Hii
mada nimeikuta kwenye jamvi langu la zamani kabla sijahamia huku. Kwa
kuwa lile jamvi ni kama limekufa na mwanandoa huyu anahitaji sijui ni
msaada au anataka tujifunze, basi nimeileta humu na nimemtaarifu afate
majibu yake humu.
Please nisaidieni jamani: Mimi nimeolewa miaka 15 sasa na tumejaaliwa
watoto 4. Ndoa yetu ilipofikisha miaka 4-5 mume wangu alicheat,
nikamkamata through sms akapinga sn lakini baadae alikubali akakiri
kosa na kuomba msamaha. nikamsamehe Tumeendelea kuishi na nilipopata
mtoto wa tatu akanicheat tena, safari hii alikuwa nje ya nchi kimasomo,
napo alikiri na kuomba msamaha, nikamsamehe wakati niko mjamzito
mimba ya mtoto wa nne alinicheat tena, kibaya zaidi alinicheat na house
girl wng akampa ujauzito. kwa ivo wkt mimi nina mimba na House girl
naye mjamzito(japo sikujua km house girl alikuwa mjamzito kwani
aliondoka nyumbani) niligundua baadae kuwa mtt wa aliyekuwa house Girl
wangu ni wa mume wangu kama kawaida yake akaomba msamaha safari hii
hadi kupiga goti na kulia ili nimsamehe...na mimi kwa kuwa bado
nampenda na nimemvumilia kwa mengi nikaamua kumsamehe tena..ila
tulikubailana masharti mengi na akakubali masharti yote niliyompa..
mwanzoni alibehave vizuri sn akawa muwazi kwng hanifichi chochote
kuhusu huyo mtoto.. na tuliishi maisha ya furaha kwn alinijali mno na
alionekana kweli amerigrate. sasa cha kushangaza siku za karibuni
amebadilika san, amekuwa msiri na hasemi chochote kuhusu huyo mtt wa
nje..siku hizi anatuma hela kwa siri na pia anawasiliana na huyo mama
wa mtoto kwa siri haniambii chochote.. nilipoona mabadiliko niliamua
kumuuliza imekuwaje tena mbona siri tena wkt tulikubaliana kila kitu
kiwe open? hakunijibu isipokuwa alikuwa mkali na kufoka na kusema hilo
swala tumeshamalizana nalo sitaki kulisikiasikia tena.. nikajaribu tena
siku nyingine kumuuliza na majibu ndio hayo hayo, kwa kifupi hataki na
anakwepa kuzungumzia hilo suala kabisa...sasa najiuliza kwa nini
anafanya siri? km hakuna jambo lolote baya basi anaficha nini? ina
maana kuna kitu zaidi ya mtoto.
Sasa jamani mimi nimeamua km ifuatavyo 1. Na mimi nimeamua kuwa na
mahusiano nje ya ndoa, jamani msinilaumu nami pia nahitaji kuliwazwa na
kufarijiwa kwa kifupi nimechoka na mastress yasiykuwa na mwisho,
sikuwahi kumcheat mume wng ktk maisha yote ya ndoa. ila sasa
atanisamehe tu ht akijua wl sijali , nipo tayari kwa lolote.. 2. Sina
mpango wa kuondoka kwenye nyumba tuliyojenga pamoja nitaishi hapa hapa
kwani sipendi wtt wng walelwe na mzazi mmoja..wtt hawajui
kinachoendelea in fact hata ndugu na jamaa hawajui chochote kwani mimi
sijawaambia na wala sijawahi kuwaeleza matatizo ya ndoa yng..kwa nje
tunaonekana familia iliyobarikiwa na ina furaha lkn wenyewe ndio
tunaojua ndani kukoje 3. Kwa sababu sisemagi matatizo yangu kwa ndugu
na marafiki nimeamua kuweka hapa labda nitapunguza kitu fulani kichwani
kwani sometime naona km nazidiwa mawazo vile.