Kampuni za Kitanzania zenye majina makubwa hazijiandikishi soko la hisa(DSE)

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,370
3,956
Hivi hii hali inasababishwa na nini? Utakuta kampuni kubwa tu na ina mafanikio pamoja na malengo kadhaa ya ukuaji, lakini hawaoni haja ya kuhusisha wananchi wengine katika umiliki wa kampuni zao (kitu ambacho kingewaongezea mtaji).

Au hawana imani na kushirikisha watu wengine katika kampuni yao na wataona labda wanapoteza kwa kiasi fulani umiliki wa kampuni zao? Au hawana shida na mitaji? Ila sidhani kama kuna aliyetosheka mtaji, na wengi wao makampuni makubwa yanajidai kutoa ajira nyingi kwa Watanzania na uchangiaji wa pato la taifa.

Ila wakae wakijua duniani kote wale wote walioandikisha kampuni zao katika masoko ya hisa ya kwao ndio wale ambao makampuni yao yana thamani kubwa kwa sasa Afrika (Dangote) na Marekani (Apple, Google na wengine).

Au labda wanadanganya usoni kuwa milling, transport, petroleum, mobile telephone, soft drinks vinalipa kumbe wanafanya magumashi yao kupata faida nono, au ndio wale production nzima haifuati usalama wa kazini, udhibiti wa bie products zao na uajiri (kuajiri kwa kigezo flani tu).

Au wadau mnasemaje?
 
Hao wanaoongoza DSE ndo wanashindwa kufanya marketing watu waijue! Sasa uandijishe kampuni wakati wanunuaji wa hisa hakuna serikalin ingeweka sheria dse wajtangaze bure radio/ TV za serikalin ili kuboost soko na uchumi
 
Hii nchi mambo mengi bado, angalia Nairobi Stock Exchange, aibu, au Nigeria, balaa, sie hapa kuna makampuni potential kabisa wala hata hayako listed, sababu wanajua wakiwa listed maanake info. Ziwe public na wao kodi, na sheria zingine kama kazi, mazingira nk. Ni magumashi unatemegea nn, hii bongo mtu ukisema ukweli unaonekana mbaya.
 
Kwanza inabidi ujiulize kwanini wauze hisa? Mtu anauza hisa anapohitaji mtaji wa kupanua biashara au kuongeza kitu fulani ndani ya kampuni.

Makampuni ya simu karibu yote yanamilikiwa toka nje ya Tanzania ambapo makampuni mama yamekuwa listed kwenye stock exchanges zao.
 
Mara nyingi kuuza kwa hisa kunaambatana na ukuaji wa kampuni yenyewe(under ideal conditions), ukiwasoma au kuwasikiliza baadhi yao wana malengo makubwa sana ya kuzikuza kampuni zao na wanatumia mikopo ya banks mbalimbali,kwanini wafanye hivi?wakati njia rahisi ipo kutenga baadhi ya hisa na kuziuza na wao wenyewe kuendelea kumiliki asilimia ya kutosha tu.

Na kwa kuwamilikisha wananchi na ndio pale suala la nunua bidhaa za kitanzania litakapo kubaliwa 100% na wananchi sababu wakiwa na umiliki wanajua wananunua bidhaa zao wenyewe.

Siongelea makampuni ya simu pekee naongelea makampuni mengine ya watanzania kama vile SSB,MeTL,IPP Media,Dar Express Ltd na mengine ya kaliba kama hii.
 
Last edited:
Hii nchi mambo mengi bado, angalia Nairobi Stock Exchange, aibu, au Nigeria, balaa, sie hapa kuna makampuni potential kabisa wala hata hayako listed, sababu wanajua wakiwa listed maanake info. Ziwe public na wao kodi, na sheria zingine kama kazi, mazingira nk. Ni magumashi unatemegea nn, hii bongo mtu ukisema ukweli unaonekana mbaya.
Naona unakubaliana na mimi kua wakiwa public wataingiliwa na serikali kirahisi kwa kufatiliwa kila hatua kuanzia safety regulations, quality control,waste treatment, ajira za mikataba ,na mwisho wa siku uwatangazie wananchi financial statements za kampuni!!wakifikiria haya wanaona duuuhhh hapana ila wanakosea.

