Mshani de Orbital
Member
- Oct 10, 2014
- 14
- 4
kesho jumanne serikali kupitia mhimili wake wa 'serikali kuu' itatia kambi kunako viwanja vya K.I.U-Dar branch kupitia mwakilishi wa kiongozi mkuu wa mhimili huo(DK Mrisho J.K) akiwakilishwa na bw. RYMOND MUSHI mkuu wa wilaya ya ilala,kutolea ufumbuzi wa kanjanja linaloendelea hivi sasa,mhimili huu umeahidi ya kuwa kesho ndio itakuwa mwisho wa magumashi yanayoendelea chuoni hapo kwa kuwa itatia timu chuoni hapo ikiwa na wahusika wote wa sakata hili.
Ahadi hii imewapa wanafunzi hali ya kuwa na imani na mwakilishi huyo wa rais ambaye ameonyesha nia ya kulimaliza tatzo hili hasa baada ya waziri wa elimu kushindwa kufikia walau pale alipofikia mwakilishi huyu wa rais(mkuu wa wilaya ya ilala),kunako ijumaa ya 8 may 2015 aliweza kufika chuoni hapo na maafisa wa NACTE na maafisa hao kukiri kutokitambua chuo lakini walitoa muongozo wa kuanza kukitambua chuo kuanzia tar 5 may 2015 kwa kuwaonyesha wanafunzi barua ya utambuzi wa chuo hiki na kuahidi kuanza kuwaingiza wanafunzi wa diploma na vyeti wa chuo hiki katika mifumo ya NACTE ili waweze kutambuliwa rasmi.
Pamoja na hatua hiyo iliyofikiwa na wanafunzi hao lakini bado walimwakikishia mkuu wa wilaya hawatoingia darasani mpaka hapo matatizo yao yote yatakapokamilika ikiwa ni pamoja na kurudi kwa wenzao.
mhimili huu unaonekana kuonyesha nia baada ya muda mrefu kupita hii inatokana na sababu kuwa tayari malalamiko haya ya wanafunzi hawa yamekwisha wasiliswa katika kamati ya mhimili wa pili unaotenda shughuli zake kwa kisheria zaidi yaani BUNGE kupitia kambi ya upinzani ambayo imeahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo ndani ya wiki hii.