Kampeni ya CCM “Kukataa Katiba Imeanza Rasmi” | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kampeni ya CCM “Kukataa Katiba Imeanza Rasmi”

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by niweze, Dec 29, 2010.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wananchi Tumesikia Jaji Werema? Kampeni ya Kukataa Katiba Ndio Imeanza. JK Kampata Jaji Werema na Wengine Waziri wa Sheria na Katiba Kuanza Kukataa Katiba kwa Kutumia Hii Misemo “Watanzania Turekebishe Katiba kwa Kuweka Viraka” Hatari ya Misemo Kutoka CCM “INATISHIA AMANI NCHINI” Hakuna Kitu Kingine Zaidi. Tukianza kwa Uteuzi wa Jaji Warema na Waziri wa Katiba, Hawa Wenyewe Wametuliwa Kinyume na Matakwa ya Watanzania. Hiki Kipengere cha Raisi Kuteua Wapiga Rangi Viatu Kutoka Kambi ya CCM Tumeshasema ni Hujuma kwa Nchi, Katiba Mpya Haita Ruhusu Uteuzi wa Hizi Nafasi za Serikali.
  Hii Peke yake Sio Tosha Tu Katiba Mpya Itabadilisha Majaji Mahakamani, Wakuu wa Idara za Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na Mawaziri Lazima Waidhinishwe kwa Kupitia Chombo cha Bunge. Bunge la Tanzania Ndicho Chombo cha Kuunda Bajeti, Sheria na Utaratibu wa Serikali Sio Wapiga Kura za Maoni za Raisi Yeyote Yule. Katiba Mpya Itarudisha Nguvu na Uwezo wa Mamlaka ya Bunge Kusimamia Serikali na Kupima Utendaji Wake, Hii ni Sehemu Muhimu ya Jamii ya Watanzania. Katiba Mpya Itatoa Mipaka ya Maamuzi ya Ofisi za Serikali Ikiwemo Ofisi ya Raisi na Baraza Lake na Chombo cha Mahakama Kitapewa Madaraka Bila Kuingiliwa na Siasa. Kikubwa ni Nafasi za Majaji Mikoani, Nafasi Zita Jazwa kwa Upigaji wa Kura za Wananchi. Katiba Mpya Itatoa Mamlaka kwa Mahakama na Vyombo vya Usalama Kupeleleza kwa Ubinafsi Kesi Yeyote Bila Kuingiliwa na Wanasiasa. Zaidi Katiba Mpya Itaondoa “Immunity” na Uwezo wa Kulinda Viongozi Waliofanya Vitendo vya Rushwa au Hujuma Zozote Zile na Kufikishwa Mahakamani Kulazimika Utendaji wa Haki. Hii Inahusisha Kuanzia Raisi, Mawaziri, Wakurugenzi, Majaji, na Maofisa Wote wa Serikali Watafishwa Mahakamani Bila Vipingamizi. Katiba Mpya Itazumzia kwa Kipengere cha Upigaji wa Kura Nchini kwa Ajili ya Kulinda Demokrasia. Katiba Mpya Itatoa Njia ya Wazi ya Upigaji Kura na Usimamizi Utakao Toa Haki kwa Vyama Vyote vya Siasa. Katiba Itatoa Ufafanuzi wa Kisheria Jinsi Gani Kamati ya Usimamizi wa Kura Utafanyika na Jinsi Gani Wagombea Watepewa Nafasi ya Kupinga Uchaguzi Katika Nafasi Zote.
  Kikubwa Katiba Mpya Itazungumzia “Kuondolewa kwa Madaraka ya Chama Kimoja Ndani ya Maamuzi. Katiba Mpya Itaweka Sheria za Haki za Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari Tanzania. Katiba Mpya Ndio Chanzo cha Maendeleo ya Nchi Yetu Sote. Wananchi Tusidanganyike na Mabadiliko Madogo Madogo Wanataka Kutufunga Kamba Kama Miaka Hiyo 50 Iliopita, Sasa Hatuna Muda na Tutapambana Nao Mitaani kwa Nguvu.
   
 2. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili limezungumzwa sana humu, tupe way forward tu hapa.
   
 3. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Moderator,

  Mimi nadhani kama mtu analeta thread halafu hajajiandaa kuleta solutions basi ni afadhali asilete au thread ile ifichwe kabisa uvunguni. Kuna watu huwa tunawasimulia kwamba JF ni kijiji cha thinkers unakoweza kupata habari au constructive contribution.

  Sasa watu wa aina hii wanataka kukigeuza hiki kama kijiji cha malalamiko, manung'uniko na kila aina ya maneno yenye muelekeo wa inferiority complex.

  Hivi ni wapi duniani mlikoona hali inabadilika kwa malalamiko ya inferiority complex? Kama mwenzako kakuzidi nguvu unachotakiwa ni kutumia bongo zenu kujua mtamzidi vipi.

  Huyu jamaa analeta thread kwamba CCM imeanza mikakati ya kukwamisha Katiba mpya. Huku ni kukosa mawazo kabisa. Hivi ulitegemea CCM wakusaidie kukuunga mkono kwa hilo.

  Kama hoja ya katiba mpya imeundwa kiuhakika kwa nini uwe na wasiwasi na CCM kutoipenda.

  Ujasiri pekee ni kutambua kwamba CCM hawaipendi hoja hii, hivyo hoja inajengwa kiasi kwamba yeyote anayeipinga anaonekana kama ni **** kweye jamii.

  Sasa wanaolalamika humu ni wale ambao uwezo wao wa kujenga hoja ni mfupi. Sijasikia mahala John Mnyika anayepeleka hoja ile bungeni akilalama kampeni za kuipinga hoja yake. Unadhani hajui kwamba majority ya CCM bungeni ni 78%.

  Huwezi kupima hata kwenye ushabiki kwamba Yanga hawalalamiki Simba wanapoanza kampeni ya mazoezi kabla ya mechi ya watani hawa wa jadi.

  Watu kama nyinyi ndiyo mnaofanya CHADEMA ionekane ina uchanga wa siasa au imejaa vijana wenye vurugu.

  Usitegemee upanie kumptisha mbuzi wako kwenye pori lililojaa chui halafu ulalamkie kwamba chui wameanza kutoka udenda wa tamaa....
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya Mwingine Hao. Wanataka Kutuonyesha Yeye Amefikia Malengo ya Kutaka Mtanzania Yupi Azungumze Anavyotaka Yeye na Wakati Gani. Kuanzia Sasa Tusikize Nyie na Majaji na Mawaziri Mkidanganya Watanzania Kwamba Hakuna Haja ya Katiba Tukae Kimya, Unafikiri Tanzania ni IRAN SIO. Hiki Chombo Jamii Sio Kutaka Malumbano Peke Yake Ila Kuleta Information kwa Wananchi na Kufafanua Umuhimu wa Kila Kona Katika Katiba. Lengo la Hii Thread Sio Kuleta Opinons Zako. Kama Unajua Kusoma na Kuandika Utaona Thread Imezungumza Nini na Why We need These Changes in Our Constitution, Mifano

  "Bunge la Tanzania Ndicho Chombo cha Kuunda Bajeti, Sheria na Utaratibu wa Serikali Sio Wapiga Kura za Maoni za Raisi Yeyote Yule. Katiba Mpya Itarudisha Nguvu na Uwezo wa Mamlaka ya Bunge Kusimamia Serikali na Kupima Utendaji Wake, Hii ni Sehemu Muhimu ya Jamii ya Watanzania. Katiba Mpya Itatoa Mipaka ya Maamuzi ya Ofisi za Serikali Ikiwemo Ofisi ya Raisi na Baraza Lake na Chombo cha Mahakama Kitapewa Madaraka Bila Kuingiliwa na Siasa"
  Katiba Mpya Itaondoa "Immunity" na Uwezo wa Kulinda Viongozi Waliofanya Vitendo vya Rushwa au Hujuma Zozote Zile na Kufikishwa Mahakamani Kulazimika Utendaji wa Haki. Hii Inahusisha Kuanzia Raisi, Mawaziri, Wakurugenzi, Majaji, na Maofisa Wote wa Serikali Watafishwa Mahakamani Bila Vipingamizi. Katiba Mpya Itazumzia kwa Kipengere cha Upigaji wa Kura Nchini kwa Ajili ya Kulinda Demokrasia

  Kwa Kufafanua kwa Wale Wanashindwa Kusoma na Kuandika Mpaka Wasomewe na Kuandikiwa ni Hivi. "In Short The Country Need to Establish Check and Balance System = Bunge, Mahakama na Executive Branch-Ofisi ya Raisi" Wachache CCM Mnataka Chadema Wazungumzie Strategies za Kwenda Mbele na Kama Huoni Kazi ya Chadema na Matunda Yake Mpaka Sasa Hivi Basi Wewe Kipofu Wakupindukia. Tangu Kampeni Zianze Wananchi Wameweza Kuonyeshwa, Kujengeka na Kuimarishwa na Information na Wamepata Hope ya Uongozi Mpya Ukipatikana - Test of New Tanzania. Tangu NEC Waibe Kura, Wananchi Wameshuhudia Wizi na Ujambazi wa CCM na Kitendo cha Chadema TO Walk Out From Bunge, Kimewamsha Wananchi Jinsi Gani Nguvu Tunazo. CUF na CCM Sasa Ndio Wanasikia Hasira za Watanzania. Wananchi Tukiangalia Mbele, Wananchi Wakiwa Nyuma ya Chadema Tuna Strategies za Kuleta Katiba na Back Up Plans za Kila Jambo. Wewe Unauliza the Way Forward Unafikiri Hakuna? Watanzania Wanaendelea Kuelimishwa na Kuamshwa Taifa Zima na Hii ni Chadema Tu. Tunalipeleka Swala Bungeni na Ku-Mobilize Efforts Zote za Watanzania. Hii Jamii Inatoa Opportunity Kuwaelimisha Watanzania Zaidi Juu Umuhimu wa Katiba Sio Kukaa Kimya Kama Nyie Makada Manaotaka Kufuata "Fikra za Kitumwa na Umaskini" CCM Sio Chama cha Majibu Tena Wananchi Tunakuona Huna Mawazo na Uchungu wa Nchi Ndio Unabaki Kuuliza na Kushangaa Kwanini Thread za Katiba Zinakuja Kila Leo. Jifungie Umeridhika na Connections Mlizonazo Ndani ya Mafisadi. Hata Mara Moja Sijasikia Wananchi Wameshindwa Nchini Kwao, 78% ya CCM ni NEC/JK = Uhujumu na Maafa

  "Kiu cha Katiba Hakitakoma Hata Wananchi Wachache Watake au Wasitake. Wananchi Tunasonga Mbele Kubalisha Katiba 2011"
   
Loading...