PreGE2025 Kampeni za Rais Samia zilivyoshika kasi

PreGE2025 Kampeni za Rais Samia zilivyoshika kasi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,853
Reaction score
3,098
Iwe ni kujipendekeza au ni mkakati wa makusudi, sasa kuna kampeni zilizoshika kasi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye kimsingi ndiye mgombea urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kampeni hizo ni pamoja na Samia Scholarship, Samia Leagal Aid, Goli la Mama, Knock Out ya Mama, Msitu wa Mama na nyingiezo zinazoendelea kuibuka.

Kampeni hizo zinaibuka wakati ambao pia kuna makundi ya makada ya wana CCM wanaojiita chawa wakipiga kampeni kwa Rais Samia, licha ya kutotambuliwa katika mfumo wa utawala wa jumuiya za chama hicho.

Kwa kuanza na kampeni ya Msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid imeshika kasi ikitumika kuwafikia wananchi wenye changamoto za kisheria.

Kwa mujibu wa Wizara ya Katiba na Katiba na Sheria, kampeni hiyo ya miaka mitatu iliyoanza Machi 2023 itaendelea hadi Februari, 2026 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Iilizinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Mei 27, 2023 Jijini Dodoma na kuanza kufanya kazi jijini humo Mei 28, 2023.

Kampeni imejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi hususan katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala, na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla. Utekelezaji wa kampeni unafanyika kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia, Wanazuoni na Wadau wa Maendeleo.

Lengo kuu la Kampeni ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini.

“Katika kufikia lengo hilo, kampeni inaongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususan haki za wanawake na watoto; Inatoa huduma ya ushauri wa kisheria na unasihi kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kijinsia; kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu elimu ya sheria, masuala ya haki na wajibu na misingi ya utawala bora,” imesema sehemu ya taarifa ya Wizara.

Matokeo ya muda mrefu wa kampeni hiyo yametajwa kuwa ni kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza, hususan wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira hatarishi wakati matokeo ya kati ni kuimarika kwa mfumo wa utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika ngazi za Serikali Kuu hadi Serikali za Mitaa.

“Matokeo ya muda mfupi ni kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto; kupungua kwa idadi ya migogoro na matukio yanayotokana na ukosefu wa uelewa wa sheria; Kuimarika kwa uwajibikaji na uwezo wa taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali zinazotoa huduma za msaada wa kisheria.”

Miongoni mwa taasisi zizilizohusiwa kwenye utekelezaji wa kampeni hiyo ni Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Hata hivyo, baadhi ya wadau walimnyooshea kidole Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi kwa kushiriki kampeni hiyo kutokana na misimamo mikali dhidi ya Serikali.

Lakini akizungumza Februari 3, 2025, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, Dodoma, mgeni rasmi akiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mwabukusi alisema wanatumia kampeni hiyo kupigania haki.

“Tunapata changamoto watu wanapoona tukishirikiana na Serikali, wanafikiri tunalamba asali. TLS si kikundi cha magaidi, kwa hiyo sehemu ya kuonya tutaonya kwa haki, ya kupongeza tutapongeza kwa haki, ya kushiriki kufanya kazi tutashiriki pamoja, kulijenga Taifa letu na kumhudumia Mtanzania,” amesema Mwabukusi.

Samia scholarship

Kampeni nyingine ni mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu wa Samia unaosimamiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Ufadhili huo ulilenga kuwanufaisha takriban wanafunzi 700 wa elimu ya juu nchini Tanzania wanatarajiwa kunufaika kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Kwa mujibu wa Wizar aya Elimu, Sayansi na Teknolojia, sifa za mwombaji sharti awe Mtanzania,
awe amefanya mtihani wa kidato cha sita (ACSEE) unaosimamiwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika mchepuo wa sayansi (PCB, PCM, CBG, PGM, CBA, PMC, na CBN) kwa mwaka husika wa masomo.

