Kampuni kubwa ya ndege duniani Boeing inapanga kuwafuta kazi watu 4,500

stan

Senior Member
Apr 23, 2010
149
180
Kampuni kubwa ya ndege duniani Boeing inapanga kuwafuta kazi watu 4,500 kufikia katikati mwa mwaka huu katika hatua ya kubana matumizi.

Msemaji wa kampuni hiyo ameeleza kuwa kutakuwa na nafasi 1600 kwa watu wanaotaka kujiuzulu kwa hiari kufanya hivyo huku wengine wakifutwa tu.

Hatua hii inatarajiwa kuchukuliwa katika kitengo cha ndege za kibiashara wakati wateja wamepungua.

Mamia ya wakurugenzi pia wanatarajiwa kupoteza ajira.

Idadi hiyo ya watakaofutwa kazi ni asilimia 3 ya nguvu kazi ya Boeing ambayo kwa jumla ina wafanyakazi 161,000 kufikia mwisho wa mwaka jana.

160124121207_boeing_512x288_getty_nocredit.jpg
Image copyrightGetty
Image captionKumekuwa na upungufu wa kuagizwa ndege hizo
Boeing inachukua hatua hiyo kutokana na wasiwasi kwamba kumekuwa na upungufu wa kuagizwa ndege hizo.

Kampuni hiyo ya Marekani pia imekuwa ikapoteza soko kutokana na ushindani wa kampuni ya Airbus Group SE.

Boeing imetengeneza ndege 762 mwaka jana na kupita kima kilichokadiriwa awali.

Hatahivyo kumeshuhudia upungufu mkubwa mwaka jana wa wateja.

Kampuni za usafiri wa ndege zimesusia kutumia mabilioni ya dola kuagiza ndege ambazo hazitopatikana kwa miaka kadhaa.
Source BBC SWAHILI.
 
Kuna sehemu sijaelewa kwamba wateja wana wasiwasi ndege kutopatikana kwa miaka kadhaa?Ni dreamliner ndo inahusika au ndege zote za boeing?Kwa hiyo wanasitisha uzalishaji au?:rolleyes::rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Back
Top Bottom