Kambi za mafuriko Dar ‘zatiwa kufuli’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kambi za mafuriko Dar ‘zatiwa kufuli’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 7, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 06 January 2012 19:53

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Joseph Zablon

  SERIKALI imetangaza kuzifunga kambi rasmi 15 zilizokuwa zikitumika katika kuwahifadhi watu waliokumbwa na mafuriko, yaliyotokana na mvua zilizonyeshwa mwishoni mwa mwezi uliopita, jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inalenga katika kutoa nafasi kwa wanafunzi wa shule zilizotumika kwa shughuli za kambi hizo, kuanza masomo baada ya shule hizo kufunguliwa rasmi Jumatatu ijayo.


  Kufungwa kwa kambi hizo, kulitangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick ,ambaye alisema kambi hizo zilifungwa jana jioni. Sadick alisema hatua hiyo imekuja wakati maandalizi kuhusu makazi mapya kwa ajili ya watu hao, yakiwa yamekamilika.


  Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa msingi huo, kuanzia leo wananchi waliokumbwa na mafuriko, hawapaswi tena kuonekana katika kambi hizo.


  Alisema badala yake, wanapaswa kuhamia katika eneo la viwanja vyao vilivyopo Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Alisema hata hivyo, viwanja hivyo ni kwa ajili ya watu waliokuwa wanamiliki nyumba zilizoathiriwa na mafuriko katika maeneo ya mabondeni. Kuhusu wapangaji, alisema wanapaswa kutafuta nyumba zingine za kupanga katika maeneo mbalimbali salama, kama ilivyoagizwa na Serikali.


  "Mbweni na kwingineko ni kwa ajili ya watu waliokuwa wanamiliki nyumba mabondeni na wale ambao walikuwa wapangaji wanapaswa kutafuta nyumba katika maeneo mengine na hilo tuliishawatangazia" alisema Sadick. Kuhusu watoto wanaosoma, Mkuu wa mkoa alisema watapatiwa nafasi katika shule za jirani na eneo wanakohamia wazazi wao.


  Kwa mujibu wa kiongozi huyo, tayari Serikali imeshawataka wazazi kushughulikia uhamisho wa watoto hao kutoka katika ofisi za elimu za wilaya ambazo nazo zimetakiwa kuondoa urasimu katika kushughukilia uhamisho huo.


  "Tumewaagiza waondoe urasimu na kuwapa watoto uhamisho wa haraka ili waweze kuendelea na msomo wakati mipango inafanywa ya kuongeza vyumba vya madarasa katika shule wanazokwenda,” alisema Mkuu wa mkoa.


  Alisema hatua kama hiyo itafanywa pia katika huduma za afya kwa kuongeza majengo ya kutolea huduma hizo katika maeneo jirani na Mabwepande.  Alisema mikakati hiyo inalenga katika kukidhi mahitaji ya huduma za afya na elimu kwa wananchi hao ambao katika hatua za awali, wataishi katika mahema yaanayojengwa na vijana wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania.  Sadick alisema ofisi yake inafikiria ama kuwanunulia sare za shule na vifaa vingine watoto au kuwapa fedha wazazi wao kwa ajili ya kuwanunulia vitu hivyo muhimu kwa masomo.


  Akizungumzia viwanja alisema watakaopewa, watakabidhiwa hati ambazo hazihamishiki.


  "Mwenye wazo la kukiuza kiwanja mara baaada ya kupewa alifute" alisema kiongozi huyo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Ina Maana Serikali haikupata Misaada ya Mahema? UN na Red Cross hutoa Mahema ambayo wangeyajenga Maeneo ya Juu kwa wananchi pia wangepewa vyoo vya nje kwa wananchi wake ni bora kweli na visafi vinasaidia wananchi wetu.

  Sasa inaonyesha labda walipewa pesa na kuvichimbia kibindoni sababu naona shule simefungwa sasa kwahiyo sijui hawa wananchi walio kumbwa na matatizo ya Mafuriko sijui watakwenda wapi? Mipango yetu Mibovu kweli
   
Loading...