Kambi rasmi ya Upinzani, yalaani Kutekwa Kwa Mwanahabari Bi Salma Said Zanzibar

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Tanzania na dunia nzima inaelewa kuwa marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ni batili. Na kwa kuwa uchaguzi huu ni batili, watawala yaani Chama cha Mapinduzi kimeingia katika historia ya kipekee duniani kwa kuwanyima haki wananchi wake.

Matukio mbalimbali yanayoendelea Zanzibar ikiwemo matumizi ya nguvu, vitisho na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea kuitia Serikali ya CCM doa si kwa taifa letu tu pekee bali pia kwa dunia nzima.

Tukio la kutekwa kwa mwanahabari Bi Salma Said wa Deutsche Welle (DW) kimezua maswali makubwa lakini hofu kubwa kwa wananchi, familia yake na wadau hasa wanahabari wa ndani ya nchi na jumuia za kimataifa. Ni dhahiri kuwa kutekwa kwa Bi. Salma Said kunatokana na kazi yake ya uanahabari na ndio maana ushahidi wa awali ambao umepatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, unaelezea wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea hasa katika uchaguzi batili wa marudio ya Zanzibar.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inalaani kwa nguvu zote kitendo cha utekaji wa mwanahabari huyu kutokana na kazi yake. Aidha, tunaitaka Serikali kuhakikisha kuwa mama, dada, rafiki na ndugu yetu Bi Salma Said anapatikana akiwa salama.

Tunaendelea kuamini kuwa kuchelewa kupatikana kwa Bi Salma Said na ukimya wa vyombo vya Serikali na Usalama ni matokeo ya uminyaji wa demokrasia kwa wale wasiofanya kazi kwa mashinikizo ya Chama tawala.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, itaitisha maandamano makubwa nchini ili kushinikiza upatikanaji wa haraka wa Bi Salma Said lakini pia kupaza sauti kwa ulimwengu kuwa Tanzania si mahali salama kwa wanahabari.

Kwa niaba ya Kambi ya Upinzani Bungeni, tunaungana na watanzania wote hasa familia ya Bi Salma Said na watu wote wenye mapenzi mema kumuombea heri Bi Salma na kuamini kuwa atapatikana akiwa Salama Salmin na kuwatia hatiani watekaji wake.

Imetolewa na,

Joseph O. Mbilinyi (MB)

Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo.

19/03/2016
 
Naona watamwachilia wakishamaliza maigizo yao ya uchaguzi wao. Alafu wanasema uchaguzi wa huru na haki wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa .
 
Afadhali tushirikiane kupiga kelele ili mama huyu aachiwe na dhuruma inayoendelea zanzibar ikome
 
1458484343301.jpg
 
kwani akiwa mke wa mbunge wa cuf ndio atekwe ? Acha chuki zilizopindukia

Msirudie kuleta Mchezo na Maisha ya watu kupata Kick za kisiasa kama ile ya Ulimboka Mkamuokota kwny Msitu wa Mabwepande mkiwa na "Watetezi wa Haki za Binadamu" na Live coverage yaTV's stations na msururu wa wanahabari. Yaani by councidence wote mkajikuta mko eneo la tukio kumuokoa alieteswa. Hii ni awamu ya JPM hataki maigizo.
 
Ni dhahiri kuwa kutekwa kwa Bi. Salma Said kunatokana na kazi yake ya uanahabari na ndio maana ushahidi wa awali ambao umepatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, unaelezea wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea hasa katika uchaguzi batili wa marudio ya Zanzibar.
Katekwa,Kajiteka au kaenda kwa hawara kula sikuku kuu naye? Ripoti za kupotea mwanamke au msichana mtu mzima ukizipeleka polisi husita kidogo.Wakaishia tu kusema sawa ripoti tumepokea.Maana aweza kuwa kaenda mchepuko.

