Kampuni ya Petra Diamonds matatani kifedha

Kampuni ya Petra Diamonds matatani kifedha

GTA

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
878
Reaction score
653
_98239440_4d436c1d-833b-41c7-9f9e-6e5c1cd0ba48.jpg

Pete iliyopambwa kwa almasi kutoka kwa mgodi wa Cullinan
Kampuni moja ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa za uchimbaji madini ya almasi Afrika, Petra Diamonds, imetangaza kwamba inakumbwa na matatizo ya kifedha.

Kampuni hiyo, ambayo huendesha shughuli zake Afrika Kusini na Tanzania, imesema kwamba kuna uwezekano ikashindwa kulipa mikopo yake kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Mapema mwezi uliopita, maafisa wa serikali nchini Tanzania walitwaa kipande cha almasi kutoka kwenye mgodi wa Williamson, wakisema thamani yake kamili haikuwa imefichuliwa.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa madai sawa na hayo karibuni, hasa kuhusu migodi ya dhahabu nchini humo.

Wachanganuzi hawajashangazwa na tangazo la Petra kwamba huenda wakashindwa kutimiza wajibu wao katika kulipa mikopo.

Lakini hisa za kampuni hiyo katika soko la hisa la London zilishuka thamani kwa asilimia tano Jumatatu asubuhi.

Petra wameahidi kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yao watakapotangaza matokeo ya kifedha ya kila mwaka wiki ijayo.

Ni pigo kubwa kwa Petra, ambao wameathiriwa na mzozo kuhusu wafanyakazi katika migodi yake Afrika Kusini na kukazwa kwa sheria za uchimbaji madini Tanzania.

Shughuli nyingi za Petra huwa Afrika Kusini ambapo wanamiliki miongoni mwa migodi mingine, mgodi maarufu wa Cullinan.

Lakini mgomo wa wachimbaji madini umeathiri sana shughuli katika migodi yake Afrika Kusini, hata ingawa mkataba wa miaka mitatu kuhusu ujira ulitiwa saini wiki iliyopita.
Credit - bbcswahili.com
 
Ccm ndio inayoongoza Afrika ya Kusini...!!

Kila kitu wa copy na ku-paste..Rangi (sare ya chama) Nyimbo ya Taifa...Ufisadi.... nao kwa sasa nchi imewashinda...!!
 
Kampuni moja ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa za uchimbaji madini ya almasi Afrika, Petra Diamonds, imetangaza kwamba inakumbwa na matatizo ya kifedha. Kampuni hiyo, ambayo huendesha shughuli zake Afrika Kusini na Tanzania,

imesema kwamba kuna uwezekano ikashindwa kulipa mikopo yake kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Ni pigo kubwa kwa Petra, ambao wameathiriwa na mzozo kuhusu wafanyakazi katika migodi yake Afrika Kusini na kukazwa kwa sheria za uchimbaji madini Tanzania.

Shughuli nyingi za Petra huwa Afrika Kusini ambapo wanamiliki miongoni mwa migodi mingine, mgodi maarufu wa Cullinan. Lakini mgomo wa wachimbaji madini umeathiri sana shughuli katika migodi yake Afrika Kusini, hata ingawa mkataba wa miaka mitatu kuhusu ujira ulitiwa saini wiki iliyopita.

Mapema mwezi uliopita, maafisa wa serikali nchini Tanzania walitwaa kipande cha almasi kutoka kwenye mgodi wa Williamson, wakisema thamani yake kamili haikuwa imefichuliwa.

Serikali ya Tanzania imekuwa ikitoa madai sawa na hayo karibuni, hasa kuhusu migodi ya dhahabu nchini humo.

Wachanganuzi hawajashangazwa na tangazo la Petra kwamba huenda wakashindwa kutimiza wajibu wao katika kulipa mikopo. Lakini hisa za kampuni hiyo katika soko la hisa la London zilishuka thamani kwa asilimia tano Jumatatu asubuhi. Petra wameahidi kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yao watakapotangaza matokeo ya kifedha ya kila mwaka wiki ijayo.

Source: Bbc
 
  • Thanks
Reactions: Bky
Tatizo mkuu ukishakuwa mwanaccm sijui akili zinaenda wapi? mambo yako wazi hapo sioni ugumu.
Mambo gani yapo wazi, kuwa specific like a sane man unlike nyumbu.
Kwani si walikuwa wanatuibia ukweli, au unawatetea hawakuwa wanatuibia, angekuwa raisi Mbowe au Lisu ungetaka awaachie?
Na article si inasema wazi wafanyakazi wao wa SA wamegoma.
Sasa ni uwazi gani unaoongelea na kuutetea. Usitumie akili za nyumbu kwenye mada kama hizi, unaonekana punguani
 
Kwenye group lenu la madog wa CCM wewe ndiyo wamekuteua kujibu hoja mkuu? pole sana mkuu na hivi unamkia butu.
 
Back
Top Bottom