Kampuni ya Khas ya Moshi na utapeli wao

Kampuni ya Khas ya Moshi na utapeli wao

Solarpanel

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2012
Posts
235
Reaction score
38
Habari wanajamvi, naomba niwajulishe kwa wasiofahamu kampuni hii, kuwa makini na huduma zao. Ni kampuni inayohusika na kutafuta wafanyakazi kama vile housegirl, houseboy, garden boy nk. wao ni middlemen kama ilivyo radar.

Tatizo lao ni kwamba shughuli wanayoifanya ni nzuri endapo wangeifanya kwa intergrity lakini imegeuka usanii mkubwa, wanawapa watu mkataba, na kisha kukupa mfanyakazi asie na kiwango. Pia wanawafundisha uongo mwingi mno wa kudanganya mabosi zao.

Hela wanayolipwa ni kuanzia elfu 80 hadi 120 kwa mwezi, na pindi unapoona mfanyakazi hajitumi na ukaripoti basi wanakuzushia maneno mengi ikiwemo, ukali wa bosi, masimango, na hata kuonekana bosi amemtaka mfanyakazi kimapenz. Yote hiyo ni ili uwe umeshatoa hela na zisiweze kurudishwa kulingana na mkataba.

Hivyo tuwe makini. Sikatai kuwa unaweza pata mfanyakazi mwadilifu ila kwa kiasi kikubwa ni usanii na uongo mwingi

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom