Kampeni za uchochezi ni hatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za uchochezi ni hatari

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MziziMkavu, Mar 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  KWA siku kadhaa zilizopita, Watanzania wamepokea taarifa za kushangaza za kuwepo kwa habari za kupikwa zinazolenga kuleta uchonganishi na uvunjifu wa amani miongoni mwa viongozi wa vyama vya upinzani.

  Mwishoni mwa wiki jana, kulitolewa kile kilichodaiwa kuitwa ni waraka ulioandikwa na naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, aliyedaiwa kupingana na uongozi wa chama hicho katika kuendesha kampeni za uchaguzi.

  Waraka huo ulidai kuwa Zitto hakubaliani na matusi yanayotolewa na makada wenzake, na kwamba aliunga mkono juu ya suala la Vicent Nyerere kutokuwa mtoto wa nduguye na Mwalimu Julius Nyerere.
  Hata kabla vumbi hilo halijaisha, umetolewa tena mwanzoni mwa wiki hii, kitu kama kilekile lakini safari hii kikimlenga Katibu Mkuu wa chama

  hicho, Dk. Willibrod Slaa. Zamu hii, mtendaji huyo anashutumiwa na watu waliojiita ‘maafisa’ wa juu ya chama hicho.
  Kama ilivyokuwa kwa Zitto, Slaa kupitia kurugenzi ya uenezi, alibaini na kisha kukanusha nyaraka zote hizo na kubainika kuwa ziliandikwa na

  watu wenye malengo machafu ya kuleta vurugu na uchochezi kwa chama hicho.
  Tunachukua nafasi hii kulaani kwa nguvu zote njama za aina hii ambazo kwa namna yoyote ile ni za kitoto na zinazofanywa na watu wenye fikra finyu. Tunaamini kuwa kama taifa la watu wakomavu, upuuzi wa aina hii hauvumiliki hata kidogo.

  Watanzania wanataka kuona ushindani wa kisomi, kistaarabu na wenye lengo la kuibua changamoto za kistaarabu zitakazoleta maendeleo kwa Watanzania. Lakini baadhi ya wanaodhani wanastahili kuitwa viongozi na wanaofikiri kuwa wana hatimiliki ya kuongoza, wameibua mambo ya hovyo na yanayoshangaza kwa watu wenye busara.

  Kampeni za kupakana matope, zimekuwa za kawaida kwa chama fulani cha siasa ambacho tumeshuhudia kila unapofika wakati wa uchaguzi hata wa ndani ya chama hicho, watu wakifikia hatua ya kutishana kuuana na hata kutangaziana uhalali na uharamu wa uraia.

  Watanzania hawajasahu jinsi ambavyo chama hicho kilivyoweza kuwatuhumu hata makada na viongozi wake wa siku nyingi na ambao waliwahi kushika nafasi za juu serikalini kuwa ni wauaji na hivyo hawastahili kushika madaraka.

  Tunapenda kuwaomba Watanzania na watu wote wapenda maendeleo kuwa sasa umefika wakati wa kuchukua hatua ya kuwazomea na hata kuwakataa kwa kila njia viongozi wa siasa wanaolenga kuchafua amani ya nchi kwa manufaa ya matumbo yao.

  Aidha tunawataka viongozi hao uchwara kutambua kuwa sasa tumechoka kuvumilia ujinga wao na kuanzia sasa tutawaweka hadharani kwa majina na vyeo vyao wale wote wanaoendekeza mchezo huu wa kuchafua wenzao kwa nyaraka feki bila kujali hadhi na vyeo vyao katika jamii.
  Kampeni za uchochezi ni hatari

   
Loading...