Kampuni ya Fastjet yasitisha safari Kilimanjaro-Nairobi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575




Tanzania imesitisha safari zake kati ya Kilimanjaro na Nairobi. Fastjet ilikuwa ikifanya safari kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi mara mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapaili.

Kusitishwa kwa safari kwenye njia hiyo kunatokana na kuwepo mahitaji haba ya abiria kwenye masoko yote mawili ya Kilimanjaro na Nairobi hali iliyosababisha kutokuwa na manufaa kibiashara. Shirika hilo limeeleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha linarudisha safari hizo kati ya Kilimanjaro- Nairobi pindi tu na wakati ambapo wateja wataihitaji.

Safari za fastjet kutoka Dar es salaam na Kilimanjaro kwenda Nairobi zilianza Januari 11, 2016. Mahitaji ya abiria kwa safari hizo ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kibiashara kati ya majiji ya Dar es Salaam na Nairobi ambayo kwa pamoja yana idadi ya watu ambao ni zaidi ya milioni nane yamekuwa makubwa na kuifanya fastjet hivi karibuni kuongeza safari zake kwenye njia hiyo ili kukidhi mahitaji makubwa ya abiria.

Fastjet kwa hivi sasa inafanya safari mbili za kwenda na kurudi kati ya miji hiyo kila siku ndani ya wiki na hivyo kufanya jumla ya safari zake kwa wiki kati ya Uwanja wa Kimataifa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuwa ni 28.

Mtiririko mpya wa safari unawapatia wateja huduma sahihi mapema nyakati za asubuhi na jioni na matokeo ya ratiba hiyo ni kuwepo kwa takribani viti 19,000 kila mwezi kwenye safari hizo kati ya majiji hayo mawili na hali kadhalika kuwapatia wateja mbadala sahihi wa kusafiri kwa nauli wanayoimudu.

Nauli za fastjet kimsingi ni za chini ikilinganishwa na tozo za mashirika mengine ambayo kwa sasa yanafanya safari zake kati ya Kenya na Tanzania. Nauli kutoka Tanzania kwenda Kenya zinaanzia shilingi 176,000 kwa safari moja, bila kodi ambayo ni shilingi 107,800 kwa kuondokea Tanzania na dola 40 kwa kuondokea Kenya, na hivyo fastjet kuwashauri abiria kukata tiketi zao mapema kabla ya siku ya kuanza safari ili kutumia fursa hiyo ili kufaidi na nauli ya chini.

Nauli kutoka Kenya zinaanzia dola za Marekani 120 kwa safari moja zikijumuishwa kodi za serikali ambayo ni dola 40 kwa kuondokea Kenya. Matokeo ya safari hizi kati ya Nairobi na Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa kutokana na ukweli unaojidhihirisha kwamba nauli kwenye mashirika shindani yanayofanya safari kati ya nchi hizi mbili zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 40 tangu fastjet ianzishe safari zake.

Fastjet inasisitiza kwamba kupunguza mtiririko wa safari kwenye njia kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya kuongeza uwezo zaidi kwa njia zilizopo kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na hali kadhalika kuwepo uwezekano wa kufungua njia nyingine mpya siku za karibuni.
 
For business reasons, it is very okay, is we tu wanataka kusitisha operation Kwa sababu ya kushindwa Ku meet operation cost........we still need them, Yes our economy need them too.
 
Moshi/Arusha - Nairobi ni karibu sana kujisumbua na usafiri wa ndege wakati kuna option ya haraka na cost-effective ya usafiri wa barabara. Arusha - Nairobi ni less than 4 hrs wakati kwa ndege pale airport peke yake unatakiwa 3 hours
reporting time international flight plus 1 hr in air. Pamoja na kwamba kwa barabara kuna delay fulani pale Namanga border lakini pia hata kwa ndege kuna kausumbufu fulani pale Nairobi airport.

Ukiangalia vigezo hivyo, Arusha - Nairobi usafari wa barabara ni more cost-effective and faster than air. Muda wenyewe wa kutoka Arusha hadi Kilimanjaro Airport au Nairobi City Centre hadi Jommo Kenyatta airport kwa barabara ni almost nitakuwa nimeshafika Namanga border. So, sababu ziko wazi kwanini hiyo route ni lazima idorore.
 
wewe ndio wa kwanza nakusikia usafiri wa ndege usumbufu utakua sawa na gari..biashara zimedorora kati ya izo nchi mbili kwa sasa watu hawasafiri kwa sasa hao fastjet bei yenyewe ya change iyo kwa mfanyabiashara inawasaidia sana..aisee msikate ya jozi bwana..
 
Sentensi ya kwanza kabisa katika aya kwanza, sio sahihi. Serikali ya Tanzania haina uhusiano wowote katika mipango ya biashara ya Fastjet. Serikali inafanya kazi ya kukusanya mapato yake kutoka Fastjet na taratibu nyingine za anga.

