Kampuni ya Songas imetishia kusitisha uzalishaji wa umeme kutokana na mgogoro baina yake na TANESCO

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,311
152,112
Wakati sukari ikikosekana na kupanda bei kila kukicha,janga la kukosekana umeme nalo linapiga hodi. Kampuni ya kufua umeme ya Songas imetishia kuzima mitambo yake ya kuzalisha umeme kuanzia Jumatano wiki hii kutokana na mgogoro baina yake na TANESCO ambapo kamupuni hiyo inaida TANESCO zaidi dola milioni 90.

Hata hivyo,Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Eng.Mramba amewatoa hofu wananchi kufuatia taarifa hiyo ya Songas na ameongeza kuwa Songasi kusitisha uzalishaji wa umeme ni kwenda kinyume na mkataba na amesema TANESCO wataipeleka kampuni hiyo mahakamani iwapo itatekeleza uamuzi wake huo wa kusitisha uzalishaji wa umeme.Mramba ameongeza kuwa makampuni kudaina katika biashara ni jambo la kawaida.

Chanzo:ITV

Binafsi niliwahi kuhoji hapa JF,ingawa kuna watu walinibeza, kama uamuzi wa TANESCO kushusha bei ya umeme ulikuwa ni uamuzi wa TANESCO yenyewe au ilikuwa ni shinikzo la watu fulani maana hapa chanzo cha mgogoro ni TANESCO kushindwa kuwalipa Songas fedha zao.

=====================

Mvutano Tanesco, Songas watishia nchi kuwa gizani


KAMPUNI ya Songas Limited, inayozalisha umeme kwa kutumia gesi asilia, imetishia kuzima mitambo ya kuzalisha nishati hiyo kuanzia kesho kutokana na kulidai Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

KAMPUNI YA SONGAS LIMITED.
Songas ambayo inazalisha na kuingiza megawati 198 kwenye gridi ya taifa, imesema inaidai Teneco zaidi ya Sh. Bilioni 179.28, kutokana na kuiuzia umme huo.

Tanesco, kupitia kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wake, Felichismi Mramba, imethibitisha kudaiwa na kampuni hiyo lakini haikutaja kiasi kwa madai kuwa ni kinyume cha kanuni na kwamba kwa kutaja kiasi inachodai, songas imekiuka masharti ya mkataba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Songas, Nigel Whittaker, alisema kampuni hiyo imeshindwa kuendesha shughuli za uzalishaji kutokana na kukosa fedha.

“Tumeamua kuzima mitambo yetu ifikapo Jumatano (kesho) usiku, kwa sababu hatuna fedha za kuendeshea mitambo,” alisema.

Whittaker alisema tangu Januari, mwaka huu, kampuni hiyo ilitakiwa kusitisha shughuli zake, lakini Tanesco na serikali waliwaomba kuendelea na uzalishaji.

“Songas inapata mapato mengi kutoka Tanesco, ambao ndio wateja wake, hivyo kama ilivyo kwa kampuni yoyote binafsi haiwezi kugharamia shughuli zake za kiuendeshaji bila kulipwa kwanza na kwamba mapato ambayo Songas inayapata yanarudishwa tena kwenye biashara kwa ajili ya kulipia gharama za uendeshaji na matengenezo, kodi na kulilipa Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC),” alisema.

Alisema Desemba, mwaka jana, Songas iliingia makubaliano na Tanesco kuwa ifikapo Aprili, mwaka huu, ingekuwa imemaliza malimbikizo yote lakini hadi jana ilikuwa haijatekeleza ahadi hiyo.

“Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, Tanesco, Wizara ya Nishati na Madini na Songas tuliafikiana namna ya kulipa malimbikizo ya nyuma. Malimbikizo yanaendelea kukua na shughuli za uendeshaji za Songas zinakuwa hatarini tena,” alisema.

“Singas ni wachangiaji wakubwa wa uchumi wa nchi. Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, sisi tumeonyesha uvumilivu wetu na dhamira ya wananchi kwa kuendelea kufanya kazi. Tumekuwa tukisubiri Tanesco kutekeleza ahadi za kutoa fedha inazodaiwa lakini haijafanya kama tulivyokuwa tunatarajia,” alisema.

Tangu mwaka 2014, Songas imekuwa mchangiaji mkubwa wa sekta ya nishati nchini, kwa kutumia gesi kutoka Songosongo mkoani Mtwara na kusambaza kwa kuchangia asilimia 20 kwenye gridi ya Taifa.

Tanesco yajibu mapigo

Wakati hatua hiyo ya Songas ikizua hofu ya kukosekana kwa umeme, Mramba amesema tayari Songas imeshazima asilimia 81 ya mitambo yake, lakini huduma za umeme zimeendelea kupatikana kutokana na kuwapo kwa maji mengi.

“Tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa masuala yanayohusu kampuni ya Songas yanashughulikiwa na Tanesco pamoja na serikali na huduma ya umeme itaendelea kupatikana nchini,” alisema mramba alipozungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Mramba alisema hakuna athari zozote zitakazotokea kutokana na hatua hiyo ya Songas na kuwahakikishia Watanzania kuwa umeme utakuwa wa uhakika.

