Kampuni CCECC ya China ipo tayari kujenga reli ya kati

Kampuni CCECC ya China ipo tayari kujenga reli ya kati

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578

​

KAMPUNI ya ujenzi na uhandisi wa majengo ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) imesema iko tayari kuja Tanzania na kujenga upya reli ya kati ili iwe ya kisasa zaidi endapo wataombwa wafanye hivyo.

Hayo yamesemwa jana jioni (Ijumaa, Oktoba 18, 2013) na Rais wa CCECC, Bw. Yuan Li alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jijini Beijing, China. Waziri Mkuu jana alikuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo.

Akizungumza na Bw. Li pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Tanzania alioambatana nao, Waziri Mkuu alimweleza Bw. Li kwamba hivi sasa reli hiyo imechakaa hali inayofanya mizigo mingi kutoka bandarini isafirishwe kwa barabara na hivyo kuongeza gharama kwa wasafirishaji.

Alisema hali hiyo inachangia mzigo kwa Serikali kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa barabara kutokana na uzito wa magari yanayobeba mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi nchi jirani kwa sababu wanaitegemea sana bandari hiyo kwa kupokelea mizigo.

Alipoulizwa ni uzito kiasi gani unaruhusiwa kwenye barabara za nchini China, Bw. Li alijibu ni tani 25 (axle load) hali iliyomshtua Waziri Mkuu ambaye alilazimiak kumweleza mgeni wake kwamba barabara za Tanzania haziwezi kudumu kwa miaka mingi kwani hivi sasa zinaruhusu magari yenye uzito wa tani 56 kupita kwenye barabara zake.

Alisema kutokuwepo kwa usafiri madhubuti wa reli imekuwa ni kikwazo kikubwa cha usafiri kati ya Dar es Salaam na Kigoma na Tabora hadi Mwanza lakni pia kutoka Tabora hadi Mpanda. "Kukamilika kwa reli hii ambayo ni uti wa mgongo wa Taifa letu, kutasaidia hapo baadaye kufungua milango na Burundi, Rwanda na DRC lakini pia tutaweza kupeleka mizigo hadi Uganda kwa kupitia Mwanza," alifafanua.

Kwa upande wake, Bw. Li alimweleza Waziri Mkuu kuwa tayari wameanza mazungumzo na Wizara ya Uchukuzi na iwapo watafikia muafaka wako tayari kuja kuijenga reli hiyo.

Akitoa mfano wa zoezi kama hilo, Bw. Li alisema kutokana na mkopo wa benki ya Exim ya China, Septemba mwaka huu, wameanza ujenzi wa reli kati ya Djibouti na Sudan Kusini pamoja na reli nyingine ya kuunganisha Djibouti na Ethiopia ambapo zote mbili zinatarajiwa kukamilika baada ya miaka miwili.

"Hatuwezi kufumua reli yote kwa mara moja. Ninachoona hapa, ujenzi wake itabidi uende kwa awamu kwa sababu una gharama kubwa lakini kwa kuanzia tunaweza kuanza Dar es Salaam hadi Morogoro, awamu ya pili tukatoka Morogoro hadi Dodoma na kuendelea ili usafiri wa treni uwe ukiendelea wakati ujenzi wa reli nao ukiendelea," alishauri.

Kampuni ya CCECC ndiyo iliyojenga reli ya Tanzania hadi Zambia (TAZARA) yenye urefu wa kilometa 1,860 na madaraja 320. Ujenzi wake ulianza mwaka 1970 na kukamilika mwaka 1976.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, (OWM) Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Zanzibar, Bw. Abdallah Jihad Hassan; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bibi Saada Salum Mkuya.

Pia amefuatana na Balozi wa China, Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahaman Shimbo, Wakuu wa mikoa ya Mtwara, Shinyanga na Simiyu; wabunge wawili, Bw. Godfrey Zambi (Mbozi) na Dk. Titus Kamani (Busega) na viongozi wakuu wa Tanzania Private Sector Foundation, Bw. Reginald Mengi, Bw. Salum Shamte na Bw. Godfery Simbeye.
 
Ulaji mtupu wa taxpayers money:

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, (OWM) Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Zanzibar, Bw. Abdallah Jihad Hassan; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bibi Saada Salum Mkuya.
Pia amefuatana na Balozi wa China, Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahaman Shimbo, Wakuu wa mikoa ya Mtwara, Shinyanga na Simiyu; wabunge wawili, Bw. Godfrey Zambi (Mbozi) na Dk. Titus Kamani (Busega) na viongozi wakuu wa Tanzania Private Sector Foundation, Bw. Reginald Mengi, Bw. Salum Shamte na Bw. Godfery Simbeye.​
 
Kama lengo ni kujifunza wamepatia.
Sijajua kama ziara hiyo imehusisha waandishi wa habari wenye malengo ya kujifunza na kutufunza sisi tulio na kiu na sio WATALII.
 
Business as usual,Talk the talk is what CCM useless leaders do best.
 
Hapo! shughuli ipo! cjui nisuse kulipa kodi!!! maana hapo ufujaji wa kodi jumlisha 10% tarajali kwani huo mradi wa kujenga reli tenda yake ishatangazwa kwa mujibu wa sheria?
 
Ulaji mtupu wa taxpayers money:

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, (OWM) Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Zanzibar, Bw. Abdallah Jihad Hassan; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bibi Saada Salum Mkuya.
Pia amefuatana na Balozi wa China, Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahaman Shimbo, Wakuu wa mikoa ya Mtwara, Shinyanga na Simiyu; wabunge wawili, Bw. Godfrey Zambi (Mbozi) na Dk. Titus Kamani (Busega) na viongozi wakuu wa Tanzania Private Sector Foundation, Bw. Reginald Mengi, Bw. Salum Shamte na Bw. Godfery Simbeye.​
Wakirudi huko, utaona kila moja amevaa kofia yenye nyota nyekundu kama ya Kada flani!
 
Kama lengo ni kujifunza wamepatia.
Sijajua kama ziara hiyo imehusisha waandishi wa habari wenye malengo ya kujifunza na kutufunza sisi tulio na kiu na sio WATALII.

Kujifunza nini? Wewe hapo umegundua lipi Jipya amabalo ulikuwa ulijuhi? Au ni wale wale wavivu wa kusoma na Kufuatilia?
 
Djbout na Ethiopia wanajenga 750+KM za Train ya umeme na ndani yake 100KM ni Double Track kwa 600 USD Mil. Ambayo ni sawa na 1Tril sisi tunashindwa nini? Mbona Tuli Bail OUT makampuni ya pamba kwa 1Tril. Na tumekopa huko sijuhi 26Tril. Hizo hela zimeenda wapi na zimefanyia nini jamani?

Hivi kama Tungekopa kujenga barabara na Mahospitali, Mashule nA Rail kiukweliukweli 24 Tril leo Hii nChi ingekuwaje?
 
Tanzania tuna bahati mbaya sana ya kuwa na Viongozi wenye upeo mdogo sana sana mpaka wanasikitisha!Fikiria namna walivyoliua Shirika la Reli Tanzania kwasababu za kijinga kijinga tu eti ili wapuuzi flani hivi biashara zao za Malori ziende vizuri..Hii akili fupi sijawahi kuona ikionyshwa na Viongozi wowote Duniani.Hawa Vilaza wanafanya maamuzi mabovu kwa kuangalia faida zao za leo lakini wanashindwa kuelewa namna wanavyoidhohofisha Nchi hii na kuifanya ishindwe kushindana na Nchi nyingine Kimaendeleo na zaidi wameikandamiza hii Nchi ishindwe kuibuka Kiuchumi.
 
Mikataba 21 iliyokwusha sainiwa reli ya kati haikuwemo? Waombwe basi haraka tunahiitaji hiyo njia. sisi tulioko mikoa ya penzeni tumeisha nyonywa vya kutosha toka wakubwa wawekeze ktkt magari makubwa ya mizigo- hawataki kusikia reli ya kati.
 
hawa mawaziri wote wameenda kufanya nini, hapa palitakiwa Waziri Mkuu na Waziri wa Uchukuzi na waziri wa Ujenzi basi, wengine wameenda kufanya shopping tu hakuna lolote
 
Hii pesa walikopeshwa ama walipewa bure?

Na serikali inafuatilia kuakikisha hayo makampuni wanatumia hiyo pesa kama ilivyokusudiwa na sio kwenda kujenga nyumba Mbezi beach!

Bure na CAG alifanya uhakika kuna Bil kibao hazijulikani amepewa nani.
 
Japan juzi juzi walisema wanataka kutujengea reli ya kati,kupanua bandari ya dar es salaam,kujenga viwanda vya pikipiki na vifaa vya umeme leo wachina wanasema wanataka kutujengea reli ya kati baada ya kuchukua mkopo exim tunatakiwa tuelezwe nini kinaendelea maana kama Japan wakiipanua bandari ya dar ina maana bandari ya bagamoyo inakufa kifo cha mende na pia Tanzania imekuwa soko kubwa la vifaa vya umeme na pikipiki toka china kitendo cha japan kingezalisha ajira maradufu na kuongeza mapato kupitia kodi kuna bandari ya tanga na Mtwara pia kuna reli ya Tanga inatakiwa kujengwa wachina waache usanii na benk yao ya exim
 
Alikwenda Namibia na akaona reli ya Namibia na kuahidi kujenga reli kama ya Namibia. Akaenda Ujerumani na kuahidi kwamba, wajerumani watakuja kujenga reli ya Kati kama kumbukumbu yao. Ni zaidi ya miaka 6 sasa hatujaona hata taruma jipya lililokuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo.

Wachina hao hao tukaambiwa wanakuja kujenga JNIA na kuwekeza ndege mpya. Porojo zikawa zile zile.

Hivi mi-CCM imesahau kwamba kipindi cha uchaguzi kilisha isha na sasa si muda wa ahadi tena?

Tumeshachoka na ahadi zao kila siku. Watuachie nchi yetu ili tuya tafute maendeleo kwa kasi ya ajabu.
 
Bila reli imara maisha bora kwa kila mtanzania ni ndoto!!!
Reli ya kati kujengwa pia ni ndoto maana reli ikijengwa tu yale maroli yanaenda kupaki ikulu
 
Hapa waandishi wakiwa nje wanatuma taarifa nusu nusu na wakisafiri na viongozi sijui wanadaka maneno mangapi au lugha za viongozi wao hazieleweke.

Kwa sie wapita njia tunaona wachina wametoka Nyaua na wanakaribia Itigi wanatoa reli za zamani na wanaweka mpya ya kisasa. sasa ukisema wachina wanakuja kujenga wakati wako site na wanakaribia kumaliza sijui hiyo wanayoweka sasa watabomoa.
 
Ulaji mtupu wa taxpayers money:

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Nchi, (OWM) Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Waziri wa Uvuvi na Mifugo wa Zanzibar, Bw. Abdallah Jihad Hassan; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bibi Saada Salum Mkuya.
Pia amefuatana na Balozi wa China, Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahaman Shimbo, Wakuu wa mikoa ya Mtwara, Shinyanga na Simiyu; wabunge wawili, Bw. Godfrey Zambi (Mbozi) na Dk. Titus Kamani (Busega) na viongozi wakuu wa Tanzania Private Sector Foundation, Bw. Reginald Mengi, Bw. Salum Shamte na Bw. Godfery Simbeye.​

Wangekuwa wasikivu safari nyingine wangepunguza huo mlolongo wa warasimu manake hakuna wanachojifunza ambacho wataweza kukiweka katika vitendo. wameshaenda sana na hakuna jipya la ajabu waongeze washiriki wa sekta binafsi na wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom