Uchaguzi 2020 Kampeni za Uchaguzi Vs Sheria za Upigaji Kura

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Habarini wadau.

Kuna kitu kimekuwa kikinichanganya kidogo kuhusu kampeni za uchaguzi pamoja na sheria za upigaji kura. Ningeomba wadau wa siasa na pamoja na tume ya taifa ya uchaguzi kutupatia majibu na ufafanuzi wa hili.

Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi katika upigaji kura anae ruhusiwa kupiga kura ni raia yeyote yule wa tanzania ambaye amefika umri wa miaka 18 na ni lazima awe na akili timamu. Hii ni sheria katika kipengele cha umri.

Lakini kinachonishangaza ni kwanini ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 wanaruhusiwa na mara zingine wanalazimishwa kwenda kwenye kampeni? Nitatolea mfano, nimekuwa nikishuhudia shule za msingi zikisitisha masomo/vipindi vya siku husika na kuwataka wanafunzi hao kwenda kushiriki kusikiliza kampeni za mgombea labda X.

3/4 ya washiriki wa hizi kampeni huwa ni watoto ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 wengi ndio hujaza uwanja na kushika vipeperushi.

Hoja yangu ni kwanini tunaruhusu wale ambao hawajafikisha umri wa miaka 18 na kisheria hawana maamuzi ya kupiga kura kushiriki kampeni? Huku si kuwapotezea muda na kuharibu utaratibu wao either wa kazi au masomo? Je, NEC haioni umuhimu wa kuzuia hili ikawa wanaoruhusiwa kushiriki kusikiliza kampeni ni wale waliofikisha umri wa miaka 18?

Nawasilisha
 
Uvunjifu mkubwa wa sheria unafanywa na ccm na hatua hazichukuliwi mfano sasa jiwe anafanya ukabila wa nguvu kila mahali na hakuna lolote analoambiwa. Tuwe makini na mtu huyu ni hatari kwa ustawi wa taifa letu.
 
Back
Top Bottom