Kampeni za CHADEMA na CCM Kimandolu

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,973
9,572
Wana Jf,
Leo kampeni za uchaguzi wa diwani ziliendelea katika kata mbali mbali nchini, ambapo kwa upande wa Kimandolu ccm walikuwa upande wa soko la kimandolu, mkutano wao uliongozwa na Naibu waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanry, jambo ambalo lilishangaza kwenye mkutano wa ccm ni kwamba hakukuwa na salamu za ccm hoyee, baada ya kugundua kuwa hakuna angewautikia, hivyo kila aliyepanda jukwaani alikuwa anatoa salamu za kidini nakuendelea na sera.
Waziri Mwanry aliwadanganya wananchi wa kimandolu kuwa kuna wanavikundi wa kimandolu wamefaidika na mikopo iliyotolewa na halmashauri, na akasema kuwa kikundi cha kimandolu kimepata mkopo wa milioni hamsini, na kwamba hizo ni juhudi zake kama waziri, na endapo wakimchagua atahakikisha yeye kama Waziri ataongeza mikopo kwa wajasilia mali.
Ukweli ni kwamba kikundi cha kimandolu kilikopeshwa shilingi milioni mbili na siyo milioni hamsini kama waziri alivyozungumza, manake wakati anazungumza mimi mwenyewe nilikuwepo nikiwa pamoja na mwenyekiti wa kikundi cha wanakimandolu ndugu Msuya ambaye alimshangaa waziri kwa kuongea uwongo!
Kwanza kitendo cha kuzungumzia kuwasaidia wananchi kwenye majukwaa ya siasa kama waziri kwa kuahidi ahadi kama waziri is an absolute abuse of office!
Mbaya zaidi mkutano wa ccm ulihudhuriwa na watu wachache wasiozidi watu 30!
Picha nilishindwa kuichukua kutokana na mazingira na usalama wangu!

Kwa upande wa CHADEMA mkutano wao wa Kimandolu ulifanyika katika ofisi ya kata ya Kimandolu, ambapo mkutano wao kama kawaida ulihudhuriwa na viongozi wa kata tofauti na mikutano ya ccm ambapo tokea zianze mikutano yao imeongozwa na viongozi wa chama kitaifa kama Nape Nauye, Mwigulu, pamoja na mawaziri Ole Medeye, Mwanri na Kinana!

Katika Mkutano wa CHADEMA mgombea udiwani wa kimandolu aliwaomba umati mkubwa wa watu waliohudhuria mkutano kujitokeza kupiga kura Jumapili ili waweze kufanya mabadiliko, aliwaambia tanzania yenye neema inawahusu wao, na bila kuiondoa madarakani ccm kupitia kwenye sanduku la kura hatutaweza kufika kwenye nchi ya ahadi iliyojaa asali na maziwa ambayo sasa yanafaidiwa na wageni! Aliwaambia yeye pia amekagua ofisi ya kata ameona kuna mapungufu mengi kama walivyoona, hakuna umeme wala choo cha nje, lakini akawaahidi kuwa siyo kipaumbele chake kwa sasa, kwani wananchi kwanza mambo mengine baadaye!
Pamoja na mambo mengine aliahidi kuwa baada ya kuwashughulikia panya waliopo kwenye halmashauri, ataelekeza nguvu zake kwenye ujenzi wa zahanati ambayo ilishatengewa fedha muda mrefu!
Akiongea katika mkutano huo James Ole Milya aliwaambia watu wa Kimandolu wapuuze ukabila unaoenezwa na ccm kwa kumchagua diwani kwa ukabila. Akasema kuwa yeye anaamini katika demokrasia, lakini kitendo cha ccm kutaka wamasai kumchagua Edna kuwa diwani kwa sababu ni masai mwenzao ni kinyume hata na kabila lake la kimasai, akasema ni bora azungumzie demokrasia maana kabila la wamasai sote tunajua mila zao kuhusu nani awe kiongozi wa mila!

Mwenyekiti wa chama kata nyingine kamanda Mungi alielezea kusikitishwa kwake na sms zinazosambazwa na ccm kwa kuwambia kuwa wamchague Edna kwakuwa anaifahamu jiografia ya kimandolu, na kwamba wasimchague mpita njia, kwani ccm ndiyo itawaletea maendeleo wana kimandolu!
Kamanda Mungi aliwaambia kuwa kauli na sms hizi za ccm kwa wanakimandolu ni dharau na dhihaka kwa watu wa kimandolu, akasema kuwa ccm wameongoza kimandolu zaidi ya miaka 50, na pia Meya Laurence Hedi alikuwa diwani wa hapa, lakini hawakufanya chochote kwa wanakimandolu zaidi ya kujijengea baa na gest kwa maslahi yao. Aliwauliza wanakimandolu kama walishawahi kumwona Edna akinunua sukari au sabuni hapa kimandolu? Watu wakajibu hawajawahi!
Akawaambia wasipoteze muda wao, bali wamchague Rayson Ngowi kuwa diwani, kwakuwa anawafahamu wanakimandolu, anaishi kimandolu, na huduma zake za kijamii anazipata kimandolu!
Aliwatahadharisha watu wa kimandolu kuwa wasitishwe wala kushawishiwa na kauli na ahadi za akina Nape na Mwigulu pamoja na mawaziri wote waliofika kimandolu, kwa maana kimandolu inawahusu wanakimandolu, kwani baada ya uchaguzi hao wote hawataonekana tena, sasa kama watamchagua diwani mzuri anayewafaa kutoka chama kinachojali wananchi itakuwa ni amani kwao. Lakini wakimchagua diwani kutoka kwenye chama ambacho kimechoka, hakina Mawazo mapya, watabaki na shida zao, kwani akina Nape watakuwa wameondoka!
Mungi aliwaambia wanakimandolu kuwa hawa wahuni Nape na Mwigulu Mungu aliwapa sauti, lakini aliwanyima akili ndiyo maana badala ya kuongea sera wanatoa matusi!
Aliwaahidi wanakimandolu kuwa wasiwe na wasiwasi, wajitokeze kwa wingi kupiga kura, na sisi tumejiandaa kupiga kura!
Wengine waliopasha jukwaa kimandolu ni pamoja na Bahati David, Derick Magoma!

Tanzania yenye neema inaanzia hapa!

Wasalaam,

Mungi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
asante kwa taarifa zako za uongo zenye kuelemea upande mmoja,
 
asante kwa taarifa zako za uongo zenye kuelemea upande mmoja,

Mkuu huo ndiyo ukweli, hakuna sehemu nimeongea uwongo

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom