Kamati yakwamisha bajeti ya Uchukuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati yakwamisha bajeti ya Uchukuzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 28 May 2011 10:33

  [​IMG]

  Waziri Omari Nundu

  Exuper Kachenje
  KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imeyakataa mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Uchukuzi yaliyowasilishwa jana mbele yake jijini Dar es Salaam.

  Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa pamoja na mambo mengine katika mkutano huo ambao waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia, wizara hiyo iliwasilisha mbele ya kamati hiyo mapendekezo ya bajeti yake kwa mwaka 2011/2012, lakini ikabainika kuwa na upungufu mwingi na hivyo kamati kuikataa.

  Kwa mujibu wa habari hizo ambazo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walizithibitisha jana kwa gazeti hili juu ya kuikataa bajeti hiyo ni kuwa ina upungufu mwingi.

  Baadhi ya maeneo yaliyotia shaka na hivyo kufanya kiamati hiyo iikatae ni kukosekana kwa fedha iliyotengwa kwa ajili ya huduma za meli, ndege na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)

  “Hizi ni processes tu, ipo kikanuni. Tukasema hapana irudi ikarekebishwe na kama itashindikana, haitaenda hata bungeni,” chanzo cha habari kilieleza.

  Hata hivyo, chanzo kikadokeza kuwa kamati imeipa siku tatu wizara hiyo kufanya marekebisho hayo na baada ya hapo itaandaa ujumbe maalumu kwa ajili ya kwenda kuzungumza na waziri mkuu kuhusu tatizo hilo.

  Pamoja na kuikataa, kamati hiyo iliiagiza wizara hiyo chini ya Waziri Omari Nundu kuifanyia marekebisho ndani ya siku tatu na kuiwasilisha upya mbele ya kamati hiyo Jumatatu.

  "..Tumeipitia na kuona upungufu mwingi, ndiyo maana tunataka urekebishwe kwanza," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo aliyeomba kutotajwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa kamati.

  Alipotakiwa kutaja upungufu huo waliobaini mjumbe huyo alisema," Aah! Mwandishi, wewe si unajua upungufu uliomo kwenye Wizara ya Uchukuzi?"

  Hata hivyo, alifafanua kuwa kamati hiyo ilibaini kuwepo kwa upungufu wa kiutaratibu.

  "Kamati ilibaini upungufu wa kiutaratibu kwenye bajeti hiyo, hivyo tumewarudisha wakafanye marekebisho, lakini waje Jumatatu kuendelea kuiwasilisha," alisema mtoa habari huyo.

  Alisema kuwa baada ya kuiwasilishwa kwa taarifa hiyo upya na wanakamati kuipitia hakuna shaka wanahabari watakuwa katika fursa nzuri ya kufahamishwa.

  Mjumbe mwingine wa kamati hiyo alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, mbali ya kukiri kuyakataa mapendekezo hayo, alisema hawezi kueleza zaidi kwa kuwa madili yanambana kwani yeye si msemaji wa kamati.

  "Tulikutana na Wizara ya Uchukuzi, wanahabari hawakuruhusiwa kuingia. Ulichosikia siwezi kukanusha, lakini kimaadili mimi si msemaji. Wewe mtafute mwenyekiti, mimi maadili yananifunga," alisema mjumbe huyo wa Kamati ya Miundombinu.Habari zaidi zinaeleza kuwa Wizara ya Uchukuzi yenyewe imekiri na kuona upungufu huo ikieleza kuwa itayafanyia kazi kama kamati ilivyoagiza na kuiwasilisha tena Jumatatu ya Mei 30.

  Awali, gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM) ili atoe ufafanuzi wa taarifa hizo, lakini baada ya kupokea simu alijibu kirahisi kuwa yupo katika kikao na kuomba atafutwe baadaye.

  Hata hivyo, alipotafutwa tena mara kadhaa baadaye, simu yake iliita bila majibu.
   
Loading...