Kampeni ya furaha yangu yazinduliwa Nachingwea

Kampeni ya furaha yangu yazinduliwa Nachingwea

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
IMG-20180909-WA0056.jpg
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee Watoto,amehitimisha wiki ya uzinduzi wa Kampeni ya Furaha yangu iliyozinduliwa Septemba 1 Wilayani Nachingwea katika Mkoa wa Lindi.Kampeni hiyo yenye lengo la kuhamasisha wananchi kupima VVU na iwapo mtu kagundulika kuwa na VVU anaanzishiwa ARV mapema.

Akihutubia kwenye kilele cha uzinduzi wa kampeni hiyo, Mhe Ndugulile amesema kuwa kni hii inafuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe Kasim Majaliwa aliyoizindua mkoani Dodoma mwezi Juni kwa lengo la kuhamasisha wananchi na hasa wanaume kujitokeza na kipima VVU.
Alisema kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha ifikapo 2020 watu wote wawe wamepima VVU,watakaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU wawe wameanza kutumia ARV na watakao kuwa wanatumia ARV wawe wamefubaza VVU.

Akizungumzia zoezi la upimaji lililofanyika Wilaya ya Nachingwea alisema hadi tarehe 7 wamepimwa wanawake 809 na wanaume 537. "Hali hii inaonesha wanaume mmejitahidi lakini bado mpo nyuma katika kujitokeza kupima VVU,wanawake wasitumike kama chambo wanaume jitokezeni kupima afya zenu, alisisitiza mhe. Dkt Ndugulile. Serikali haitaki kuona mtu anapata maambukizi mapya ya VVU na kikubwa ni kuanza dawa mapema .
Kabla ya ufungaji wa kampeni hiyo Dkt Ndugulile alianza kwa kutembelea hospitali ya Wilaya na Zahanati ya Nyaipanga ambapo alijionea changamoto mbalimbali,zikiwa ni pamoja na uhaba wa majengo,utunzaji usio sahihi wa dawa na usafi usioridhisha .

Mhe Ndugulile amemwagiza mkuu wa Wilaya kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mil400 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Nachingwea zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Naye Mganga mkuu wa Mkoa Dr Genchwele Makenge alisema kuwa maambukizi ya VVU kwa mkoa wa Lindi yameshuka kutoka asilimia 3.7 mwaka 2011/12 hadi asilimia 0.3 kwa utafiti wa mwaka 2016/17. Aidha mganga mkui wa mkoa aliahidi kufanyia kazi maagizo ya mhe. Naibu Waziri kama alivyoyatoa kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Nachingwea na wasaidizi wake.

Mkurugenzi wa habari na Uraghibishi Bw Jumanne Issango kutoka TACAIDS amepongeza jitihada za Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wananchi wa Nachingwea wanapima na kujua hali zao za maambukizi ya VVU ikiwa ni pamoja na kupata huduma zingine za kiafya zinazotolewa kwa ujumla. Aidha amewatahadharisha kuachana na tabia hatarishi pamoja na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU.
 
Back
Top Bottom