GE2025 Kampeni za kishoa zatikisa 'hakuna kitakachonishinda'

GE2025 Kampeni za kishoa zatikisa 'hakuna kitakachonishinda'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Shamra shamra za kampeni za Ubunge Jimbo la Iramba Mashariki, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida zimeendelea kupamba moto, ambapo maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi kusikiliza sera na ahadi za Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jesca David Kishoa.

Mkutano huo wa kampeni umefanyika leo Septemba 21, 2025 katika Kata ya Gumanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt. Mwigulu Nchemba pamoja na wabunge wateule wa Viti Maalum akiwemo Salome Makamba.

Akizungumza na wananchi, Kishoa amewaomba kumpa kura ya ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao pamoja na kuhakikisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kishindo ili kuendeleza kasi ya maendeleo nchini.

"Oktoba 29 muende mkatiki kwa kishindo ili Mkalama yetu ipate maendeleo makubwa sana, hivi? kwa mnavyonitazama kuna kitu kitanishinda mimi?" amesema Kishoa

Kwa upande wake, Dkt. Mwigulu Nchemba amemwelezea Kishoa kama kiongozi shupavu na mwenye umakini katika kupigania maendeleo ya wananchi, akisisitiza kuwa endapo atachaguliwa, wananchi wa Iramba Mashariki watakuwa wamepata mwakilishi sahihi.

Naye Salome Makamba amewataka wananchi wasitishwe na vyama vya upinzani, akieleza kuwa hata wanachama wake wa karibu wanatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na CCM katika kuwaletea maendeleo Watanzania.​
 
Back
Top Bottom