Kamwambia rafiki yake kuwa mimi nina kitambi eti ananichuna tu

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
167
Wadau mmeamkaje,

Jana nilikua pahala natazama mpira huku nakunywa bia taratibu, ghafla akatokea rafiki wa msichana wangu alikuja hapo bar kuchukua chakula, aliponiona akaja kunisalimia, baada ya salaam, nikamwambia shem kwanini usikae na wewe japo upate bia mbili tatu wakati unasubiri chakula? Akakubali

Alipochangamka akaniambia hivi shemu unajua kuwa d anakupotezea muda wako tu hana mpango na wewe, akatoa simu akanionesha msg za whatsaap walizokua wakichati na msichana wangu muda si mrefu, nilishangaa sana.Kwamba huyo fala mi namchuna tu, hicho kitambi na unavyonijua hivi nampeleka wapi? Zilisomeka msg hizo.

Kwanza jitu lenyewe hata kuvaa halijui, zile nguo zake unaweza kudhani ni choir master wa kanisa wadau nilisoma mengi, ndipo nikashangaa, hiki kitambi siku namtongoza kilikuwepo hakikuwepo? Kilikuwepo

Mavazi haya anayodai ni ya kanisa ndio sare za kazini, ila weekend napiga pensi au jeans na t shirt, kwa hiyo anataka niende kazini na jeans?Anadai huwa nampeleka gesti za elfu tano tano, sasa alitakaje? Yaani nimpeleke bar atumbue vitu ya elfu 40 au 50 then anataka nimpeleke hotel ya elfu 50?

Tuyaache hayo

Usiku wa jana akanipigia simu kumbukeni jioni yake ndipo nimeonana na rafiki yake na kuoneshwa msg, usiku akapiga simu, na kunieleza jinsi anavyonipenda, jinsi anavyopenda muonekano wangu, kwamba nisithubutu kumsaliti kuwa atajaiua, na kuwa amenimiss mno kwamba kwa nn leo hatukuonana, yote tisa kumi akadai unakuja lini kuwaona wazazi wangu unichukue jumla.

Guys which is which now?

Huyu sio jangili kweli?
 
mshukuru huyo dada aliyekupa evidence.anza kuchukua hatua taratibu usimpige kibuti ghafla utagombanisha marafiki.vigumu kuwaamini wanawake kwakuwa wakati mwingine hata wao wanakuwa hawajui wanachokitaka wanapoanzisha mahusiano ndo maana wanakuwa na vidumu kibao.
 
Mi naamini huyo dada anakupenda, ila anafanya hivyo kwa rafiki yake ili rafiki yake asikunyemelee (inaonekana anazijua tabia za rafiki yake vizuri).

Sasa wewe mpe muda na pia upunguze kumpa pesa kama ulikuwa unampa nyingi, utata ni hapo tu anaposema eti unampeleka gest za buku 5!

Kama vipi mchunguze kwa kupitia kwa rafiki yake huyo huyo kujua kama ana mwanaume mwingine, jifanye kuwa karibu na huyo rafiki ili upate taarifa zote, ikibidi ujifanye kama ikitokea mkaachana yeye ataziba pengo. Ila pia jipange kudanganywa, maana anaweza kuongeza chumvi ili ninyi muachane.
 
'Kwaya master' hapo unachunwa tu sepa fasta,ingekuwa umeambiwa maneno tu ungeweza kupuuza lakini umeoneshwa hadi na sms!!..
Hizo swaga za kwenda kwa wazazi hapo anakukoleza tu na huenda yupo mbioni kukupiga mzinga wa maana...
 
Daa aisee inauma sana, hawa viumbe nomaa, akishaona unampa kika kitu basi kivhwa kinavimba anajiona yy ndio yy, sasa ona hiyo mitusi na nyie wanaume mmezidi kwani bila pesa hamuwezi kuendesha mapenzi?

"]Wadau mmeamkaje,

Jana nilikua pahala natazama mpira huku nakunywa bia taratibu, ghafla akatokea rafiki wa msichana wangu alikuja hapo bar kuchukua chakula, aliponiona akaja kunisalimia, baada ya salaam, nikamwambia shem kwanini usikae na wewe japo upate bia mbili tatu wakati unasubiri chakula? Akakubali

Alipochangamka akaniambia hivi shemu unajua kuwa d anakupotezea muda wako tu hana mpango na wewe, akatoa simu akanionesha msg za whatsaap walizokua wakichati na msichana wangu muda si mrefu, nilishangaa sana.Kwamba huyo fala mi namchuna tu, hicho kitambi na unavyonijua hivi nampeleka wapi? Zilisomeka msg hizo.

Kwanza jitu lenyewe hata kuvaa halijui, zile nguo zake unaweza kudhani ni choir master wa kanisa wadau nilisoma mengi, ndipo nikashangaa, hiki kitambi siku namtongoza kilikuwepo hakikuwepo? Kilikuwepo

Mavazi haya anayodai ni ya kanisa ndio sare za kazini, ila weekend napiga pensi au jeans na t shirt, kwa hiyo anataka niende kazini na jeans?Anadai huwa nampeleka gesti za elfu tano tano, sasa alitakaje? Yaani nimpeleke bar atumbue vitu ya elfu 40 au 50 then anataka nimpeleke hotel ya elfu 50?

Tuyaache hayo

Usiku wa jana akanipigia simu kumbukeni jioni yake ndipo nimeonana na rafiki yake na kuoneshwa msg, usiku akapiga simu, na kunieleza jinsi anavyonipenda, jinsi anavyopenda muonekano wangu, kwamba nisithubutu kumsaliti kuwa atajaiua, na kuwa amenimiss mno kwamba kwa nn leo hatukuonana, yote tisa kumi akadai unakuja lini kuwaona wazazi wangu unichukue jumla.

Guys which is which now?

Huyu sio jangili kweli?[/QUOTE]
 
Choir master!!!!! ni kweli mavazi ni muhimu badilika hata huyo shem wako ni bia tu ndio zilimchanganya na kuamua kukunyea
 
Kwaya master huyo anakupenda siku izi mabint wengi wanaogopana wengi wanaporana kwa hiyo lazima akuponde hili Rafiki zake wakudharau tumia akili huyo Rafiki Yake amekuwa na ujasiri gani wa kukuonyesha sms ataanza kukushobokea ndio tabia za mabinti wa sasa wewe punguza mawasiliano umuone kama ataenda resi
 
Nakushauri mdau usikurupuke kuchukua hatua yakumwacha huyo msichana wako fanya uchunguzi wa kina kupitia rafiki zake wa karibu naa hata ikibidi ndugu zake, wafanyakazi wenzake kama ni mfanyakazi hizo msg ulizoonyeshwa za whasp ni mazungumzo tu ya kawaida kwa akina dada anaongea hivyo kwa rafiki yake kumpunguza makali nia na mapenzi ya dhati anayo kwako isipokuwa FANYA HIVI Kuanzia sas acha kabisa mpango wakumpeleka gesti hata hotel mwambie awe anakuja gettoni kwako msome tabia zake.. hapo utajua anapendelea nini na hapendelei nini je, anapenda usafi wa nyumba, mapishi au mvivu anapenda kulalalala? saa ingine mjaribu kumwomba simu yake uitumie ww kupiga simu kwa ndugu zake unaowafaham ni kama mtego msikilize atakwambiaje.. pia kabla hajaondoka geto mwambie akufulie nguo na kuzipasi utagundua mambo kadhaa kwa huyo binti...mwangalie sana anapopokea simu za watu mbalmbal anajibje anaonyesha mashaka kupokea au anapotezea ukiwepo karibu nae? kama haya hayatoshi niambie nitakupa mengine mazuri...kwa leo ni hayo...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom