla akasema ni mwenzenu Hellena. Mimi moja kwa moja nikamwomba mwalimu ruhusa ya kwenda nje kujisaidia. KWAKWELI kidogo nianguke, nikapata kama tumbo la kuhara na kuhisi kama sipo shuleni kabisa.

Wakati wa break nilienda Dom aisee nililia Mnoo sio siri siku nzima.

Mara nikaanza kukumbuka nilivyokuwa namjibu, pembeni nikaona hotpot flan hivi nzuri inayofanana na yake na alinipa kama zawadi ya kuwekea msosi nikakumbuka mengi.

Nilikumbuka mengi sanaa mazuri aliyonifanyia na kujiuliza kwanini mimi sikumjali au kuonesha kumpenda.

Baadae, tukasikia tu kuna waalimu wawili wanaenda kutoa pole msibani kumbe ni kweli Hellen na wazazi wake pamoja na dereva wao walipata ajali Tegeta Dsm wakafa pale pale kasoro dereva wao (Misana) akaja kufa baadae kabisa kwa kuishiwa damu.

Sikuwahi kufika Dsm hata siku moja na nilitamani pangekuwa ni karibu ili nikamwone tu lakini haikuwezekana.

● UJUMBE:

Ukibahatika kumpata mtu anayekupenda kweli, onesha kumjali au kujali hisia zake kwasababu hujui nini kitatokea mbeleni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtuzi mzuri sana

mpk nimetoa machozi
 
Ulisomea moringe sec mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukipendwa na mtu harafu ukacheza huwa haijirudii , isipokuwa ww utakuja kumuwaza na kuumia na wakati huo yeye hana time tena,hellena hata kama angebaki hai kwa vitimbwi vyako usingeweza kuwa nae.

Ilinitokea mimi hiyo mwaka 2002 nipo form one shule moja hivi maeneo ya Mwadui,kuna mdada alinipenda lakini sikupendeka na wala ckujali upendo wake kabsa, nilichelewa kuripoti shuleni na nikakuta kuna notice wameandika wenzangu ,kwa hiyo nilikuwa nimepitwa kidogo.

Huo mtindo wako wakujifanya kutokuwajali wasichana ndo ilikuwa life style yangu.Huyo mdada alianza kuwa karibu na mimi bila mimi kujua,akaniandikia notice zote akikopi kutoka kwenye daftali zake.Alisogeza meza yake na kiti hivyo tukawa tunakaa sambamba kabsa.

Kwao pia walikuwa wanajiweza kiuchumi ukilinganisha na kwetu ambapo mimi nilikuwa napewa elfu tano au tatu hadi temu iishe,hivyo kuhuzuria uji ilikuwa ni kawaida kabsa,wale walio pitia maisha ya bording hii hali wanaijua hasa wa miaka ya 2005 kurudi nyuma hali ilikuwa tete sana mashuleni yani kama haupo vzuri mfukoni ni shida mana kile chakula kilikuwa hakitamaniki.

Turudi kwenye mada,huyu binti alinipenda hadi nikaanza kujua kuwa ananipenda,ila tatizo likaja kwenye moyo wangu sasa kwani sikuwa na hata chembe ya upendo kwake.
Alikuwa ananihudumia vitu vingi sana,mambo ya chakula alikuwa akinisaidia sana.Alikuwa akibeba vyombo vyangu kila wakati wa kwenda kwenye chakula nk.

Yani kila alichokuwa nacho mimi nilikitumia bila shida akiniletea yeye mwenyewe hata kama nilikuwa mbali alinihifadhia,ila sasa ule moyo wa mimi kuthamini yale matendo adimu aliyokuwa akinifanyiwa waaala haukuwepo.Nakumbuka alikuwa ananitafuta asubui tu tunapofika shuleni yeye akitoka bwenini na mimi nikitoka mabwenini kwetu ,alikuwa ananiambia niwe najitahidi naonana nae tunasalimiana mana usiku mzima hatukuwa wote ,hivyo ni lazima tuonane kabla hata ya kwenda paredi.

Mimi hilo kichwani halikuniingia kwani sikuwa hata na fikra nae kabisa ,Nakumbuka siku moja nilimpita nikiwa na rafiki zangu na yeye akiwa na wenzake,aliniangalia mimi nikapotezea,baadae akaja mbele yangu akaniuliza mbona ninafanya hivyo?!, akaongeza swali,hivi wewe huwaoni wenzetu wanasalimiana asubui nawanazungumza machache baada ya kuonana katika siku mpya kabla ya kuendelea na mengine?. Mie sikuwa na jibu wala umuhimu wa swali lake kwangu haukuwepo kabisa.

Maisha hayo yaliendelea ila mwisho wa siku huyo binti alikuja akahama shule bila hata kunitaarifu ndipo nilipoanza kuuona umuhimu wake.
Hata wale wslikuwa hawaniambia kama napendwa wakaanza kuniambia "wewe Fatuma alikuwa anakupenda sana" .Tangu hapo nilianza kuhangaika sana kwani alinizoesha maisha flani hivi ya kuwa kama ninacho kumbe mimi sikuwa na lolote bali ni vyakupewa na mtoaji alikuwa Fatuma.Kutokana na mimi kutokumjali hakuniachia chochote zaidi ya vyombo vyake alivyokuwa akitumia na hii nazani ni kutokana na kuchangia vyombo hivyo alihisi kuwa nitaahangaika zaidi.

Hadi leo huwa namtafuta ila sijaweza kumpata tangu aniache hapo shuleni bila kuniaga kutokana na mapuuza yangu mwenyewe.Nazani atakuwa alishaolewa mana kwa umri nilionao mimi si rahisi hata kwa yeye kutokuwa na familia.

Fundisho,ukipendwa pendeka ila pia mimi nilikuwa na jiweka hivyo kutokana na uchumi wangu mbovu kwani nilikuwa najua wazi siwezi kunywa chai kama wenzangu ambao waliweza kununua chapati na chai na mimi nikiwa sina kitu isipokuwa uji wa shule wenye sukari ya kusikilizia kwa mbali,
Japo nakupendwa kote niliendelea kuwa mbishi hadi naachwa ndo hali ikawa mbaya zaidi mana sikuwa na namna tena zaidi ya kumkumbuka Fatuma aliyekuwa binti pekee alie jali uwepo wangu hapo shuleni.Nilibaki nalitazama dawati lake huku maumivu yakiujaa moyo,kwa kweli sikutenda haki kwa yote ,leo miaka 17 sasa tungu niachane nae ila namkumbuka sana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom