Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,852
Baada ya jana kusoma habari inayolitaka gazeti la Mwanahalisi kumuomba radhi Rais,leo nimetafuta gazeti hilo kuona nini hasa kilichoandikwa katika habari husika na nimefanikiwa kupata nakala ya hilo gazeti.
Kichwa cha habari kinasomeka kama ifuatavyo:
"Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM"
Na aya ya kwanza kabisa katika habari husika inasomeka:
"Ofisi ya Raisi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),kupitia shirika lake la Elimu Kibaha,imejifunga katika mikataba mitatu tofauti na kampuni ya kigeni ya Organia Limited,kinyume cha sheria za nchi,Mwanahalisi limeelezwa"
Kichwa kidogo chini yake kinasomeka:
"Mikataba yoye hii iliyokodishwa na shirika, serikali imeambulia kiasi kisichozidi sh.320 milioni,lakini lenyewe linadaiwa zaidi ya Sh.9 7 bilioni."
Ukiendelea kusoma habari nzima hakuna mahali pengine popote JPM ametajwa kuhusika kwa aina yoyote ile zaidi ya kutajwa tu kwa neno ofis ya Raisi, TAMISEMI katika aya ya pili na zaidi ya hapo ni maelezo ya tuhuma za kampuni hiyo na shirika hilo la Elimu Kibaha.
Hapo nakuachia mwenyewe utafakari habari hiyo na wenye gazeti kutakiwa kuomba radhi.
Sasa tukirudi kwenye mada,kampuni hiyo ya Organia Limited inamilikiwa na nani?
Kampuni hii tunaambiwa katika hii habari kuwa inajihusisha na shughuli za ufugaji na kilimo hai nchini Tanzania.
Kwa nyongeza,gazeti linaripoti kwa Waziri wa TAMISEMI,George Simbachaweni amewasilisha ripoti mbele ya kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu shirika la Elimu Kibaha ambayo inaonyesha kumekuwapo ukiukwaji mkubwa wa taaratibu za uwekezaji na upotevu wa mali ya umma.
Aya moja inasomeka:
"Waziri wa Simbachaweni ananukuliwa akiliambia Bunge kuwa ubadhirifu ndani ya shirika hilo umesababisha kuwapo kwa deni la Sh.6.3 bilioni ambalo ni kubwa kuliko mali za shirika.
Hiyo ni summary tu ya hii habari lakini napenda kujua ni nani hasa mmiliki/wamiliki wa hii kampuni.
Tuanzie hapo.
"