Kampuni ya kitalii ya Wengert Windrose Safaris yamuumbua Waziri Maghembe

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,659
2,822
KAMPUNI ya Wengert Windrose Safaris (Tanzania) Limited (WWS), imesema kauli iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwamba Mahakama Kuu ilitoa amri kwa waziri ikimtaka kuirudishia Green Miles Safari Co. Limited (GML) kibali cha uwindaji na kitalu ambacho kinaendeshwa na WWS sio za kweli.

Taarifa ya WWS iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari ilifafanua kuwa hakuna uamuzi wowote uliotolewa na Mahakama ukitamka au kuamua kwamba GML ndio mmiliki halali wa kitalu cha uwindaji ambacho sasa kinaendeshwa na WWS.

Waziri Maghembe alitoa kauli hiyo wiki iliyopita wakati anajibu hoja za wabunge bungeni. Kampuni hiyo pia ilisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa Mahakama haikuwahi kuamuru Wizara ya Maliasili na Utalii kuirudishia GML leseni ya uwindaji na vitalu vya uwindaji vilivyonyang’anywa kutokana na maofisa wake kudaiwa kushiriki uwindaji haramu katika pori la uwindaji la Selous.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba ukweli kuhusu jambo hilo ni kwamba Agosti 28, WWS ndio ilifungua shauri la madai Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara dhidi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na GML.

Ilieleza kuwa katika shauri hilo WWS ilikuwa ikipinga uamuzi wa waziri kubadilisha jina la kitalu kinachoendeshwa na WWS ili kutoa mwanya wa kitalu hicho kupewa GML. “Walalamikiwa wote hao hawakuwasilisha utetezi wao mahakamani.
 
Hii ni moja kati ya Wizara nono hapa nchini....
Nakumbuka Kashfa ya Loliondo na waziri Bakari Mgumia (Rip)....
Unaweza dhani waziri Magembe kadanganywa kumbe......
 
Kama ni bahati basi Maghembe ana bahati ya kuzaliwa!! Ni watu wenye akili za kukopa tu labda ndo waliamini kuwa JPM angemjumuisha huyu mzee kwenye baraza lake la mawaziri. Hivi kati ya watzd zaidi ya 45M hayupo anayeweza kufanya hii position ya Maghembe??
 
Kama ni bahati basi Maghembe ana bahati ya kuzaliwa!! Ni watu wenye akili za kukopa tu labda ndo waliamini kuwa JPM angemjumuisha huyu mzee kwenye baraza lake la mawaziri. Hivi kati ya watzd zaidi ya 45M hayupo anayeweza kufanya hii position ya Maghembe??
Kila wakat akiteuliwa anakuwa wazir mzigo.. Saivi kawa lumbesaaa kabisaa......

Ila Maghembe Ana BAHAT ya kuzaliwa.....sababu hata kurud Bungen ilikuwa ni BAHAT sana
 
Kama ni bahati basi Maghembe ana bahati ya kuzaliwa!! Ni watu wenye akili za kukopa tu labda ndo waliamini kuwa JPM angemjumuisha huyu mzee kwenye baraza lake la mawaziri. Hivi kati ya watzd zaidi ya 45M hayupo anayeweza kufanya hii position ya Maghembe??

Nadhani ni kautamaduni kale ka kuhakikisha inagalau kila mkoa unakuwa na uwakilishi serikalini wa aidha waziri ama ingalau naibu waziri.

Na kama sijakosea, katika mkoa wa Kilimanjaro ni Jumanne Maghembe pekee ktk CCM aliyeibuka mshindi kama mbunge wa jimbo wa jimbo lake ktk uchaguzi wa mwaka jana, 2015!!

Lakini hata hivyo, Mr President angeweza kutumia option ya "viti maalumu vya Rais" kupata mwakilishi kutoka mkoa huo kuingia serikalini iwapo tu ilikuwa ni lazima saana mkoa huo nao utoe mtu kuingia ktk cabinet!!

Vinginevyo, wengi tunakubali kuwa huyu mzee ni miongoni mwa mizigo mizito ktk serikali hii na hata huo u profesa wake it's a just good for nothing!!
 
Huyu alipewa huo uwaziri kwa bahati mbaya, naona Magu anamuangalia sana anasubiri tu aingie 18 zake kwa style yoyote amtwange.
 
Back
Top Bottom