Kampuni ya vifaa vya michezo ya 'Puma' imetangaza kuacha kuifadhili timu ya Taifa ya Israel ifikapo mwaka 2024

Adrian2716

Member
Oct 23, 2023
98
293
Kupitia taarifa iliyotumwa kwa barua pepe kwa shirika la habari la Reuters, Msemaji wa kampuni Puma amebainisha kuwa mikataba ya kampuni hiyo na baadhi ya mashirikisho ikiwemo Serbia na Israel, itakoma ifikapo 2024 na kwamba mikataba hiyo haitaongezwa.
.
Ikumbukwe kwa muda mrefu Puma imekuwa ikishinikizwa kusitisha ushirika wake na Shirikisho la Soka la Israel (IFA), ambapo mashinikizo hayo yameongezeka zaidi tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel, huko Gaza, ambayo yamedaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 18,000. #via #Aljazeera
 
Puma wakizingua adidas, nike, reboek, ascis, new balance, fila, umbro na wengine wengi wanaingia mzigoni
 
Na huku Nchini Tansania Jesh la wananch limetoa onyo kali kwa magaidi wa IDF kusitisha mara moja vitendo vya kigaidi huko Gaza la sivyo litaingilia kati
Na Rais ameshamwita waziri Mkuu Netanyahu ajieleze sababu kubwa ya kuendeleza vita
 
Back
Top Bottom