Masharti mengine ni pamoja na kupata udahili katika Taasisi ya Elimu ya Juu inayotambulika ili kusomea programu za kipaumbele (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Afya) kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) nalo halikubaki nyuma, kwani sasa linatekeleza mrasi wa Nyumba wa Samia Samia Housing Scheme utakaojenga nyumba 5,000 ukitekelezwa kwa awamu, kwa gharama ya Sh466 bilioni.

Maeneo unakotekelezwa mradi huo ni pamoja na Kawe (nyumba 560), nyumba 400 eneo la Mtoni kijichi Dar es Salaam na nyumba 100 Jijini Dodoma.

Serikali pia inatekeleza kampeni ya utunzaji wa mazingira kupitia upandaji miti iitwayo Msitu wa Mama.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Machi 11, 2025 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis.

Kampeni hii iko chini ya usimamizi wa hama cha Wataalamu wa usimamizi wa Mazingira Tanzania (TEEA) inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika mikoa yote.

Michezoni

Katika michezo kampeni za Rais Samia nako zimekita mizizi, ikiwamo ya Goli la mama inayotajwa kuwatia hamasa wachezaji wa timu zinazoshiriki mashindani ya kimataifa, ambapo kila goli hulipwa Sh5 milioni hadi Sh10 milioni kutegemea na hatua ya mashindano.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amekuwa akilipia viingilio kwa mashabiki ili waingie kwa wingi uwanjani kuziongezea nguvu timu zetu kwa kushangilia.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alisema kampeni hiyo imesaidia kuhamasisha wachezaji.

“Sasa hivi tuna ushahidi wa wachezaji, anapambania timu yake ishinde na anapambaia heshima kutoka kwa rais, sio pesa tu peke yake… wenye hizo timu wanatoa bonus hata mara 20 ya hizo anazotoa Mheshimiwa Rais,” amesema.

Alisema fedha hizo zinatokana na fungu la kuchangia huduma za kijamii.

Mbali na ya kampeni hiyo, pia kwenye masumbwi nako wakaja na kampeni ya Rais Samia maarufu ‘Knockout ya Mama.”

Kampeni hiyo iliandaliw ana Mafia Boxing Promotion in Tanzania, ikishindanisha mabondia mbalimbali nchini jijini Dar es Salaam.

Japo kampeni hizi zinalenga kuhamasisha masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na michezo, lakini zinaibua maswali kama ndio kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu na hasa ikijulikana kuwa Rais Samia ameshapitishwa na chama chake kuwa mgombea.

Je, huko sio kutumia madaraka ya urais kupiga kameni za kisiasa? Kutakuwa na usawa gani kwa wagombea wengine wasio na madaraka kama hayo?
 
Lissu agombanie nafasi ya kupeperusha Bendera katika nafasi ya uraisi 2025 huku tunapush na Reforms ili huyu Mama arudi Kizimkazi akalee wajukuu.
 
na useless miracle ya no reform no elections right, gentleman? :pedroP:
Siku mlevi wa madaraka huwa na sifa kama hizi za kwako! Dharai iliyopitiliza. Halafu mambo yakibadilika, anashangaa na kutoamini macho na masikio yake.
 
Ukiona rais anapambwa kwa mapambio hivi jua ni rahisi wa viwango duni machawa yanamchukulia kwa faida.
Kwa kifupi, hatufai kabisa kutuongoza...amewekwa mfukoni kwa kujua / kutojua na baadhi ya watu.
 
Siku mlevi wa madaraka huwa na sifa kama hizi za kwako! Dharai iliyopitiliza. Halafu mambo yakibadilika, anashangaa na kutoamini macho na masikio yake.
sasa gentleman,
inawezekanaje nonsense no reform no elections ikamfanya huyo kibaka ashinde uchaguzi? :pedroP:
 
Ukiona rais anapambwa kwa mapambio hivi jua ni rahisi wa viwango duni machawa yanamchukulia kwa faida.
Kwa kifupi, hatufai kabisa kutuongoza...amewekwa mfukoni kwa kujua / kutojua na baadhi ya watu.
Chema chajiuza kibaya chajitembeza.
 
Kama hiyo promotion zinasaidia watu maskini sijaona baya hapo, let it go
 
Back
Top Bottom