Kampuni ya epa inapopata tuzo uk!!si mchezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampuni ya epa inapopata tuzo uk!!si mchezo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, May 12, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  NA PDIDY

  KAMA MNAKUMBUKUMBU YA ZILE KAMPUNI ZILIZOZALISHWA BAADA YA WIZI WA EPA HII KAMPUNI IPO KWENYE LIST NAONA BAADA YA KUONA VIPI IMEONGEZA JUHUDI WATANZANIA WAIPENDE NA KUSAHAU ILIPOTOKEA SASA WAINGEREZA WAMEAMUA KUTUNUKU VYATI KWA UBORA WAO BADO SIE TUWATUNUKU NINI??

  KAMPUNI ya ACM LTD ya Uingereza, imeitunuku Tuzo ya Kimataifa ya Ubora wa Bidhaa Kampuni ya Azania inayozalisha Unga wa ngano na Mahindi nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ACM LTD, Andrew Rowe alisema juzi Dar es Salaam kuwa kampuni hiyo ilikuwa inastahili tuzo hiyo kutokana na huduma zake bora kwa wateja. Alisema Kampuni ya Azania imepata tuzo hiyo baada ya kushindanisha kampuni kadhaa na kuonekana kuwa ni bora kuliko zingine.

  “Hii kampuni ilistahili tuzo kutokana na huduma, lakini sio kama zingine hazifanyi vizuri, bali hizi ni kama changamoto tu kwa kampuni yetu hapa nchini iendelee kutoa huduma bora kwa wateja”alisema.

  Alisema kuwa wateja wanachokiangalia ni huduma bora,bei za bidhaa,uimara na usafi wa wafanyakazi, hapo ndipo ilipo changamoto kwa wafanyabiashara hususan wanaotoa huduma za vyakula. Alisema Watanzania wengi wanakuwa na mawazo kuwa bidhaa zao hazina ubora, lakini ukweli ni kwamba kuna kampuni nyingi zinazotoa bidhaa tena nzuri.

  “Hakuna sababu za kutafuta bidhaa za nje kwani hapa hapa nchini kuna bidhaa nyingi zenye ubora wa kutosha, nawashauri Watanzania wasikimbilie nje ya nchi kutafuta bidhaa bali waimarishe uchumi wao kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hapahapa, “alisema Rowe. Naye Ofisa Masoko wa Kampuni ya Azania, Mohamedi Bashrahili alisema kuwa walifarajika kupata tuzo hiyo na imekuwa ni kama changamoto kwa kampuni yao.

  Alisema mwanzoni wateja walikuwa hawawakubali, lakini siku zinavyozidi kwenda ndivyo wanapopata wateja wengi zaidi kutokana na huduma zao kuwa bora. mwisho
   
Loading...