Kamkopesha mkwe pesa ya ada, sasa mahusiano yameingia dosari

Yohana Daniel

Member
Mar 18, 2018
59
24
Kuna rafiki yangu mmoja more than a friend alikua na mpenzi wake walipendana sana japo walianza wakiwa wadogo, walipeana ahadi nyingi sana maishani mwao mpaka wazazi wa pande mbili wote walijua mahusiano yao, bahati mbaya ama nzuri binti alikua anakaa na mama yake, kizuri ni kwamba mama yake binti alimpenda sana rafiki yangu hivyo basi akawa anashirikiana nae katika mambo mbalimbali japo rafiki yangu kwao hali ni duni.

Alijitahidi kadri ya uwezo wake,ndipo one day yule mama alimuomba rafiki yangu amkopeshe pesa na jamaa hakusita kumpa japo alimpa pesa ambayo ni ada ya shule kwa kua yule mama alisema atamrudishia but siku nenda siku rudi hakuna kurudishiwa pesa na shule anadaiwa ikabidi amwambie yule mama vipi kuhusu ile pesa duuuh kilichotokea mpaka sasa hakuna mahusiano mazuri hapo. Ushauri wenu wana JF tafadhali afanye nn?
 
Kama ana malengo ya mda mrefu na huyo binti ni bora tu asamehe hilo deni kwa Mama, otherwise he’ll end up loosing both the girl and money!
 
Yaani mpaka sasa wame breakup sababu ya hilo deni jamaa amebembeleza binti haelewi
 
kiufupi ukimkopesha mtanzania pesa ujue unapoteza pesa na unampoteza yeye haijarishi ni mkwe,rafiki au mpenzi
 
Ukitaka kuona ugumu wa kudai deni lako kopesha ukweni

Hela siku zote ina ibilisi ningesema sina sema lishatokea sina namna
 
Huyo bila shaka ni mwanaume wa Dar. Unamkopeshaje Mkwe au mpenzi wako? Huyo mwanaume hata hajui majukumu yake.
Kwani anapombinua mtoto wa watu amelipia mahari? Mwambie aache ujinga.
 
Hela ilikua ni ya Ada alikua ana chezanayo ya nini? au ametaka kuonekana kidume? kwani ni M ngapi mpaka anapiga kelele?
 
Kuna rafiki yangu mmoja more than a friend alikua na mpenzi wake walipendana sana japo walianza wakiwa wadogo, walipeana ahadi nyingi sana maishani mwao mpaka wazazi wa pande mbili wote walijua mahusiano yao, bahati mbaya ama nzuri binti alikua anakaa na mama yake, kizuri ni kwamba mama yake binti alimpenda sana rafiki yangu hivyo basi akawa anashirikiana nae katika mambo mbalimbali japo rafiki yangu kwao hali ni duni.

Alijitahidi kadri ya uwezo wake,ndipo one day yule mama alimuomba rafiki yangu amkopeshe pesa na jamaa hakusita kumpa japo alimpa pesa ambayo ni ada ya shule kwa kua yule mama alisema atamrudishia but siku nenda siku rudi hakuna kurudishiwa pesa na shule anadaiwa ikabidi amwambie yule mama vipi kuhusu ile pesa duuuh kilichotokea mpaka sasa hakuna mahusiano mazuri hapo. Ushauri wenu wana JF tafadhali afanye nn?
Aende chooni. i mean choo cha shimo alieee weee mpaka hamu iishe then amuachie Mungu
 
Kuna rafiki yangu mmoja more than a friend alikua na mpenzi wake walipendana sana japo walianza wakiwa wadogo, walipeana ahadi nyingi sana maishani mwao mpaka wazazi wa pande mbili wote walijua mahusiano yao, bahati mbaya ama nzuri binti alikua anakaa na mama yake, kizuri ni kwamba mama yake binti alimpenda sana rafiki yangu hivyo basi akawa anashirikiana nae katika mambo mbalimbali japo rafiki yangu kwao hali ni duni.

Alijitahidi kadri ya uwezo wake,ndipo one day yule mama alimuomba rafiki yangu amkopeshe pesa na jamaa hakusita kumpa japo alimpa pesa ambayo ni ada ya shule kwa kua yule mama alisema atamrudishia but siku nenda siku rudi hakuna kurudishiwa pesa na shule anadaiwa ikabidi amwambie yule mama vipi kuhusu ile pesa duuuh kilichotokea mpaka sasa hakuna mahusiano mazuri hapo. Ushauri wenu wana JF tafadhali afanye nn?
Mwambie aje aanzishe uzi yeye mwenyewe ndo tumshauri , bila shaka wewe ndo muhusika unatumia mwamvuli wa rafiki yako. Msamehe tu , hamna namna ila usirudie kumkopesha tena
 
Ni mtazamo wako tyuu ila kikubwa shukrani kwa ushauri coz yeye mimi na mimi yeye sio mbaya thanks
 
Back
Top Bottom