“Hatua ambazo Songas imezichukua ni kinyume cha mkataba wetu. Kifungu cha 4.4 cha mkataba kinaitaka kuandika notisi ya siku 90 za kuwa na majadiliano na kama haitaridhishwa inatakiwa kutoa notisi nyingine kwa serikali ya siku 90 kwa mujibu wa kifungu cha 4.6,” alisema Mramba.

Alifafanua kuwa: “Kifungu cha 17 cha mkataba kinakataza na kuzuia moja ya pande zote kutoa taarifa za mkataba na masuala yanayohusu mkataba kwa vyombo vya habari au yeyote asiyehusika katika mkataba bila kupata ridhaa ya upande mwingine.”

Alisema hatua ambazo Songas wamechukua ni kuwapa hofu wananchi, kuichafua Tanesco na serikali.

Chanzo: IPP Media
 
Kampuni ya kufua umeme ya Songasi imetishia kusitisha uzalishaji wa umeme(kama sikosei ni kuanzia Jumatano) kutokana na mgogoro baina ya kampuni hiyo na TANESCO.

Hata hivyo,Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Eng.Mramba amewatoa hofu wananchi kufuatia taarifa hiyo ya Songasi na ameongeza kuwa Songasi kusitisha uzalishaji wa umeme ni kwenda kinyume na mkataba na amesema TANESCO wataipeleka kampuni hiyo mahakamani iwapo itatekeleza uamuzi wake huo wa kusitisha uzalishaji wa umeme.

Chanzo:ITV

Binafsi niliwahi kuhoji hapa JF,ingawa kuna watu walinibeza, kama uamuzi wa TANESCO kushusha bei ya umeme ulikuwa ni uamuzi wa TANESCO yenyewe au ilikuwa ni shinikzo la watu fulani maana hapa mgogoro bila shaka ni deni la TANESCO kwa Songasi(sikusikia vizuri chanzo cha mgogoro ni nini hasa ila bila shaka ni hili deni tu).
Economic hit men hao, wawahiwe mapema sana pls!
 
Kampuni ya kufua umeme ya Songasi imetishia kusitisha uzalishaji wa umeme(kama sikosei ni kuanzia Jumatano) kutokana na mgogoro baina ya kampuni hiyo na TANESCO.

Hata hivyo,Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Eng.Mramba amewatoa hofu wananchi kufuatia taarifa hiyo ya Songasi na ameongeza kuwa Songasi kusitisha uzalishaji wa umeme ni kwenda kinyume na mkataba na amesema TANESCO wataipeleka kampuni hiyo mahakamani iwapo itatekeleza uamuzi wake huo wa kusitisha uzalishaji wa umeme.

Chanzo:ITV

Binafsi niliwahi kuhoji hapa JF,ingawa kuna watu walinibeza, kama uamuzi wa TANESCO kushusha bei ya umeme ulikuwa ni uamuzi wa TANESCO yenyewe au ilikuwa ni shinikzo la watu fulani maana hapa mgogoro bila shaka ni deni la TANESCO kwa Songasi(sikusikia vizuri chanzo cha mgogoro ni nini hasa ila bila shaka ni hili deni tu).
Mkuu mbona nadhani nadhania, kama sikosei nyingi hapo juu. Kwani hao Songas hawajasema kwa nini wanataka kuzima umeme? Songas wanaidai TANESCO kiasi gani?
Kwa hiyo u ataka kusema kwamba Songas wanataka kuhodhi umeme kama akina Zakaria walivyohodhi sukari?
 
Mkuu mbona nadhani nadhania, kama sikosei nyingi hapo juu. Kwani hao Songas hawajasema kwa nini wanataka kuzima umeme? Songas wanaidai TANESCO kiasi gani?
Kwa hiyo u ataka kusema kwamba Songas wanataka kuhodhi umeme kama akina Zakaria walivyohodhi sukari?
Ni kwasababu watu wengi si wafuatilaji wa mambo.Mgogo wa TANESCO na Songasi kuhusu TANESCO kutolipa deni lake kwa Songas uliripotiwa na gazeti la The Guardian kama mwezi mmoja uliopita na Songasi walikuwa wanatishia kuzima mitambo yao kwahiyo hii habari ni muendelezo tu.
 
Nina wasiwasi sana na na mambo yanavyokwenda nchin kwetu,Mungu atusaidie kwa kweli maana wngi twaweza kuwa affected sababu ya wachache
 
Tanesco wanadaiwa mahela mengi tu,za kulipa hawana wanapiga siasa.....kwa heri viwanda kwa heri tanzania ya viwanda,kwa heri maendeleo,ole wao watakaoficha umeme.....ntapeleka takukuru wakawashe
sie tunao tumia umeme wa solar itakuwaje sasa?
 
Kwani songas wakizima mitambo yao tanzania itaingia gizani mi nadhani sio kweli sababu tanzania kuna plants nyingine kama nne zinazozalisha umeme kutumia maji ambazo zingaingiza megawati zake katika grid ya taifa,hapo bado plants zinazotumia gesi
 
Back
Top Bottom