Kampuni ya Business Times sasa yachungulia kaburi!!!

Kampuni ya Business Times sasa yachungulia kaburi!!!

Mshaka

Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
10
Reaction score
0
Kwa masitikiko makubwa nimeambiwa kwamba hali ya Kampuni ya Business Times, inayomiliki magazeti ya Business Times, Majira na Spoti sasa imekuwa tete. Wafanyakazi wake hawajalipwa kwa miaka miwili sasa huku waandishi wa mikoani nao wakiwa hawajalipwa kwa muda wa miaka minne sasa. Talents nyingi sasa zimeondoka kutokana na Mmiliki wake Bw Mbuguni na waanaye wawili Aga na Imma kushika hatamu huku wakiwa na uwezo mdogo wa kuendesha kampuni. Wafanyakazi walijitahidi kudai haki zao kupitia chama cha wafanyakazi lakini wakafukuzwa kazi na chama kikauwawa. Na habari za ndani zinasema kwamba mtu yoyote akidai maslahi yake anaonekana adui na wengi wamefukuzwa kwa ajili ya kudai. Talent zote sasa zimeisha na wamebakia na correspondents wengi na wanafunzi toka vyuoni ambao wanaishi kwa mishiko. TRA nao wanadai fedha nyingi za VAT ambazo zinakusanywa lakini wakija maafisa wa mamlaka ya mapato wanahongwa fedha na kuondoka. Michango ya wafanyakazi NSSF nayo haijalipwa miaka mitano kwani nao wakija kudai wanahongwa pesa wanaondoka. Kama mnakumbuka hi indo kampuni ya kwanza ya wazalendo ya vyombo vya habari ambayo ilisaidia kuchakata vuguvugu la vyama vingi na ile ushiriki wa sekta binafsi katika uchumi.
 
Back
Top Bottom