Pengine mleta mada amekumbwa na mhemko. Membe atamuachiaje Lissu agombee peke yake halafu Chadema kitarajie kushinda uchaguzi wakati kimeshindwa kuweka wagombea katika majimbo yote 264? Chadema kimeweza kupata wagombea 163, nakisi ni wagombea 101.
Bila shaka umeelewa kuwa kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni Lissu kushirikiana na Membe kupata synergies za kuifurusha CCM madarakani asubuhi na mapema. Umoja ni nguvu.....usipalilie utengano.