Kampeni mpya ya Utalii Tanzania ina ufisadi

Kampeni mpya ya Utalii Tanzania ina ufisadi

mzirayk

Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
13
Reaction score
20
Juzi wakati waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Hamisi Kigwangalla akiwasilisha bajeti ya wizara yake alilieleza bunge kuwa katika kuhakikisha Tanzania inapata watalii wengi zaidi, kampeni ya kuitangaza vivutio vyetu ndani na nje ya nchi itazinduliwa na itapewa jina la Unforgettable Tanzania.

Ukweli ni kwamba kampeni hii sio mpya, wakati wa awamu ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete wizara ikiwa chini ya Mheshimiwa Nyalandu wakati huo ilitoa tenda ya kutengeneza kampeni ya utalii, kilichotokea TTB wakachagua mtu wao na wizarani wakawa na mtu wao. Matokeo yake kukawa na kampeni mbili, moja ikiwa ni The Soul Of Africa na nyingine ikawa ni Unforgettable Tanzania. Figisu zikafanyika kwa ushawishi aliokuwa nao Mheshimiwa Nyalandu ile kampeni ya watu aliowachagua yeye ikapitishwa na kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais pale Hyatt.

Fast Forward 2018 kampeni hii ambayo ilikataliwa tunaambiwa ndio itatumika na tunaambiwa kwamba kampuni imeshapewa tenda ya kuifanya wakati ukienda YouTube (angalia video niliyo-attach) unaona video yake iliyokuwa uploaded 2015 na kwenye bajeti utaambiwa na kuna mtu kalipwa kuifanya wakati malipo yalishatoka tangu enzi za Kikwete.

Kaka yangu Hamisi Kigwangalla inawezekana kuna watu wanakupotosha hawakuelezi ukweli ili waandae upigaji, sitaki kuamini kwamba wewe kwa uadilifu ulionao unaweza kuingia kwenye mtego wa kitoto namna hii wa upigaji wa mchana wakati kila mtu wizarani inajulikana wazi nini kinaendelea na unajua kabisa watu wataongea. Muogope Mungu.

Hii video iko kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu sasa, tangu utawala wa awamu ya nne. Pamoja na uzuri wake ambao ni wa asili lakini ina mapungufu kwenye maudhui yake ambayo yanatangaza zaidi kanda ya kaskazini, tamaduni za kimasai na wanaoitangaza zaidi ni watalii wenyewe.

Video hii kwa umuhimu wake nashauri ihaririwe upya na iongezewe vivutio vingine vingi tu kutoka kanda takribani zote za nchi hii kwa mfano yale mawe ya Mwanza, Ziwa Tanganyika na MV. Liemba yake, miundombinu ya reli ya kati, mito na mabonde ambavyo vyote vikikusanywa kwa uangalifu tutapata video inayosimama kutangaza vivutio tulivyonavyo Tanzania.
 
Utalii mwaka 2012 had 2015 ulikuwa unaongezeka kwa 15% Kila Mwaka

Mwaka 2016 had 2017 - Utalii unaongezeka kwa 3%

--Huyo mtoa Mada (alieanzisha huu uzi-thread) lengo lake ni kusifu au kudanganya Watanzania?

Tatizo ni kutojua Data, information za Utalii watu hawana na ili kulinganisha

Rwanda, Uganda wanatuzidi kwa ongezeko la watalii

Mauritious, Seycheles wanatuzidi idadi ya utalii kwa Lipi?
 
Ongezeko la utalii na kutaka kufanya ufisadi vinahusiana nini?
 
Utalii mwaka 2012 had 2015 ulikuwa unaongezeka kwa 15% Kila Mwaka

Mwaka 2016 had 2017 - Utalii unaongezeka kwa 3%

--Huyo mtoa Mada (alieanzisha huu uzi-thread) lengo lake ni kusifu au kudanganya Watanzania?

Tatizo ni kutojua Data, information za Utalii watu hawana na ili kulinganisha

Rwanda, Uganda wanatuzidi kwa ongezeko la watalii

Mauritious, Seycheles wanatuzidi idadi ya utalii kwa Lipi?
Karai
 
Back
Top Bottom