Kampuni ya El Hillal Minerals inatumikisha wafanyakazi bila kuwalipa mishara.

NUMET

New Member
Nov 19, 2015
2
2
Kwa miezi miwili mfululizo, kampuni ya kuchimba alamasi ya El Hillal Minerals iliyoko Mkoani Shinyanga, haijawalipa wafanyakazi wake mshahara.

Juhudi zote za kistaarabu hazijazaa matunda. Ukiongea na management wanasema wazi kuwa hawana pesa ya kulipa kwasababu serikali imewazuia kuuza almasi, kwa maana nyingine ni kwamba mwajiri ameamua kuwaadhibu wafanyakazi kwasababu serikali imetunga sheria mpya za madini.

Juzi kamati maalum ya Bunge inayoshughulikia masuala ya nishati na madini, ilifika mgodini hapo, wafanyakazi waliieleza kamati kuwa hawajalipwa mshahara kwa zaidi ya siku 50, lakini hawakupata msaada.

Wafanyakazi wanafanyishwa kazi usiku na mchana bila mapumziko wala chakula, na hata maji ya kunywa hawapewi achilia mbali mshahara wao ambao ni jasho lao.

Hakika inatia uchungu kuona wafanyakazi wanaacha familia zao , wanakwenda kufanya kazi lakini mwajiri wao hajali hata kidogo.

Swali la kujiuliza, kama kweli hana pesa za kulipa mshahara, je pesa za kuendesha mitambo anazipata wapi?

Je, ni kwanini mwajiri awaadhibu wafanyakazi kwa masuala ya serikali?

Kwanini serikali iwaache watu wake wakinyanyaswa na mwajiri?

Tunaomba serikali iingilie kati mgogoro huu, maana wafanyakazi wamechoka, wanaweza kuchukua hatua ambayo italifedhehesha taifa na kumtia hasara mwajiri au wao wenyewe.

Naamini serikali italishughulikia maana hata Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga anazo taarifa hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom