Kamati za Kudumu za Bunge acheni Usanii

Kamati za Kudumu za Bunge acheni Usanii

Mtingaji

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
1,223
Reaction score
367
Kamati za Kudumu za Bunge zinaendeleza na ku-support Wezi wanako kwenda kukagua. Utasikia Kamati ya Kudumu ya Bunge ina kataa report ya mkurugezi wa Halmashauri ina muelekeza akairekebishe kwani ina short ya fedha! Hii ni sawa na kumwambia aende akachakachue risiti na taarifa ili mahesabu ya tally. Huu mimi naona ni kulindana na kuendeleza wimbi la wizi.

Kama ripot haitally na hali halisi, kamata yeye sukuma ndani alipe au ale mvua za kutosha na viboko 12! Kamati hizi zinaendeleza usanii na wizi wa fedha za walipa kodi!
 
Ni kweli mkuu..hizi kamati nyingi zimewekwa mifukoni na zimekuwa chanzo cha wizi sana hapa nchini...kumbuka sakata la majiya sumu ya mgodi wa north mara ...mpaka leo wananchi wanalalamika sumu zinamwagwa na kamati ishaenda watu wakala posho mchezo ukaisha.........
 
kamati hizi sidhani kama zinajua majukumu yao zimejipachika madaraka makubwa nilikuwa nashangaa pale zilipokuwa zinaamuru watendaji waktwe mshahara wakati zinajua fika hawana uwezo huo kisheria kama wamegundua makosa waeleze mapungufu n
 
Haya ndo matatizo ya kuwa na Wabunge vilaza, wanawekwa kwenye kamati kwa ushabiki, ukichanganya na njaa zao, basi ni balaa tupu! Kuna haja kubwa hizi kamati kuundwa kwa kuangalia vigezo vya uwezo na taaluma ya mtu!
 
Alafu mimi namshangaa CAG. Kwanini anapangiwa kazi na Wabunge? Utaratibu wao wa kazi upoje wakati wametapakaa kila Mkoa!
 
Tungewaheshimu sana iwapo wakigundua kuna ubadhilifu sehemu, wasingekuwa wanamuomba mtoa taarifa akarekebishe mahesabu bali, Wangekuwa wana mkabidhi kwa TAKUKURU ama Polisi afunguliwe mashtaka ya wizi!

Tena huko kwenye Halmashauri, taasisi, mashirika na makampuni ya umma ndiko kuna "akina-jairo" wa kumwaga!
 
Hizi kamati za bunge zingefaa ziwe na wataalamu ya fani ambazo kamati hizo zinahusika. Kwa mfano kama kamati inaangalia mambo na matumizi ya fedha, inabidi mtaalamu wa ukaguzi na matumizi ya fedha awaepo ili kazi ifanyike kitaalam zaidi.
 
Ndiyo maana tunasema kuna haja ya kubadilisha mfumo mzima wa serikali na bunge i mean mihimili yote ili kuleta tija katika kusukuma mbele gurudu la maendeleo.Watu wanafanya kazi kwa mazoea ndiyo maana mambo yanapelekwa sivyo ndivyo.
 
Back
Top Bottom