Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,946
- 38,668
Hapa nazungumzia wimbi kubwa la wezi wanaotumia mitandao ya simu kuwaibia mawakala wa huduma za simu pesa.
ndani ya mwezi wa nane nimeshuhudia mawakala zaidi ya watano wakiibiwa floats zao kupitia mitandao. wengi wa wezi hao wamekuwa wakitumia mbinu ya kuwapigia waajiriwa w mawakala wakijinasibu kwa namba za mwajiri wao wakitaka watumiwe floats huku wakitumia namba zikisomeka kama mwajiri wao. halafu wanatoa maelekezo kwa sms kuwa fedha zitumwe kwenye namba wanazoelekeza. hapo bosi wa duka akipigiwa muda huo anakuwa hapatikaniki na huku namba yake ikituma sms kuwa yupo bize atumiwe sms.
Wakishafanikiwa kuiba ndipo hata msaidizi wa duka anaweza kumpigia bosi wake akitaka. na mara nyingi hupiga kuthibitisha transaction, hapo ndipo wanagundua wamepigwa.
kwa nini nazituhumu kampuni za simu. Ni kuwa hata taarifa itakapoolewa haraka kwa opareta wa huduma kwa wateja majibu ama ushirikiano unakuwa haupo. na namba iliyopokea pesa inapowasilishwa kwa opareta huwa hakuna msaada hata wa kuzuia wasifanye transactions zingine. ifahamike kwamba watumiaji mitandao huwa wanasajili kabla hawajaanza kutumia line ya simu, pia wanatoa picha zao na server za kampuni za simu huweza kurekodi IMEI ya simu wanazotumia ambapo mara nyingi hutumia line nyingi kwa simu moja kufanikisha uhalifu wao.
Nina imani kwamba wahusika wa wizi aina hii wapo ndani ya kampuni za simu na wanalindwa kwa sababu mtandao wa wizi huu ni mkubwa na wanalindana. Juzi nimeshuhudi duka moja la wakala akiibiwa shs milioni tatu kwa njia hiyo....
Mashaka yangu kwa hizi kampuni za simu hayaishi labda nielimishwe kwa namna gani hawahusiki na ujambazi wa cold blood