Hicho kisauti kinachosemekana kinafanana na chake ndio ushahidi tosha wa kusema katekwa na serikali au na polisi?.Hawa waliotoa tamko hilo wana uhakika ni yake au ya kuigiza? wao ni wataalamu wa Forensic? Wakiburuzwa mahakamani waweza toa ushahidi kuwa polisi wanahusika?

Wanasiasa wa Tanzania hasa wa upinzani hawajui sheria.Huyo mfano yuko guest house na hawara ndiko anakopigia wao ndio wanajua aliye guest house na hawara na aliyetekwa?

Anaweza kufanya mchezo wa kuigiza kuwa katekwa ili kupandisha joto la kisiasa lakini ni hatari kwake ikigundulika kuwa wakati anapiga hiyo simu alikuwa kifuani kwa mtu au alikuwa nyumbani kwa nduguze katulia akijifanya katekwa.

Alichofanya yawezekana ni michezo ile ya kitoto unajificha halafu unawataka wenzio wakutafute ulipojificha!!!! Ujinga mtupu.Siasa za kitoto na za kizamani
 
Msirudie kuleta Mchezo na Maisha ya watu kupata Kick za kisiasa kama ile ya Ulimboka Mkamuokota kwny Msitu wa Mabwepande mkiwa na "Watetezi wa Haki za Binadamu" na Live coverage yaTV's stations na msururu wa wanahabari. Yaani by councidence wote mkajikuta mko eneo la tukio kumuokoa alieteswa. Hii ni awamu ya JPM hataki maigizo.
http://unaonekana ulifeli vibaya sana darasani

Badala ya kujibu suala unajiuma uma vidole kwa mdomo jama demu anaetongozwa
 
Msirudie kuleta Mchezo na Maisha ya watu kupata Kick za kisiasa kama ile ya Ulimboka Mkamuokota kwny Msitu wa Mabwepande mkiwa na "Watetezi wa Haki za Binadamu" na Live coverage yaTV's stations na msururu wa wanahabari. Yaani by councidence wote mkajikuta mko eneo la tukio kumuokoa alieteswa. Hii ni awamu ya JPM hataki maigizo.
TAREHE 25 NANI ALISHINDA?
 
Katekwa,Kajiteka au kaenda kwa hawara kula sikuku kuu naye? Ripoti za kupotea mwanamke au msichana mtu mzima ukizipeleka polisi husita kidogo.Wakaishia tu kusema sawa ripoti tumepokea.Maana aweza kuwa kaenda mchepuko.

Hicho kisauti kinachosemekana kinafanana na chake ndio ushahidi tosha wa kusema katekwa na serikali au na polisi?.Hawa waliotoa tamko hilo wana uhakika ni yake au ya kuigiza? wao ni wataalamu wa Forensic? Wakiburuzwa mahakamani waweza toa ushahidi kuwa polisi wanahusika?

Wanasiasa wa Tanzania hasa wa upinzani hawajui sheria.Huyo mfano yuko guest house na hawara ndiko anakopigia wao ndio wanajua aliye guest house na hawara na aliyetekwa?

Anaweza kufanya mchezo wa kuigiza kuwa katekwa ili kupandisha joto la kisiasa lakini ni hatari kwake ikigundulika kuwa wakati anapiga hiyo simu alikuwa kifuani kwa mtu au alikuwa nyumbani kwa nduguze katulia akijifanya katekwa.

Alichofanya yawezekana ni michezo ile ya kitoto unajificha halafu unawataka wenzio wakutafute ulipojificha!!!! Ujinga mtupu.Siasa za kitoto na za kizamani
Dunia inawashanga sana
 
unaonekana ulifeli vibaya sana darasani

Badala ya kujibu suala unajiuma uma vidole kwa mdomo jama demu anaetongozwa

Ningefeli vibaya darasani si ungeniona nagombea Uenyekiti wa Chama chako? Kumbe ukitongozwa huwa unajiuma uma vidole mie sitombi watafuna kucha tafuta Mwingine!
 
Back
Top Bottom