Kampeni za CHADEMA vs CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni za CHADEMA vs CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kisendi, Aug 12, 2010.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF, Jana nilipata habari kupitia TV zetu kuwa Bw. Tambo hizza akikanusha kilichochapishwa na MwanaHalisi, Lakini pia Mwanahabari Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi Said Kubenea akisema, hizo habari ni za kweli. Yupi tumfuate??

  Pili Me nawaomba chadema kampeni zao wafanye wakitueleza nini watafanya wakichukua nchi?? Tuna matatizo ya maji hapa dar, uchafu, tatizo la kupanda bei ya vitu kiholela, watu kuwa na mali nyingi kuliko kipato i mean mshahara wa kila mwezi, Umeme kukatikati, foleni dsm, viongozi wazembe, wafanyakazi wa umma salary kiduchu huku wabunge na viongozi wa taasisi za umma wakiwa na mishahara juu kama vile TRA, Agency za serikali etc Na mambo mengi chungu nzima.

  Kuhusu ufisadi ni janga la kitaifa watalikomesha je?? Haya wakituambia na tukawapa kura then baada ya miaka 5 tutapima je wametimiza angalau 75% ya yale waliyoahidi kama hakuna tunachagua wengine.


  Kwa upande wa CCM sina jipya maana wana 40 years in governance lakini hatujapata suluhisho la maji mijin kuanzia hapa dsm kuna watu hapa dsm hawajawahi hata kuoga maji ya bomba, mpo?? foleni hili kila mtu analijua, afya bado, bima ni za wachache?? ofisi za serikali bado ziko nyuma kiutendaji hakuna strategic plan, umeme ni shida, vitu kupanda bei kiholela hakuna udhibiti kama other country huwezi kupandisha kitu bila concern iliyokusababisha upandishe.

  Kuhusu kukua uchumi si kweli watu kuwa na magari mengi si tija ya kukua kwa uchumi, sijasoma uchumi lakini ni idea, Magari watu wanamikopo, saccoss etc, angalia shilingi ya tz na shilingi ya kenya tangu mwaka 2006, utaona wenzetu ukienda kwenye dollar wamepaa sisi tunadidimia. Watu wanaweza kuwa na magari kila mtu lakini wanaoga maji ya chumvi, hakuna mashule, hakuna mahospitali za uhakika etc

  Tukipa hayo mimi na ndugu zangu tutaenda kupiga kura otherwise ni kuacha na kuendelea na mengine.

  KIBOGOYO aka Arsenal iliyochoka
  Wana JF mnasemaje hapo??
   
Loading...