Kwahiyo si sahihi kisema Tanzania imesitisha safari zake kutoka Kilimanjaro kwenda Nairobi wakati Fastjet sio shirika la umma. Wao Fastjet wanaweza kuangalia kama hiyo safari ilikuwa inawalipa au la. Pia kuna uwezekano wa kuwa walikutana na vikwazo katika taratibu za usafiri wa anga. Naridia; Fastjet, Precisionair, Coastal Aviation, Flightlink Auric Air nk hawawezi kufanya lolote katika biashara zao na ikachukuliwa kama ni mashirika ya umma. Na Serikali ya Tanzania haiwezi kuwa MSEMAJI wa Mashirika haya katika biashara zao, ila inaweza KUYASEMA chochote kama yakikiuka taratibu fulani za kisheria na kiusalama
 
Sema sijajua kwa upande wa Kenya airways wao wanasafiri mara ngapi isiije ikawa mameneja wanapewa ushauri wa kukatishwa tamaa. Maana karibia wataliii wengi wanakuja kwa ajiri ya Tanzania. Kwa iyo kitendo icho kiangaliwe kwa jicho la tatu
 
Naipenda Fastjet, ila wana viusumbufu flani hivi vinakera sana. Mfano abiria waliorudishwa kutoka Dar - Kilimanjaro, wakarudishwa tena Dar eti kwasababu taa za uwanja wa Kilimanjaro ziligoma kuwaka. Iweje waanze safari bila kuhakiki destination?
 
Moshi/Arusha - Nairobi ni karibu sana kujisumbua na usafiri wa ndege wakati kuna option ya haraka na cost-effective ya usafiri wa barabara. Arusha - Nairobi ni less than 4 hrs wakati kwa ndege pale airport peke yake unatakiwa 3 hours
reporting time international flight plus 1 hr in air. Pamoja na kwamba kwa barabara kuna delay fulani pale Namanga border lakini pia hata kwa ndege kuna kausumbufu fulani pale Nairobi airport.

Ukiangalia vigezo hivyo, Arusha - Nairobi usafari wa barabara ni more cost-effective and faster than air. Muda wenyewe wa kutoka Arusha hadi Kilimanjaro Airport au Nairobi City Centre hadi Jommo Kenyatta airport kwa barabara ni almost nitakuwa nimeshafika Namanga border. So, sababu ziko wazi kwanini hiyo route ni lazima idorore.
Ni kweli mkuu si rahisi kupata abiria wengi kwani vinoah na coaster za tours ni usafiri rahisi na wa haraka kuliko sijui utoke Arusha halafu uende Bomang'ombe usubiri saa kama 3 hivi,halafu ulipe malaki wakati huo mwenzako yupo Kajiado wewe bado upo unakaguliwa ,kuja kumaliza na kuanza kupaa tayari jamaa yupo Nairobi kwa TZS 30,000.
 
Ni kweli mkuu si rahisi kupata abiria wengi kwani vinoah na coaster za tours ni usafiri rahisi na wa haraka kuliko sijui utoke Arusha halafu uende Bomang'ombe usubiri saa kama 3 hivi,halafu ulipe malaki wakati huo mwenzako yupo Kajiado wewe bado upo unakaguliwa ,kuja kumaliza na kuanza kupaa tayari jamaa yupo Nairobi kwa TZS 30,000.

Mkuu wewe umenielewa nachomaanisha. Kuna mdau hapo juu kashangaa eti "usafiri wa ndege usumbufu utakua sawa na gari"; kwa route fupi ya Arusha - Nairobi, gari ni more convenient than air hasa kutokana na logistics na usumbufu mwingi wa ndege tangu kukata tiketi mara uanze kuvizia msimu nafuu na ujinga mwingine kama huo. Ila kwa long distance obviously dege iko poa.
 
dudus ndege ni ndege mkuu iwe safar fupi au ndogo hakuna tochi kule wala kamanda mpinga wala husikii viroba kwa marubani au walichomekeana..
 
dudus ndege ni ndege mkuu iwe safar fupi au ndogo hakuna tochi kule wala kamanda mpinga wala husikii viroba kwa marubani au walichomekeana..

Nakubaliana na wewe Mkuu; ndege ni ndege lakini pale penye options abiria pia hupima; kigezo muhimu zaidi kikiwa gharama. Hivi kwa mfano, kama difference ya muda kati ya ndege na barabara haizidi 2 hours (nachukulia tangu mtu anapotoka nyumbani kwenda stendi/airport hadi anapofika destination) yet kwa barabara nauli ni 60,000/= while kwa ndege ni more than 400,000/= (zote return) unadhani walio wengi wata-opt ipi? Jibu liko wazi Mkuu usilete ubishi usio na maana.
 
dudus kilichopo ni kuanguka kwa biashara kwa Arusha na Nairobi kama biashara ipo ok iyo 400000 haina shida inalipwa tuu..biashara kwa wakati huo ndio inakufanya usafiri na usafiri gani mkuu ila mimi wewe sikushangai hata watanzania wengi wanaenda south Africa kwa bus harafu wakisechiwa beitbridge boarder wakikutwa na dola zilizozidi kiwango wanatoa rushwa wakati oliver tambo hakuna huo upuuzi..hakuna alichookoa zaidi ya kupoteza mudana na hela.
 
Back
Top Bottom