Unavosema hizo stock exchanges nyingine ni aibu unamaanisha market capitalization yao ni kubwa sana au vp???
 
Hao wanaoongoza DSE ndo wanashindwa kufanya marketing watu waijue! Sasa uandijishe kampuni wakati wanunuaji wa hisa hakuna serikalin ingeweka sheria dse wajtangaze bure radio/ TV za serikalin ili kuboost soko na uchumi
Hapana sikubaliani na wewe,watu wanaijua sana tu,rejea hisa za NMB walivotoa mara ya kwanza zilikua oversubscribed.
 
Serikali yenyewe haitaki wajiunge maana itazuia upigaji dili kwny kukwepa kodi. Mfano wizara ya Nishati na Madini imegoma kutunga kanuni zitakazolazimisha makampuni ya madini kujiunga DSE licha ya sheria ya madini kutaka hivyo.
 
Naona unakubaliana na mimi kua wakiwa public wataingiliwa na serikali kirahisi kwa kufatiliwa kila hatua kuanzia safety regulations, quality control,waste treatment, ajira za mikataba ,na mwisho wa siku uwatangazie wananchi financial statements za kampuni!!wakifikiria haya wanaona duuuhhh hapana ila wanakosea.

Unavosema hizo stock exchanges nyingine ni aibu unamaanisha market capitalization yao ni kubwa sana au vp???

Mkt cap. Angalia pia volume, turnover hata no . Of deals, indeces pia
 
Serikali yenyewe haitaki wajiunge maana itazuia upigaji dili kwny kukwepa kodi. Mfano wizara ya Nishati na Madini imegoma kutunga kanuni zitakazolazimisha makampuni ya madini kujiunga DSE licha ya sheria ya madini kutaka hivyo.
Kwahyo unasema wakiingia sokoni watakua hawapigi madeal ya kukwepa kodi tena?
 
Mara nyingi kuuza kwa hisa kunaambatana na ukuaji wa kampuni yenyewe(under ideal conditions), ukiwasoma au kuwasikiliza baadhi yao wana malengo makubwa sana ya kuzikuza kampuni zao na wanatumia mikopo ya banks mbalimbali,kwanini wafanye hivi?wakati njia rahisi ipo kutenga baadhi ya hisa na kuziuza na wao wenyewe kuendelea kumiliki asilimia ya kutosha tu.

Na kwa kuwamilikisha wananchi na ndio pale suala la nunua bidhaa za kitanzania litakapo kubaliwa 100% na wananchi sababu wakiwa na umiliki wanajua wananunua bidhaa zao wenyewe.

Siongelea makampuni ya simu pekee naongelea makampuni mengine ya watanzania kama vile SSB,MeTL,IPP Media,Dar Express Ltd na mengine ya kaliba kama hii.

Binafsi ninaweza kuwa na majibu matatu;

1. Kampuni nyingi zinaendeshwa kienyeji sana na short cuts nyingi, kwahyo ukisema wawe listed ni kama kampuni inakufa au hawataweza kupitia short cuts zao.

2. Kampuni nyingine wameamua kuweka biashara zao kwenye level za familia zaidi, hayo mambo ya public listing hawataki hata kusikia.

3. Inawezekana wamiliki wa makampuni mbalimbali hawana elimu tosha juu ya faida za kulist kampuni yako DSE.
 
Serikali yenyewe haitaki wajiunge maana itazuia upigaji dili kwny kukwepa kodi. Mfano wizara ya Nishati na Madini imegoma kutunga kanuni zitakazolazimisha makampuni ya madini kujiunga licha ya sheria ya madini kutaka hivy
Kwahyo unasema wakiingia sokoni watakua hawapigi madeal ya kukwepa kodi tena?

Wakiingia sokoni kila kipato kitakuwa wazi kiasa kwamba hadi wananchi watakuwa na haki ya kuchunguza kwa hiyo ukwepaji utakuwa mgumu
 
Ujanja ujanja mwingi kwenye biashara ya haya makampuni na mfumo Mzima wa hisa Bado ni msamiati nchini hakuna mwamko
 
Back
Top Bottom