Kampuni imesajiliwa inauzwa




Ok swala la muda nimelielewa.

Swali je toka 2012 tra wakasema hiyoo kampuni ilikuwa inafanya kazi bila kulipo kodi. Alienunua atajiteteaje??
 
Ok swala la muda nimelielewa.

Swali je toka 2012 tra wakasema hiyoo kampuni ilikuwa inafanya kazi bila kulipo kodi. Alienunua atajiteteaje??
Asante kwa swali lko zuri
Katika jambo hili kampuni hununuliwa baada y kukabidhiwa na kuhakikishiwa kuwa kil kitu kipo sawa. Hauwezi kununua kampuni km bidhaa bali lazima kujiridhisha sehemu husika za BRELA na TRA
Na mwisho inapotokea suala la kudaiwa ina maana wamiliki wa kampuni watawajibika kwa gharama husika. Ndiyo maana utaona katika tangazo gharama za BRELA zimewekwa wazi na vlvl zimejumlishwa ktik bei ya mauzo
 
Mkuu nazani usemi wa muda....kwa upande wangu lazima iwe pia imewahi ku-oparate kwa maana hiyo ita act kama ndio reference yako kwa clients...kwamba iliwahi kufanya kazi so and so
 
Mkuu nazani usemi wa muda....kwa upande wangu lazima iwe pia imewahi ku-oparate kwa maana hiyo ita act kama ndio reference yako kwa clients...kwamba iliwahi kufanya kazi so and so
Hili ondoa shaka. Kuna watu wangapi wanaoperate shughuli zao kienyeji. Hivyo wakihitaji jina linabeba kazi yake.
 
Kuna kitu hukiweki wazi, sijajua kama hujui taratibu za TRA returns au unafanya kusudi. Maana kama kampuni haijafanya kazi (dormant) na hujawahi kuandika official letter kwenda TRA kwamba hujaanza kufanya kazi, lazima kodi utalipa yote tangu isajiliwe. Kutofanya kazi ni suala lingine na kutoa taarifa TRA kwamba hujaanza kufanya kazi ni suala jingine, na pindi ukitoa taarifa ndio kodi haihesabiwi kuanzia hapo, lakini ya nyuma yote lazima ulipe pamoja na MNICIPAL LEVY 3% (kwa municipal ulipoandoka address ). NO option. So many people do open company without knowledge of company laws, especially TRA Returns na Municipal Levy.
 
Nawe Mkuu nadhani kuna kitu hujakisoma na kukielewa vema. Soma ukurasa vema na kwa utaratibu utaona imeandikwa kuwa hii ni ONLY REGISTERED BRELA DOCUMENT. Hayo yooote nayafahamu vema sana
 
Sorry Nina kampuni yangu ndo nataka nicheki brela nadaiwa bei gani, ni ya tangu 2013. Iko dormant pia, ila nataka nianze kazi, mtaji tu unazingua. TIN ipo ila nilifile nikiwa mbeya mjini Kwa estimation 0! Sijajua watanibabua shilingi ngapi! Lengo nikiona siwezi kuendeleza niiuze pia! Nimekuwa nikisita kuiuza kwa sababu walizosema akina Afrorink...
 
Mkuu ondoa khofu na hilo
We jaza fomu za BRELA za Annual returns kuanzia unataja tarehe uliyofungulia kampuni lkn kwa mwaka unaofuata. Mfano 08.03.2014; 08.03.2015........ 2018. Kisha nenda ofisi zao BRELA. Kwa makadirio ya haraka haraka naona utakuwa katika 450+k
TRA hapo kama una maelezo mazuri unaweza kulipa lakini naamini kwa kiwango sio cha kuogofya. Sana sana kuna cases za wengi wanatakiwa kupeleka na zile Income annual returns forms ikiwa na audited financial statements na vielelezo vya kutosha kuonyesha haikufanya biashara kabisa
Karibu sana
 
Thanks.....kwakuwa TIN nilipatia Mbeya, na nikakadiriwa 0 japo sikuwahi kurudi tena ofisini kwao wala sikufanya kazi, sasa nikarudi kuishi Dar, na ndo sasa nataka niresume shughuli za kampuni hii badala ya kufungua nyingine, so nahisi kuna faida kuendelea na hii yenye umri angalau miaka kadhaa...JE niende na TIN hii kwenye TRA office katika eneo langu?
 
Kama unaikumbuka vema na TIN NO yako nakushauri nenda tawi lolote. Lakini je wakati wa kuzi-update kutoka zile TIN No za zamani kuja katika mfumo huu mpya hukuweza ku-update?
Vilevile nakushauri waweza kwenda kama kuulizia tu, maana hapo ishu ni kuhamisha files kutoka Mbeya kuja Dar sometimes huwa wanazingua.
Mwisho nakushauri kama kama mzunguko mrefu omba kufungua upya ambapo nadhani taratibu sio ngeni kwako kwa utaratibu sahihi wa kupata TIN NO ya kampuni
 
THANKS, ila TIN certificate ipo, ninayo kabisa ya tangu 2013. Sikwenda kuhakiki kipindi kile, coz nilikuwa shule sehemu mbali na mjini. Kwaivo nina certificate of Incorporation na TIN certificate ya kampuni hii. Naishi Kimara, nilipenda kama naanzisha ofisi nianzishie maeneo ya ubungo, mwenge au sinza.
 
Nenda na hiyo Tin no yako na hizo docs za kampuni kama MEMORANDUM, CERTIFICATE OF INCOP kwanza kama docs za awali. Then watakupa mwongozo wa vielelezo vya ziada ambavyo normally huwa mkataba wa eneo la ofisi, barua 3 ie Board resol letter, tax consult appointment letter, na updating file letter kwa mahala walio strict
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…