Kamati ya Uchaguzi TLS imfute Tundu Lissu na Masha kwa kampeni zenye mrengo wa kisiasa

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
37,141
46,411
Baada ya majina yao kuwa nominated kama wagombea wa nafasi ya Urais TLSL, Tundu na Masha wameanza kupiga kampeni mapema, kampeni zenye mrengo wa kisiasa.

Ni hivi karibuni tu wawili hao wamekua wakitoa kauli zenye mrengo wa kisiasa kuelekea Uchaguzi wa TLS na pia wafuasi na mashabiki wa watu hao wenye mrengo wa siasa za upinzani wakipiga kampeni kwa kuuambia uma kuwa ni zamu sasa ya ukawa kuiongoza TLS kwa kuwa kwa muda mrefu ilikua chini ya makada wa CCM.

TLS kama Bar Association ya Tanganyika ni society ya kitaaluma ambayo hushughulika na maswala muhimu ya mawakili, na sheria.

TLS haina afiliation na chama chochote cha siasa wala haijihusishi na siasa.

TLS sio ngo ya maswala ya kupigania haki za raia.

TLS ni jumuiko la kitaaluma.

Hivyo kwa wagombea hao kuanza kampeni zenye zinazoonesha mrengo flani wa kisiasa ni kukengeuka.

Ili kulinda TLS kamati ya Uchaguzi iwaondoe watajwa mara moja katika orodha ya wanaogombea nafasi ya Urais.
 
Yaani kisa ni Lisu tu..!??!
Ama kweli Lissu kiboko,kawatia joto kila kona!
Na azidi kukomaa, hizi figisu hizi ni bure tu, kama vipi na vyama vya upinzani vyote vifutwe basi kwa kuwa vilianzishwa na binadamu..
 
Yaani kisa ni Lisu tu..!??!
Ama kweli Lissu kiboko,kawatia joto kila kona!
Na azidi kukomaa, hizi figisu hizi ni bure tu, kama vipi na vyama vya upinzani vyote vifutwe basi kwa kuwa vilianzishwa na binadamu..


Ukiniuliza mimi na vifutwe kama kuna huo ulazima, kwani nini bhana?
 
Hatuwezi kuwa na serikali na chama imara kama tutakosa taasisi /watu imara wenye kukosa, kuhoji na kudadisi matendo ya serikali na chama. Let Lisu be, let TLS be.

KADA
Lisu tayari anaforum ya Bunge apeleke siasa panapostahili.

TLS itumike kuangalia maswala yanayowahusu wanasheria na sheria zenyewe.
 
Ni kweli kabisa, kila kitu kinaweza kufutwa na wenye mamlaka na wakatokea watu kama wewe kuunga mkono!

Ndio maana ya dunia kuwa na universal indicators za demokrasia na utawala bora...
 
Mi nadhani wapelelezi wa ngada wawe wanapitia na humu. Kupitia michango ya watu wanaweza kabisa kujua nani yuko sober na nani siyo. Mi nimehisi hapa kuna mtu hayuko sober lakini mwenyewe anaona yuko vizuri na ana hoja ya kujadiliwa. My foot!
 
Back
Top Bottom