Kampuni ya ujenzi inahitaji "partner" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni ya ujenzi inahitaji "partner"

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Congo, Aug 10, 2010.

 1. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Jambo wandugu, nina kampuni ya ujenza Class VII. Imesajiliwa na ina leseni zote lakini kwa bahati mbaya haipati kazi kwa sababu mbalimbali. Natafuta mtu ambaye ana uwezo wa kupata kazi lakini hana kampuni wala mtaji akajiunga nasi ili tutafute kazi kwa pamoja. Awe na uwezo wa kusimamia kazi zitakazopatikana. Kampuni ninayo na mtaji upo lakini kazi sina. Tutazungumza namna gani ya kugawana mapato yatayopatikana. Kama una interest tafadhali ni-pm.
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nyie ndio mnaoangusha majumba kwa kujenga bila viwango? Teh teh teh ... .... Unataka utajiri kwenye fani ambayo hata huielewi. Tangaza kazi na uwalipe professionals kiwango kinachotakiwa na wao kwa kutumia usomi wao na qualifications zao watapata kazi. Kama kweli mpunga unao kama unavyosema tangaza kumtafuta managing director aliyebobea na weka sifa zake wako wengi tu siku hizi hapa bongo. Angalia wasikuletee vyeti vya kugushi. Good luck.
   
 3. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu.WEKA MAELEZO YA KUTOSHA ILI WATU WAJUE NA WAKUPE USHAURI, KWA NINI UKOSE KAZI ZA KUFANYA?!, AU KUNA TATIZO KATIKA USIMAMIZI WA KAMPUNI YAKO?.SASA UTAWEZA VIPI KUPATA MSHIRIKA PASIPO KUWA MUWAZI JUU YA MATATIZO YANOISIBU KAMPUNI YAKO?.
   
 4. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo zaidi ni-pm. Hakuna tatizo.
   
 5. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Fani ya utajiri ni ipi? Nadhani unatakiwa kurudia kusoma nilichoandika. Isingesajiliwa bila kufuata taratibu zote.
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Fani yoyote inaweza kukupa utajiri. Kusajiliwa kampuni sio kazi kubwa sana lakini ku-prove competence kwenye hiyo fani/kampuni (what you do with it, type of work etc.) ndio tatizo, na hilo unaliona baada ya kushindwa kupata kazi. Ukisoma my post nimesema tafuta Managing Director/advertise the position kwa sababu wewe mpunga upo utawapata tu hapa bongo wapo wengi sana.
   
 7. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mkuu fafanua iko mkoa gani na inahusika na ujenzi wa nini?visima maghorofa madaraja au magari?
   
 8. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  MIAFRIKA ndivyo ilivyo! Amesema kwa maelezo zaidi mum-pm, nyie maneno meeeeeeeengi! Heh!
   
 9. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Civil na Building. Iko Dar es Salaam, lakini leseni za ujenzi ni pan territorial.
   
 10. babalao

  babalao Forum Spammer

  #10
  Aug 14, 2010
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ushauri uliopewa wa kutafuta meneja mzuri ungeuzingatia kwani unachohitaji siyo partner unahitaji raslimali watu ambayo inaweza kukutafutia kazi na kuzisimamia kazi zako partners watakusumbua ajiri mtu.
   
 11. M

  MAKOLA Member

  #11
  Aug 20, 2010
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  waungwana nina mitiki 150 ina umri wa miaka 20. Nipeni bei tangaza dau. Miti ipo maeneo ya tanga handenoi
   
 12. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mitiki huwa nasikia ni dili sana.....lakini ulichokosea mkuu makola ni kuchomekea mada kwenye thread ya Jamaa wa kampuni ya ujenzi.

  Ushauri wa bure kama bado hujafanya, ni vizuri ukaanzisha thread yako kwenye section ya habari na hoja mchanganyiko
   
Loading...